Kikosi Rasmi cha TAIFA STARS vs UGANDA

Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Emmanuel Amunike ametaja majina ya wachezaji 25 wanaounda kikosi cha Stars ambacho kitaikabili Uganda Cranes kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019

Miongoni mwa wachezaji waliojumuishwa katika kikosi hicho, Aishi Manula, Jonas Mkude na John Bocco wametoka katika klabu ya Simba

Breaking News: Ephraim KIBONDE wa CloudsFm Amefariki Dunia Leo

Taarifa iliyotufikia muda huu ni kwamba Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde amefariki dunia leo Machi 7, 2019.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amethibitisha kwamba Kibonde amefariki akiwa Mwanza, alianza kusumbuliwa na Presha toka Bukoba kwenye msiba wa Ruge Mutahaba na kuhamishiwa Mwanza.


Aidha, siku chache zilizopita, Clouds Media iliondokewa na mkurugenzi wake wa vipindi, Ruge Mutahaba aliyezikwa nyumbani kwao wilayani Bukoba mkoa wa Kagera.

Soka Updates inatoa pole kwa CLOUDS MEDIA GROUP.

Amunike kutangaza kikosi cha Stars kesho

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itachuana na Uganda March 24 2019 katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za michuano ya AFCON 2019 itakayofanyika mwezi Juni nchini Misri

Kocha Mkuu wa Stars Emmanuel Amunike kesho Ijumaa March 08 anatarajiwa kutangaza kikosi cha Stars

KAGERE: Aibuka Mchezaji BORA | Mwezi Februari | TUZO

Mshambuliaji wa timu ya Simba, Meddie Kagere amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019.

Kagere raia wa Rwanda ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Salim Aiyee wa Mwadui na Salum Kimenya wa Prisons alioingia nao fainali.

Kamati ya Tuzo pia imemchagua Kocha wa Prisons ya Mbeya, Mohamed Rishard kuwa Kocha Bora wa mwezi Februari akiwashinda Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems na Kocha Mkuu wa Mwadui, Ally Bizimungu.