Kocha Mkuu Rwanda Atangaza kikosi KAGERE ndanii NIYONZIMA NJE

– Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Rwanda, Mashami Vicent muda huu ametangaza Kikosi cha timu hiyo ya Taifa “Amavubi” kitakachoivaa Jamhuri ya Afrika ya kati Katika Mechi ya kuwania kucheza Fainali za mataifa ya Afrika “AFCON” Mwakani nchini Cameroon, Rwanda watacheza Mchezo huo Novemba 18 mwaka huu Katika Uwanja wa “Stade De Huye”.
.
– Kikosi kamili alichoita kocha Mashami Vicent kinajumuhisha nyota 27 Ambao wanaingia kambini Novemba 08, wakiwemo Washambuliaji hatari Meddie Kagere kutoka Simba SC ya Tanzania, Dany Usengimana kutoka Terasan ya Misri na Jacques Tuyisenge kutoka GOR Mahia ya Kenya, Katika viungo kuna nyota kama Niyonzima Olivier kutoka Rayon Sports, na Bizimana Djihad kutoka Waasland Beverin ya Ubelgiji na Mukunzi Yanick kutoka Rayon Sports bila kumsahau Iranzi Jean Claude kutoka APR FC.
.
– Na Kwa Mara ya kwanza baada ya Miaka 11 Kiungo Haruna Niyonzima ametemwa Katika Katika Kikosi hicho, Ikumbukwe Niyonzima anacheza soka la kulipwa nchini Tanzania Katika Klabu ya Simba SC.
.
– KIKOSI KAMILI NI.
.
🔸WASHAMBULIAJI: Medie Kagere (SC Simba, Tanzania), Tuyisenge Jacques (Gor Mahia, Kenya), Hakizimana Muhadjiri (APR FC), Usengimana Danny (Terasan, Egypt), Shema Tresor (Torhout 1992km FC, Belgium), Mico Justin (Sofapaka, Kenya), Nshimiyimana Amran (APR FC), Kalisa Rashid (SC Kiyovu) & Mushimiyimana Meddy (Police FC).
.
🔸VIUNGO… Niyonzima Olivier (Rayon Sports FC), Mukunzi Yannick (Rayon Sports FC), Bizimana Djihad (Waasland Beveren, Belgium), Buteera Andrew (APR FC), Niyonzima Ally (AS Kigali), Iranzi Jean Claude (APR FC), & Rubanguka Steve (Patromaasmeshelen, Belgium)
.
🔸MABEKI: Nirisarike Salomon (AFC Tubize, Belgium), Rwatubyaye Abdoul (Rayon Sports FC), Rugwiro Herve (APR FC), Manzi Thierry (Rayon Sports FC), Fitina Ombolenga (APR FC), Imanishimwe Emmanuel (APR FC), Rutanga Eric (APR FC) & Rugirayabo Hassan (Mukura VS).
.
🔸MAKIPA: Kimenyi Yves (APR FC), Bashunga Abouba (Rayon Sports FC) na Rwabugiri Omar (Mukura VS). – Instagram

