Ratiba ya mechi ya leo #TanzaniaPremierLeague
Category: michezo
Timu ya Taifa ya Senegal U17 imewasili asubuhi hii
Timu ya Taifa ya Senegal U17 imewasili asubuhi hii tayari kwa mashindano ya Total Afcon U17 yatakayofanyika Tanzania kuanzia Aprili 14-28,2019
credit: @tanfootball
Viporo vya Simba kupangiwa ratiba maalum

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Wambura alisema ratiba ya michezo ya Simba imekuwa na changamoto kutokana na ushiriki wa timu hiyo kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Msimu wa Ligi Kuu 2018/19 unatarajiwa kumalizika May 26 2019 huku Simba, mabingwa watetezi wakiwa bado na michezo 16 ambayo watalazimika kuicheza katika kipindi cha mwezi mmoja na siku kadhaa
“Tutafanyia kazi ratiba ya Simba ili kuhakikisha haiathiri kalenda yetu,” alisema Wambura
“Tutaandaa ratiba maalum kwa klabu ya Simba ili kuhakikisha wanamaliza michezo yao yote bila kuathiri kalenda ya TFF ambapo ligi inapaswa kumalizika mwezi Mei”
Juzi Bodi ya ligi ilisogeza mbele mchezo wa Simba dhidi ya Biashara United ili kuwapa nafasi wawakilishi hao wa nchi wafanye maandalizi ya mchezo wa pili wa robo fainali dhidi ya TP Mazembe
Simba inatarajiwa kuondoka kesho Ijumaa kuelekea DR Congo tayari kwa mchezo huo utakaopigwa uwanja wa TP Mazembe keshokutwa, April 13 2019
Magazeti ya leo, Alhamisi, April 11 2019











PICHA: Man United wapoteza nyumbani dhidi ya Barcelona Champions League
FT: Simba U20 1-1 Cameroon U17
Timu ya vijana leo imetoka sare ya goli 1-1 na timu ya Taifa ya Cameroon U-17 katika mchezo wa kirafiki ambao umepigwa kwenye viwanja vya JK Youth Park. #NguvuMoja
Rais TFF Aomba Kamati ya Taifa Stars kuisaidia SERENGETI BOYS
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya hamasa ya Taifa Stars Paul Makonda kuendelea kuisaidia @serengetiboystz ishinde kupitia Kamati hiyo.
FT: Singida Utd 0-0 Kmc Fc
Mpira umemealizika Singida Utd 0-0 Kmc Fc #TanzaniaPremierLeague
Mazoezi ya mwisho kabla ya kuikabili Kagera Sugar

Mchezo huo utapigwa kesho Alhamisi katika dimba hilo
Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Mwinyi Zahera amesema mazoezi waliyofanya tangu jana yalikuwa ya kuondoa uchovu kwa wachezaji wake
Amesema ana matarajio kuwa vijana wake watakuwa sawa katika mchezo wa kesho baada ya kuwapa mazoezi hayo maalum








Dewji aitabiria Simba nusu fainali ligi ya mabingwa

Dewji amesema Simba ya mwaka huu ni `moto’ na ina uwezo wa kuwang’oa Mazembe kutokana na kuundwa na wachezaji wenye vipaji na ari ya kupata matokeo chanya.
Akizungumza jana mjini Dar es Salaam, Dewji aliyeifikisha Simba fainali za Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) mwaka 1993, alisema kitu pekee kinachopaswa kufanywa na wachezaji na viongozi wa Simba ni kuondoa mchecheto wa mchezo na badala yake kuelekeza nguvu katika mchezo wa marudiano
“Ni kweli Mazembe ni timu ngumu na kongwe. Ukiangalia ina historia kubwa Afrika na ndani ya miaka hii kumi tumeshuhudia ikitwaa ubingwa tofauti wa michuano ya CAF mara tano. Ni rekodi bora sana, lakini pamoja na ubora wao, nikiangalia ubora na uthubutu wa wachezaji wa Simba, naona vijana wetu wanaweza kufanya kweli,” Dewji amenukuliwa na Bin Zubeiry
“Wachezaji wa sasa wa Simba nawafananisha na wale wa enzi zile tunafika fainali CAF.
“Walikuwa wanajituma sana uwanjani. Na hawa ukiwaangalia wana kila kitu kinachoweza kuwaduwaza Mazembe kwao.
“Angalia walivyowakimbiza hapa Dar es Salaam, kwa kawaida Mazembe si wa kujiangusha hivyo, lakini uliona katika mchezo wa kwanza, walizidiwa sana ila bahati haikuwa kwa Simba.
“Na hata hao wanaobeza penalti ya John Bocco watambue Simba hii ni moto wa kuotea mbali na usishangae kuona mpira umetangulia Lubumbushi na wachezaji wanakwenda kumalizia kazi ya kuandika historia zaidi kwa soka ya Tanzania,” alisema
Akizungumzia tukio la klabu hiyo kupinga kubadilishiwa mwamuzi wa mchezo wa marudiano dhidi ya Mazembe, alisema jambo hilo litawarejesha mchezoni wachezaji, lakini pia kuongeza umakini wa waamuzi katika mchezo huo.
“Hata kama CAF hawatabadilisha uamuzi huo, mwamuzi aliyepangwa (Janny Sikazwe wa Zambia) atakuwa makini zaidi na kizuri ni kwamba hatataka kuharibu sifa zake zilizomwezesha kuchezesha michuano karibu yote mikubwa duniani.
“Amechezesha Kombe la Dunia mara mbili, Kombe la Mataifa ya Afrika mara mbili, pia fainali za Klabu Bingwa ya Dunia, achilia mbali hii michuano ya klabu Afrika,” alisema Dewji aliyewataka Watanzania kuendelea kuwaunga mkono wawakilishi hao wa taifa.
Katika mchezo wa kwanza mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, timu hizo hazikufungana, hivyo kuzifanya timu zote kuwa na nafasi ya kusonga mbele hatua ya nusu fainali, matokeo ya mwishoni mwa wiki yakiwa mwamuzi wa mwisho.











