SAMATTA Azidi kuweka Rekodi za KIBABE

Mshambuliaji wa klabu ya KRC Genk na nahodha wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Mbwana Ally Samatta jana amecheza mchezo wake wa 100 katika ligi kuu nchini Ubelgiji, huku timu hiyo ikiendeleza rekodi ya kutopoteza mechi msimu huu baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Royal Excel Mouscron.
Samatta ambaye alianza katika kikosi cha jana, alicheza kwa dakika zote 90 za mchezo licha ya kutofunga bao lolote.

Kwa matokeo hayo, Genk inaendelea kuongoza ligi ya Ubelgiji ikifikisha pointi 35 baada ya kutoka sare mechi tano kati ya mechi 15 ilizocheza, nyingine zote 10 ikishinda. Ambapo sasa inafuatiwa na Club Brugge yenye pointi 31 katika mechi 15 pia na sawa na Antwerp.

MESSI AKABIDHIWA TUZO

Lionel Messi amekabidhiwa tuzo ya mchezaji bora wa la liga na mfungaji bora ⚽2009/10: Magoli 34
⚽2011/12: Magoli 50
⚽2012/13: Magoli 46
⚽2016/17: Magoli 37
⚽2017/18: Magoli 31

Mchezaji bora laliga:
2008–09, 2009–10, 2010–11, 2011–12, 2012–13, 2014–15, 2017–18

SAMIR NASRI IS BACK

SAMIR NASRI IS BACK
:
:
Unakumbuka Samir Nasri lakini? Nauliza mnamkumbuka vizuri? Kule Ufaransa anakumbukwa sana na kashfa yake ya kugoma kumpisha siti Thierry Henry kwenye basi la timu ya taifa. Inasemekana Henry alikuwa na siti yake maalum lakini Nasri alikaidi utaratibu huo kiasi cha kuitwa mtukutu ndani ya timu ya taifa.
:
Sasa anarudi tena EPL. Awamu hii anaeleka West Ham sasa. Taarifa zinasema anakamilisha vipimo vya afya.

Ni baada ya safari ndefu ya maisha ya kusuasua ya kisoka tokea alipoanza kutemwa timu ya taifa na Bwana Didier Deschamps. :
:
Amekumbwa na dhoruba nyingi ingiwemo adhabu ya kufungiwa miezi 18 ya kutokujihusisha na soka baada ya kusadikika kutumia madawa ya kusisimua misuli. :
:

Kwa sasa hana mkataba na klabu yoyote baada ya kuvunja mkataba wa klabu kutoka Uturuki ya Antalyaspor.

Nasri mwenye miaka 31 anatarajia kupokea kiasi ya £80,000.

Hebu fikiria hii West Ham 🇨🇱 Manuel Pellegrini kocha
🇦🇷 Pablo Zabaleta
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Andy Carroll
🇲🇽 Javier Hernandez
🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 Jack Wilshere
🇫🇷 Samir Nasri

Drogba vs Etoo

Drogba 🇨🇮 Vs 🇨🇲 Eto’o

Takwimu ngazi ya vilabu:
🔵DIDIER DROGBA:
Mechi: 686
Magoli: 300
Assist: 114
🕒 48.313 [Goli kila baada ya dakika 161]
:
🔴SAMWEL ETO’O:
Mechi: 700:
Magoli: 353:
Assists: 114,
🕒 Dakika 56.163 [Goli kila baada ya dakika 159]

Takwimu timu za taifa
:
🇨🇮Ivory Coast
Mechi 83, Magoli 57, assists 12
:
🇨🇲Cameroon:
Mechi 88, Magoli 45, assists 5

Wamekutana mechi 14
🔵Drogba alicheza dakika 928
🔴Eto’o alicheza dakika 1117
🔵Drogba: Magoli 3, assist 0
🔴Eto’o: Magoli 6, assist 2

S

uala la makombe sio la mtu binafsi hilo tunaziachia timu husika, ubora wa mtu utabaki palepale hata kama hakutwaa mataji, lakini wakuu mimi nawaachia nyie, unadhani ni yupi alikuwa mchezaji bora kumzidi mwenzake kwa wakati wao?

Full Time: Atlanta 4-1 Inter

Muosha huoshwa, tarehe 12/03/ 2017 Inter iliifumua Atlanta 7-1, leo Atlanta wameibamiza Inter magoli 4-1
:
Serie A on @dstvtanzania
1 – 0 ⚽Hans Hateboer 8′
1 – 1 ⚽Mauro Icardi 47′ p
2 – 1 ⚽Gianluca Mancini 62′
3 – 1 ⚽Berat Djimsiti 88′
4 – 1 ⚽Alejandro Gómez 90+4′

FT : Atalanta 4-1 Inter