CAF Awards 2018 Vipengere vyote

– Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” limetoa vipengele vinavyowaniwa tuzo za mwaka huu Kwa Mashindano Mbalimbali yaliyofanyika “CAF Awards 2018”, Hivi ndivyo vipengele vilivyotajwa baada ya kukaliwa kwa kikao jijini Dakar nchini Senegal..
.
.
1. African Player of the Year (Mchezaji Bora Afrika wa Mwaka).
2. Women’s Player of the Year (Mchezaji Bora wa mwaka kwa Wanawake Afrika).
3. Youth Player of the Year (Mchezaji Bora Kijana wa Mwaka Afrika).
4. Men’s Coach of the Year (Kocha Bora wa mwaka Afrika wa Kiume).
5. Women’s Coach of the Year (Kocha Bora wa mwaka Afrika wa kike).
6. Men’s National Team of the Year (Timu Bora ya Taifa Kwa Wanaume ya mwaka).
7. Women’s National Team of the Year (Timu bora ya Taifa Kwa Wanawake ya mwaka).
8. Goal of the Year (Goli Bora la Mwaka).
9. Africa Finest XI (Kikosi Bora Afrika Cha Mwaka).
.
👉 Kipengele cha Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa kiume na wa Kike, kura zake zitapigwa na..
– Kamati ya Ufundi ya CAF na Waandishi wa Habari za Michezo.
– Wachezaji wakongwe wa Afrika (Legendary).
– Makocha wa Vilabu waliozifikisha timu Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho na Klabu Bingwa Afrika, Makocha wa timu za Taifa zote 54 member wa CAF na Manahodha wake.
.
👉 Kipengele Cha Tuzo ya Mchezaji bora kijana, Kocha Bora wa kiume wa Mwaka, Kocha Bora wa kike wa mwaka, timu ya taifa bora ya mwaka ya Kiume na ya Kike, kura zake zitapigwa na..
.
– Kamati ya Ufundi ya CAF na Waandishi wa Habari za Michezo.
– Wachezaji wakongwe wa Afrika (Legendary).
– Makocha Ambao wamevifikisha Vilabu hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na Klabu Bingwa Afrika.
– FIFPro itatolewa kulingana na uwezo wa mchezaji alioonesha kwa mwaka ndio ataingia kikosi Bora cha Afrika.
– Goli Bora la Mwaka litapigiwa kura, lenye kura nyingi ndio litatangazwa kuwa bora.
.
– Ili kuwa mshindi wa tuzo hizo ni kulingana na kiwango bora zaidi kuanzia Mwezi February 2018 Mpaka mwezi November 2018.
.
– Sherehe ya kutangaza washindi wa tuzo hizo kulingana na kura pamoja uteuzi Kwa mwaka huu 2018 zitafanyika Siku ya Jumanne ya January 08,2019 nchini Senegal ndani ya jiji la Dakar. – Instagram

DELE ALLI:Aongeza Mkataba Tottenham

– Kiungo wa timu ya Taifa ya England, Dele Alli amesaini mkataba mpya wa miaka Sita (6) Kuendelea kuichezea Klabu yake ya Tottenham Mpaka mwaka 2024..
.
– Dele Alli Alijiunga na Spurs mwaka 2015 akitokea MK Dons, na tokea hapo akawa ni Mmoja wa Wachezaji bora Barani Ulaya chini ya kocha wake Mauricio Pochettino.
.
– Tokea ajiunge na Klabu hiyo ya London amefanikiwa kufunga Magoli 48 na Assist 41 Katika mechi 153 akiwatumikia farasi weupe.
.
– Tottenham wanawaongeza Mikataba mipya Wachezaji wao Wote Ambao ni tegemeo, kabla ya Alli walitoka kumpa Mkataba mpya Mshambuliaji wao Hary Kane ambaye alisaini mwezi juni mkataba unaofikia kikomo mwaka 2024 pia Spurs walimuongeza mkataba wa miaka mitano kocha wao mkuu Mauricio Pochettino..
.
– Spurs Sasa wanahakikisha wanawafunga Wachezaji wao muhimu Kwa Mikataba ya muda mrefu kabla ya kufikia mwaka 2019 na ndio mwaka Ambao wataamia rasmi Katika Uwanja wao wa White Hart Lane uliokuwa Katika ukarabati wa Kuongeza ukubwa ambapo kwasasa wanatumia Uwanja wa Taifa “Wembley Stadium”

Real Madrid : Kocha Mpya

– Real Madrid wanamtaka kocha mkuu wa Tottenham, Mauricio Pochettino mwenye umri wa miaka 46 kuwa kocha wao mpya baada ya kumtimu Julen Lopetegui hapo jana.
.
– Madrid wanatarajia kumtangaza kocha mpya kabla ya Kumalizika mwezi ujao wakati Kwa Kipindi hawatokuwa na kocha timu hiyo Itakuwa chini ya Santiago Solari ambaye ni kocha wa Real Madrid B “Castila”.
.
– Lopetegui alitimuliwa hapo jana baada ya Matokeo mabovu ya Klabu hiyo akidumu Kwa miezi minne na nusu tu Ndani ya Bernabeu – Sasa Madrid wanatafuta kocha mpya na tayari kuna majina matatu ya makocha wanaotajwa kuja kuifunza klabu hiyo ambao kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte, kocha wa Sasa wa Tottenham Mauricio Pochettino na kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ubelgiji, Roberto Martinez.. Instagram @Lugoyah_sports

