Mwenyekiti wa Bodi wa Wakurugenzi ya Simba Mohammed Dewji ‘Mo’ amewatoa hofu wapenzi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo juu ya kiungo mkata umeme Jonas Mkude
Mo amesema Mkude ataendelea kubaki Msimbazi
Mkude amekuwa akihusishwa na timu kadhaa ikiwemo klabu ya Yanga inayodaiwa kumuahidi zaidi ya Tsh Milioni 120
“Wanasimba msiwe na wasiwasi, Mkude haendi popote! Jumaah Kareem,” ameandika Mo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
Mkude ni miongoni mwa wachezaji waliomaliza mikataba Simba na alikuwa akisubiri kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Msimbazi