credit: @sokawaytz_…
OFFICIAL | Haijalala!! Mara Moja Baada ya kuwasili Nchini jioni hii, Kiungo wa Kimataifa wa Kenya Francis Kahata Amesaini Mkataba wa Miaka Miwili kuitumikia Klabu ya Simba SC.
.
– Kahata mwenye umri wa Miaka 27; Ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kucheza eneo la kiungo, kwasasa akiwa sehemu ya wachezaji wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya, msimu ujao atavaa jezi ya Mabingwa hao Tanzania Bara.
.
– Amejiunga Msimbazi akitokea Gor Mahia ya Kenya ambapo akiwa kwenye klabu hiyo alishinda Kombe la Ligi Kuu mara tatu, kiungo bora wa mwaka wa Ligi Kuu ya Kenya mara mbili na mchezaji bora wa msimu 2018/2019 wa Gor Mahia.
#TPLTransferUpdates