







Vinara wa ligi hiyo Yanga wao watashuka dimbani mkoani Iringa kesho Jumamosi kuikabili Lipuli Fc katika mchezo ambao matokeo ya ushindi yatazidi kuin’garisha timu hiyo kileleni

Jana jioni Simba ilijifua katika uwanja wa Taifa yakiwa ni maandalizi yake ya mwisho katika uwanja huo kabla ya mchezo hapo kesho
Aussems amesema licha ya kuwa tayari wamefikia malengo ya msimu huu ya kutinga hatua ya makundi, lakini wana nafasi adimu ya kutinga robo fainali kama watashinda mchezo huo utakaopigwa mbele ya mashabiki wake takribani elfu 60
“Mimi nipo sawa na hata wachezaji wangu wapo vizuri, ni mechi yenye msisimko sana tunajua tukishinda tutaingia robo fainali na tumesubiri jambo hili kwa miezi 7 sasa,” amesema
“Hata kama matarajio hayakuwa makubwa sisi kufika mbali kwenye ligi ya mabingwa Afrika, lakini bado tuna nafasi kwa hiyo hatuna presha, zaidi presha ipo kwao (AS Vita) kwa sababu ni wanafainali wa kombe la shirikisho mwaka jana na kama hawatafuzu itakuwa jambo baya sana kwao.”
“Hatupo katika hali inayofanana, chochote kitakachotokea ni ziafa kwetu, tuna nafasi adimu ya kucheza mchezo huu muhimu mbele ya mashabiki 60,000 kwa hiyo itakuwa mechi nzuri na wachezaji wapo tayari.”
Mchezo huo utapigwa saa moja usiku sambamba na mchezo kati Al Ahly dhidi ya JS Saoura
Good Morning Mtu wangu wa nguvu leo March 15, 2019, nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za za nyuma za Magazeti ya Tanzania.














Mzee Akilimali amewaomba wadau wa Yanga na Watanzania wote kwa ujumla wamuombee ili aweze kupona maradhi yanayomsumbua
“Hali yangu sio nzuri. Niko huku Bagamoyo najiuguza maradhi ya kisukari. Mniombee kwani kisukari kinanitesa sana,” Mzee Akilimali amenukuliwa na Spoti Xtra
Mzee Akilimali ni miongoni mwa wanachama wa Yanga vinara wa kutoa maoni juu ya masuala mbalimbali ya klabu hiyo
Wakati mwingine hujikuta akiingia katika mgogoro na wanachama wenzake, wakimtuhumu kuwa ni mpinga maendeleo.
Kikosi cha As Vita Club tayari kipo nchini baada ya kuwasili jana Jumatano usiku tayari kwa mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Klabu bingwa Afrika dhidi ya Simba Sc Jumamosi hii Marchi 16





Djuma aliyewahi kuhudumu Simba akiwa kocha msaidizi kwa misimu miwili, amesema Simba itakayokuwa nyumbani ina kila sababu ya kushinda mchezo huo Jumamosi
“Timu zinazoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu zimetumia vyema viwanja vyao vya nyumbani. Naamini Simba itatumia uwanja wake vizuri pia,” Djuma aliiambia Radio eFM
Djuma aliondolewa Simba mwezi Oktoba mwaka jana baada ya kutofautiana na kocha Mkuu Patrick Aussems.
Nafasi yake tayari imechukuliwa na kocha Denis Kitambi
Djuma anabaki kuwa miongoni mwa makocha waliopita Simba na kukubalika sana na mashabiki wa timu hiyo

















Kikosi cha Yanga Sc kinatarajia kuondoka jijini Dar Es Salaam leo Asubuhi kuelekea mkoani Iringa tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Lipuli Fc utakaopigwa Jumamosi hii March 16 katika uwanja wa Samora mkoani humo.

Simba iliyorejea jana kutoka Algeria inajifua kwenye uwanja wa Boko Veterans

Nyoni na Okwi hawakusafiri na Simba ilipokwenda nchini Algeria kumenyana na JS Saoura kutokana na kuwa majeruhi
Wachezaji hao leo wamejumuika na wachezaji wengine wakihusika katika program zote za mazoezi hivyo kuongeza matumaini kuwa wako tayari kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi