Magufuli atumia simu ya mkononi kuwapiga picha Kikwete, Rais Ramaphosa

Nchini Afrika Kusini leo Jumamosi Mei 25, 2019 ni siku ya kukumbukwa kutokana na Rais Cyril Ramaphosa kuapishwa kuwa kiongozi wa Taifa hilo kwa muhula wa pili.
Katika hafla ya kuapishwa kwake iliyohudhuriwa na viongozi wa nchini mbalimbali, akiwemo Rais John Magufuli na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kiwete kuliibuka matukio mengi ya kufurahisha.

Moja kati ya matukio hayo ni kitendo cha Rais Magufuli kutumia simu ya mkononi kuwapiga picha Rais Ramaphosa na Kikwete.

Tukio hilo limevuta hisia za watu wengi katika mitandao ya kijamii na kushangazwa na Rais Magufuli jinsi alivyoshikilia vyema simu hiyo na kuwapiga picha wawili hao.
Viongozi hao walionekana kufurahia tukio hilo wakiwemo baadhi ya marais wa mataifa mengine waliokuwa pembeni yao.
Rais Magufuli ameambatana na Kikwete pamoja na makamu mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula nchini Afrika Kusini kuhudhuria sherehe hizo.
Ramaphosa ameapishwa na Jaji Mkuu wa Afrika Kusini, Mogoeng Mogoeng.

Hafla hiyo ilipambwa kwa maonyesho ya ndege za kijeshi zilizorushwa angani na askari waliotua kwa miavuli na kupigwa mizinga ya heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu huyo.

FT : Alliance 1-1 Yanga, mikwaju ya penati 4-3 yaipeleka Yanga nusu fainali

Mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga wametinga nusu fainali ya kombe la FA (ASFC) baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 4-3 kufuatia matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Alliance Fc

Yanga ilitangulia kupata bao la kuongoza kwenye dakika ya 39 likiwekwa kambani na Heritier Makambo kwa kombora la nje ya 18

Alliance Fc iliyokuwa kwenye kiwango bora ilisawazisha bao hilo kwenye dakika ya 62 kupitia kwa Joseph James

Baada ya kumalizika kwa dakika 90 huku matokeo yakiwa 1-1, changamoto ya mikwaju ya penati ikatumika kuamua mshindi

Deus Kaseke, Paulo Godfrey, Thabani Kamusoko na Haruna Moshi ndio waliofunga penati za Yanga wakati Kelvin Yondani na Mrisho Ngasa walikosa

Yanga sasa itachuana na Lipuli Fc kwenye mchezo wa nusu fainali

Jesus Apiga MBILI Bzazil Dhidi Ya Jamhuri YA CZECH

JESUS APIGA MBILI BRAZIL DHIDI YA JAMHURI YA CZECH

MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa yaya Brazil Gabriel Jesus, juzi, aliifungia timu yake mabao mawili ilipopata ushindi wa 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Czech.

Brazil walipata ushindi huo kwenye mchezo muhimu wa kirafi ki ambao Brazil walionyesha kiwango cha hali ya juu sana uwanjani.

Wakati Jesus akifunga mabao hayo staa mwingine wa timu hiyo anayeichezea klabu ya Liverpool, Roberto Firmino, alifanikiwa kuifungia timu yake bao lingine moja.

Czech walianza kwa kishindo mchezo huo baada ya kuanza kwa kuongoza kwa bao lililofungwa na David Pavelka katika dakika ya 37 ya mchezo huo.

Kiungo wa Liverpool, Roberto Firmino aliisawazishia timu yake mapema kipindi cha pili, kabla Jesus hajafunga mabao mawili kipindi cha pili cha mchezo huo.

Brazil wamerejea kwenye ushindi baada ya wikiendi iliyopita kupata sare ya bao 1-1 na Panama.

Mastaa wa Brazil, Firmino, Philippe Coutinho na kipa wa Liverpool, Alisson walionyesha kiwango cha juu sana kwenye mchezo huo.

FT : Simba 2-0 Ruvu Shooting

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wameendeleza wimbi la ushindi katika ligi baada ya leo kuibamiza Ruvu Shooting mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa

Mabao ya Simba yalipatikana kwenye kipindi cha pili yakiwekwa kambani na beki Paul Bukaba (51′) huku bao la pili likifungwa na Meddie Kagere kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 55 baada ya Adam Salamba kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems alifanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake leo akiwapumzisha baadhi ya nyota waliocheza mchezo wa ligi ya mabingwa mwishoni mwa wiki

Aidha bao alilofunga Kagere leo limemfanya afikishe mabao 13 sasa akishika nafasi ya pili nyuma ya Salim Aiyee wa Mwadui Fc mwenye mabao 16

Simba inaendelea kushika nafasi ya tatu ikiwa imefikisha alama 54, alama tano nyuma ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili huku Yanga ikiongoza ikiwa na alama 67

Hata hivyo Azam Fc na Yanga zimecheza michezo saba zaidi ya Simba