Trippier atua rasmi athletico Madrid

credit: @sokawaytz_…

✍️ Rasmi, Kieran Trippier amejiunga na Atletico Madrid kwa Mkataba wa miaka mitatu kutoka Tottenham ya Uingereza… Inafahamika kwamba Atletico imelipa £21.7m kama dau la uhamisho wa Beki huyo wa Kimataifa wa Uingereza ambaye alifaulu vipimo vya Afya ndani ya klabu hiyo ya Hispania mapema hii leo Jumatano.

.

– Spurs walipewa fursa ya Kumsajili Mshambuliaji, Angel Correa wakati wa mazungumzo lakini wamechagua kupewa fedha moja kwa moja..Trippier anatoka Tottenham baada ya kucheza Michezo 114 ndani ya misimu Minne..

.

– Muingereza mpya ndani ya Laliga, alikuwepo Patrick Roberts pale Girona kwa mkopo akitoka Man City lakini alitimka na Sasa yupo Norwich City..

#TransferNewsUpdates

@Sokawaytz_

Leave a comment