SAMATTA : Azidi Kuipaisha GENK

– Mbwana Samatta amefunga bao wakati klabu yake ya KRC Genk ikitoka sare ugenini ya bao 1-1 dhidi Standard de Liege katika Ligi Kuu ya Ubelgiji.
.
– Mchezo unawafanya Genk kufikisha mechi 12 msimu na zote hawajapoteza mchezo hata Mmoja, wametoka sare Mara tatu na kushinda mechi Tisa (9) na ndio vinara wa Ligi Kuu Nchini humo wakiwa na pointi 30 – Pointi tatu zaidi na wanaishika nafasi ya pili ambao ndio mabingwa watetezi Club Brugge.

RONALDO: Sababu za Kuihama Real Madrid

– Mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo amesema kuwa aliihama Real Madrid na kujiunga na miamba hiyo ya Italia kwa sababu rais wa klabu hiyo ya Hispania, Florentino Perez hakumfanya ajihisi kuwa mchezaji anayethaminiwa Santiago Bernabeu.
.
– Ronaldo mwenye umri wa miaka 33, amesema kuwa Perez alikuwa akimtazama kwenye mahusiano ya kibiashara zaidi na hicho ndicho anachotambua hivyo kila alichomuambia kilikuwa hakitoki moyoni mwake.
.
– ”Perez alikuwa akinitazama mimi kwenyemahusiano ya kibiashara zaidi na hicho ndicho ninachofahamu hivyo kila alichokuwa akiniambia kilikuwa hakitoki moyoni mwake,” amesema Ronaldo… – Raia huyo wa Ureno ameongeza, “Nilisikia ndani ya klabu, hasa kutoka kwa rais mwenyewe kwamba hawakunichukulia mimi sawa na vile walivyofanya wakati nakuja kwenye miaka minne au mitano iliyopita.”
.
– “Rais alikuwa akinitazama, macho yake yakitoa tafsri ambayo haiyendani na kile anachozungumza, kiasi kwamba sikuwa na nafasi tena kwao. Kama unaelewa ninachomaanisha, hicho ndicho kilichonifanya kufikiria kuondoka.”
.
– “Wakati mwingine nilikuwa nikitazama habari, namna wanavyozungumza nilijiuliza kuhusu kuonda. Ni machache tu kati ya hayo lakini ukweli ni kwamba rais asingelinizuia nisiondoke,”
.
– “Kama yote ingekuwa nafanya kwaajili ya pesa basi ningekwenda China mahala ambapo ningeweza kupata fedha nyingi kuliko hata Juve au Real. Sikuja Juve kwasababu ya fedha ningepata sawa tu na Madrid kama siyo zaidi.”
.
– “Tofauti ni kwamba Juve, ni kweli wananihitaji wamekuwa wakiniambia hivyo na nikaamua kuliweka sawa kwasababu wamenithibitishia.’ Alisema Cr7.
.
– Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo amejiunga na klabu hiyo ya Serie A akitokea Real Madrid ya Hispania mapema kabla ya kuanza Kwa msimu huu.

NDEGE ya mmiliki wa Leicester city Yapata AJALI

BREAKING NEWS: Ndege ya mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha imeungua baada ya kugonga pembezoni mwa uwanja wa King Power Stadium.

Mashuhuda wanasema ndege hiyo aina ya Helikopta iliyumba wakati inajiandaa kuondoka kisha ikalipuka.

Mpaka sasa hakuna taarifa kuhusu waliokuwamo ndani. Inasemekana mtoto wa bosi huyo ndiye aliyekuwa akiitumia ndege hiyo mara kwa mara. Tukio hili limetokea mara baada ya mchezo kati ya Leicester City na West Ham kukamilika [1-1]. Bosi huyo wa Leicster ana Utajiri wa ÂŁ5 bilioni. Taarifa pia zinadai huenda bosi huyo alikuwamo ndani ya ndege hiyo.

Juventus 2-1 Empoli

Juventus wanatimiza pointi 28 baada ya michezo 10 – Cristiano Ronaldo akiwapa ushindi dhidi ya Empoli
.

Cristiano Ronaldo ndani ya Serie A :
.
.
. ⛳Mechi 10…. âš˝Magoli 7…. 🎯 4 assists.

Mchezaji bora wa mechi mara 8 🥉