Matokeo ya mechi za leo #Tpl
Category: all
Full Time Fulham 1-2 Chelsea
Full Time
Fulham 1-2 Chelsea
Chambers ⚽ | Higuain ⚽ Jorginho ⚽
#Epl
MATOKEO LIGI KUU LEO FEB 27
Full Time #Tpl


MATOKEO YA MECHI ZA LEO FEB 26
Full Time #Tpl


Droo: Fainali za AFCON 2019 U17
Droo ya upangaji makundi ya michuano ya AFCON kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 imefanyika leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam
Tanzania itakayokuwa mwenyeji wa michuano hiyo, imepangwa kundi A sambamba na Angola, Nigeria na Uganda.
Tanzania itafungua michezo ya kundi A kwa kucheza na Nigeria wakati Angola itapepetana na Uganda wakati upande wa kundi B Guinea itaanza kwa kuchuana na Cameroon huku Morocco ikipepetana na Senegal
Simba 4-1 Mbabane Swallows
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba leo wametakata uwanja wa Taifa baada ya kuwafumua Mbabane Swallows mabao 4-1 kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa hatua ya awali.
Ikicheza kandanda safi na la kuvutia, Simba iliwapoteza kabisa vijana hao wa Uswatini ambao huenda safari ya kuyaaga mashindano haya imewadia.
Nahodha wa Simba John Bocco ndiye aliyeanza kufungua kalamu ya mabao kwenye dakika ya 07 baada ya kufunga bao safi akiunganisha krosi ya Nicolas Gyan.
Mbabane walisawazisha bao hilo kwenye dakika ya 24 mfungaji akiwa Giovane Nzambe aliyefumua shuti kutoka nje kidogo ya 18.
Kwenye dakika ya 32 Bocco aliiongezea Simba bao la pili kupitia mkwaju wa penati baada ya Emmanuel Okwi kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari na mlinda lango wa Mbabane.
Mpaka wakati wa mapumziko Simba ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1.
Kwenye kipindi cha pili Simba ilirejea na kasi iliyomaliza nayo kipindi cha kwanza.
Baada ya kosakosa nyingi, kwenye dakika ya 83 mlinda lango wa Mbabane aliirahisishia Simba kuandika bao la tatu lililowekwa kambani na Meddie Kagere baada ya kipa huyo kuteleza na kushindwa kuondosha mpira aliokuwa amerudishiwa
Hassani Dilunga aliyeingia kwenye dakika za majeruhi alimtengenezea Cletos Chama pasi mpenyezo na bila ajizi ‘CCC’ akaukwamisha mpira kimiani kuiandikia Simba bao la nne katika dakika za nyongeza
Ushindi huo unaiweka Simba katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwani inahitaji sare au isifungwe zaidi ya mabao mawili kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa huko Eswatini wiki ijayo
Tanzani (U23) 3-1 Burundi (U23)
Timu ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 23 imeshindwa kulinda ushindi wa mabao matatu baada ya kuondoshwa katika michuano ya kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019 kwa vijana licha ya ushindi wa mabao 3-1.
Tanzania ilikuwa mbele kwa mabao 3-0 hadi dakika ya 89 kabla Cedric Mavugo mdogo wa aliyekuwa mshambuliaji wa Simba Laudirt Mavugo kuifungia Burundi bao muhimu lililowapa tiketi ya kutinga raundi ya pili.
Mabao ya Tanzania yalifungwa na Habibu Kiyombo (4′), Mbaraka Yusufu (43′) na Kihimbwa (70′)
Tanzania ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi lakini ilishindwa kuzitumia vyema nafasi nyingi ilizotengeneza.
Liverpool 2-0 Fulham : Full Time
Unbeaten Run Continues!! – Magoli ya Shaqiri na Salah yanaipeleka Liverpool kileleni – huku wakiiombea mazuri United dhidi ya City.
MONACO 0-4 BRUDGE
Thierry Henry bado anasubiri ushindiwake wa kwanza tangu ajiunge na Monaco, ameiongoza timu hiyo katika mechi 5 bila ushindi tangu alipotangazwa kuwa kocha wa timu hiyo.
STARS Kujifua Afrika Kusini Siku 10
Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” imeondoka leo alfajiri kuelekea nchini Afrika Kusini kuweka Kambi kujiandaa na mchezo wake wa kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon 2019 dhidi ya Lesotho.
Kambi hiyo ya siku 10 itakuwa katika Mji wa Bloemfontein kabla ya kikosi hicho kuelekea mjini Maseru,Lesotho.
Taifa Stars ipo nafasi ya pili katika kundi L ikiwa na alama 5 nyuma ya vinara Uganda wenye alama 10 wakati Cape Verde wapo nafasi ya tatu wakiwa na alama 4 na Lesotho wakiburuza mkia na alama mbili.
Mchezo dhidi ya Lesotho unataraji kuchezwa Novemba 18,2018 mchezo ambao utatoa taswira ya Taifa Stars kufuzu kucheza Afcon mwakani itakayofanyika Cameroon.










