
credit: @dimbani_leo…
Uongozi wa klabu ya Simba umemtambulisha mshambuliaji Deo Kanda aliyejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja
Kanda anatua Simba kwa mkopo akitokea klabu ya TP Mazembe
Simba imethibitisha usajili wa nyota huyo aliyewahi kuitumikia timu ya Taifa ya DR Congo “Kazi ya kusajili wakali watakaohakikisha kikosi cha Mabingwa kinazidi kuwa tishio kwa wapinzani inaendelea” “Mshambuliaji raia wa Congo DR, Deo Kanda (29) amejiunga na Mabingwa wa nchi. “Kanda amesaini mkataba wa mwaka mmoja kukipiga Msimbazi akitokea TP Mazembe ambapo alikuwa mmoja wa wachezaji ambao waliiwezesha kushinda Ubingwa wa Afrika mwaka 2009, 2010 (aliifungia goli kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Esperance) na 2013 lakini pia akiwa ameshiriki Kombe la Dunia la Vilabu mwaka 2009, 2010, 2013”