#ManchesterDerby – Vikosi vya timu zote vinavyoanza! Pogba OUT! Lukaku anaanzia benchi! Saa 1:30 on @dstvtanzania pekee


#ManchesterDerby – Vikosi vya timu zote vinavyoanza! Pogba OUT! Lukaku anaanzia benchi! Saa 1:30 on @dstvtanzania pekee


Kesho ni mechi ya mabingwa wa kihistoria kutoka Italia. Wanakutana AC Milan wenye idadi ya vikombe 30 na Juventus waliotwaa mataji 54. Ni moja ya mechi kubwa sana ndani ya Italia. Ni miaka 117 imepita tokea vilabu hivi kukutana kwa mara ya kwanza 28 April 1901 [Juventus 2-3 Milan


Mara ya mwisho vilabu vimekutana Juventus 4–0 Milan kwenye Coppa Italia 9 May 2018.
Head 2 head🔃
Mechi 166:
✔️Juventus: Ushindi 63: Magoli 232
✔️Milan: Ushindi 50: Magoli 214
➗Sare: 53
Takwimu
Ushindi mkubwa:
🛑Milan 8-1 Juve (1911–1912)
Magoli mengi mechi 1:
🛑Juve 8-2 Milan (1926–1927)
Ushindi mkubwa kwa Juventus:
💥Juventus-Milan 8–2 (1926–1927)
💥Juventus-Milan 6–0 (1925–1926)
Ushindi mkubwa kwa Milan:
⛔Milan-Juventus 8–1 (1911–1912)
:
Sare zilizozalisha mabao mengi:
🌗Juventus-Milan 3–3 (1930–1931)
🌗Milan-Juventus 3–3 (1946–1947)
Ushindi mkubwa wa Juventus Ugenini:
⛔Milan-Juventus 1–6 (1996–1997)
:
Ushindi mkubwa wa Milan ugenini:
⛔Juventus-Milan 1–7 (1949–1950)

Mabingwa wapya wa klabu bingwa barani afrika ni klabu ya @esperance_sportive_detunis :
🛑Esperance wamefanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa kuwachabanga Al Ahly [3-1]: :
:
🔄Mchezo wa kwanza ulifanyika Misri kwa Al Ahly kushinda bao 3-1 mchezo ambao mwamuzi alillamikiwa sana kwa kufanya maamuzi ya kutatiza kwa kutoa penati ambazo zimelalamikiwa sana.
Huu ni ubingwa wa 3 katika 7 walizocheza:
🎯1994
🎯2011
🎯2018
❌1999❌2000, ❌2010, ❌2012
#ManchesterDerby – Kuelekea mchezo wa Derby ya Jiji la Manchester jumapili hii – tuangalie umuhimu wa Maroune Fellaini ‘Kipenzi cha Jose Mourinho’ katika timu ya United.
:
Fellaini ambaye alikuwa ameumia kwa wiki kadhaa kabla ya kurudi katika mchezo dhidi ya Juventus ambapo alichangia kwa kiasi kikubwa kuirudisha United Uingereza na ushindi vs Juventus.
:
Kocha wa Juventus Massimiliano Allegri alisema hawakuweza kupambana na Fellaini alipoongia – aliwazidi kwenye kucheza mipira ya juu na aliwaletea madhara yaliyoenda kusababisha mashambulizi mengi langoni mwao.
:
Mourinho amekuwa akimzungumzia Fellaini kwa kumuita ‘Plan B’ pindi mipango yake ya mwanzo inapogoma na amekuwa akiisaidia sana United pindi aingiapo dimbani.
:
Takwimu zinaonyesha United inafunga magoli kwa wastani Fellaini anapokuwepo dimbani kuliko ambapo anakuwa hayupo. :
Kuelekea mchezo vs City, United wanamhitaji sana Fellaini awe kwenye kiwango bora kwa maana kiuhalisia United hawawezi kupambana na City kwa kucheza mpira chini – wanahitaji mbinu mbadala na uwepo wa Fellaini kikosini utaongeza ubora wa mbinu ya tofauti ya kuweza kuiletea madhara defence ya City. :
Manchester Derby ya kwanza ya msimu itachezwa jumapili hii majira ya saa 1:30 usiku – itaonyeshwa live kupitia @dstvtanzania pekee
Goli la kwanza la Olivier Giroud chini ya kocha Maurizio Sarri limeisaidia Chelsea kufuzu hatua ya 32 bora kwenye michuano ya Europa League baada ya kupata ushindi dhidi ya Bate Borisov.
Arsenal wamefanikiwa kupita hatua ya makundi ya Europa baada ya kutoka suluhu dhidi ya Sporting CP. Mchezo wa hapo awali uliisha kwa Arsenal kushinda bao 1 kwa nunge bao pekee la Danny Welbeck kule Ureno. Hata hivyo katika mchezo wa marudiano Mshambuliaji huyu Danny Welbeck alipatwa na majeraha mnamo dakika ya 24 na kutolewa nje. :
Msimamo
:
Arsenal mechi 4 alama 10
Sporting mechi 4 alama 7
Poltava mechi 4 alama 3
Qarabag mechi 4 alama 3



Sare waliyopata KRC Genk bado inawafanya waendelee kuongoza Kundi I kwa pointi zao 7 baada ya mechi 4 walizocheza.
Baada ya timu nyingine pia kucheza mechi 4
Sarpsborg-pointi 5
Malmo-pointi 5
Besiktas-pointi 4
DANGOTE AWATOLEA TENA UVIVU ARSENAL.
Tokea mwaka 2015 ilisemekana kuwa Bilionea Aliko Dangote ana ndoto za kuimiliki Arsenal. Yeye anasema ni mshabiki damu damu wa Arsenal na mara kadhaa alikuwa akimkosoa sana meneja wa zamani wa Arsenal Bw Arsene Wenger:
:
Bilionea huyo ameeleza hisia zake kuwa bado ndoto zake za kuinunua Arsenal zipo pale pale. Ingawa amesisitiza kuwa ndoto zake hizi zinaelekea ukingoni. Hata hivyo amesema kuwa kama Arsenal wanaringia ofa yake basi atanunua klabu nyingine:
:
“Naipenda sana Arsenal. Kama hawapo tayari kuiuza basi nitanunua klabu nyingine” :
:
“Mwaka jana nilitangaza wazi kuwa baada ya kukamilika kiwanda changu cha mafuta, mapato yataongezeka mpaka kufikia dola Bilioni 22 hivyo haitaniathiri kiuchumi” :
:
Dangote mwezi agosti mwaka huu alitajwa na na jarida la Forbes kuwa ana utajiri wa Paundi bilion 11.
Katika uwanja wa Giuseppe de Meaza ni mtanange wa 19 kwa Inter kukutana na timu kutoka Hispania.:
🏅Wameshinda 9
🥊Na sare ya leo inatimiza sare ya 9
😥Wamepoteza mmoja
Sare hii ya 1-1 ni mchezo wa pili katika mechi 9 walizokutana kuisha kwa timu zote kufungana magoli [3-1 2011 na mchezo wa leo].
:
:
Barcelona wamefikisha alama 10
Inter wana alama 7.
Barcelona anahitaji alama 1 tu kufuzu huku Inter wakihitaji alama 4 pekee kujihakikisha nafasi ya kufuzu.
Saúl Níguez amefikisha magoli 40 tangu aanze kucheza soka katika ngazi ya vilabu
Atlético Madrid B (8)
Rayo Vallecano (2)
Atlético Madrid (30)
What a talent. 🌟