Beki wa klabu ya Simba Sc Erasto Nyoni ameitwa kunako kikosi cha timu ya Taifa kuchukua nafasi ya Andrew Vicent anaesumbuliwa na majeraha tayari kwa mchezo wa Jumapili March 24 dhidi ya Uganda
Category: michezo
Ibenge aivulia kofia Simba

Vita Club ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Simba na kuondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ikiiacha Simba ikitinga robo fainali
Akizungumza baada ya mchezo jana, Ibenge alisema Simba ina wachezaji wazuri
Aidha, Ibenge alifichua kuwa walimuwekea ulinzi mkali Meddie Kagere kwa kuwa ndio mchezaji waliokuwa wakimuhofia zaidi
“Simba walionyesha ushindani mkali kwetu, walicheza vizuri matokeo waliyopata walistahili, tunawapongeza,” amesema
“Kagere ndio mchezaji tuliyekuwa tunamuhofia zaidi na niliwaagiza wachezaji wangu wamchunge lakini mwisho wa siku mpira ni mchezo wa makosa, tumefanya makosa tumeadhibiwa”
Mabao ya Simba yalifungwa na Mohammed Hussein na Clatous Chama aliyefunga bao la ushindi katika dakika za lala salama
Magazeti ya leo, Jumapili, March 17 2019












Matokeo ya Mechi za leo Tpl


Ratiba Ya Mechi Za Leo TPL


RATIBA Ya Mechi Za Leo KUNDI D


MAGAZETI Ya Leo March 16











SIMBA SC: Mazoezi ya mwisho kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya AS Vita Club.
📸: Mazoezi ya mwisho kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya AS Vita Club. #CAFCL #DoOrDie #NguvuMoja ✊🏽







MATOKEO: Mechi Za Leo Ligi Kuu Tanzania Bara




Manara amtahadharisha Zahera
Zahera ameonekana akiambatana na viongozi wa timu ya Vita Club itakayochuana na Simba hapo kesho
“Hii ni mechi ya kitaifa na ya kimataifa, tunaiwakilisha nchi, kuna kocha yeye kazi yake imekuwa ni kuzunguka na Vita tu na aliaga anaenda kwao Congo hata Iringa hajaenda.
“Hii ni mechi ambayo nchi inajua, Rais anajua, sasa ole wake aendelee kutuharibia mipango,” amesema Manara kwenye mahojiano yake na eFM radio
Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Manara amesema kikosi kiko tayari, ari na morali ya wachezaji iko juu kuelekea mchezo huo
Amewataka mashabiki kuwahi mapema uwanja wa Taifa hapo kesho ili wawe sehemu ya historia ambayo Simba imepania kuiandika









