LIPULI FC INADAIWA ZAID YA TSH. 60M

LIPULI INADAIWA ZAIDI YA TSH. 60M
:
Lipuli FC ipo katika wakati mgumu baada ya kukumbwa na deni la zaidi ya Tsh. 60m kutoka kwa wadau walioisaidia wakati ikiwa ligi daraja la kwanza.
:
Deni hilo limedumu tangu mwaka 2015 ambapo mahakama iliamuru Lipuli iwalipe wadai wake lakini imeendelea kukaidi.
:
Wakili wa wadai amesema: “Wateja wangu wamekuwa na madai dhidi ya timu ya Lipuli ya Iringa. Timu hii ilikuja kuweka kambi mjini Mafinga mwaka 2015, walikaa pale karibu mwezi mzima na waliomba huduma ya chakula kutoka kwa Tunte na huduma ya malazi kutoka kwa Ernest Lusangira.”
:
“Walitoa ahadi kwamba watalipa baada ya muda lakini hawakufanya hivyo wakaondoka na deni ambalo wamekuwa nalo hadi leo.”
:
“Walipaswa kumlipa mama huyu (Tunte) pamoja na kesi zai ya Tsh. 33m kwa upande wa Lusangira walipaswa kumlipa zaidi ya Tsh.30m. Walipelekewa amri ya mahakama ya kulipa deni hilo lakini wakakaidi.”
:
Wakili huyo amesema kutoka na klabu ya Lipuli kukaidi kulipa deni, amepeleka ombi mahakama itoe amri ya kuwakamata viongozi ambayo tayari wameipata kwa hiyo viongozi wa Lipuli wanaweza kukamatwa wakati wowote.
:
Kaimu mwenyekiti wa klabu ya Lipuli Ayubu Kiwelo amesema hawezi kuzungumza chochote hadi atakapokutana na wahusika.
:

“Tunaambiwa ni deni la mwaka 2015, sisi tumeingia madarakani mwaka jana mwezi wa 7 na hukumu ilitolewa mwezi wa 6 mwaka jana kabla hata hatujaingia madarakani kwa hiyo siwezi kuongea chochote juu ya hilo hadi tukunae na wahusika kujua deni hilo lipoje”-Kiwelo.

CHELSEA NA ARSENAL JIPANGENI

KUNDI B:
CHELSEA NA ARSENAL MJIANDAE KUMPOKEA HARY KANE

Tottenham msimu UCL wanaelekea kupoteza dira. Wana alama 1 tu. