Nafasi ya MANJI kujazwa January 13 2019

Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la soka nchini (TFF) ambayo ilipewa jukumu na BMT ya kusimamia mchakato wa uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi katika klabu ya Yanga, imetangza rasmi kuanza kwa zoezi hilo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ally Mchungahela amesema zoezi la kutolewa fomu kwa wagombea wa nafasi hizo ikiwemo ya Mwenyekiti wa Yanga litaanza rasmi Alhamisi, Novemba 08, 2018

Aidha, Mchungahela ametangaza tarehe ya uchaguzi kuwa ni Januari 13 2019.

Wakati TFF ikitangaza hayo, hali si shwari upande wa klabu ya Yanga ambayo kupitia viongozi wa Matawi wa klabu hiyo, wametangaza kupinga uchaguzi wa timu hiyo kusimamiwa na TFF.

BMT iliipa Kamati ya uchaguzi ya TFF jukumu la kusimamia uchaguzi huo baada ya kubaini Kamati ya uchaguzi ya Yanga ina mapungufu.

Wanachama hao pia walipinga uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wakiutaka uongozi wa klabu hiyo kwanza uwahakikishie kama kweli Mwenyekiti wao Yusufu Manji amekataa kurejea katika nafasi yake.

Nafasi zinazotarajiwa kujazwa kwenye uchaguzi huo ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na nafasi nne za wajumbe wa Kamati ya Utendaj

Leave a comment