Mbabane Swallos yaigwaya SIMBA

Baada ya kupangwa kuanza na mabingwa wa Tanzania Bara, Simba kwenye mchezo wa hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Mbabane Swallows imeonyesha ‘mchecheto’ kuelekea mchezo huo.

Ujumbe ulioandikwa kwenye ukurasa wa mtandao wa Facebook wa timu hiyo unaonyesha kuihofia Simba hasa baada ya kubaini ina wachezaji 10 wanaocheza timu za Taifa

“Tumepangwa na timu kutoka nchini Tanzania, Simba kwenye mchezo wa awali wa michuano ya ligi ya mabingwa,” umesema ujumbe huo.

“Sio ratiba mbaya na lengo letu ni kama msimu uliopita, kufuzu kwa hatua ya makundi”

“Hata hivyo Simba sio timu ya kubeza, ina wachezaji nane kwenye timu ya Taifa. Wanacheza mchezo mzuri na ina washambuliaji wa pembeni wenye kasi”

Mbabane Swallows inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Swaziland, itakuja nchini kati ya Novemba 27-28 kuivaa Simba kwenye uwanja wa Taifa kabla ya mchezo wa marudiano wiki moja baadae huko Uswazi.

Simba inaendelea na maandalizi kuelekea mchezo huo ambapo Ijumaa wiki hii itacheza na mabingwa wa Malawi, Big Bullets kwenye mchezo wa Kimataifa wa kirafiki.

Leave a comment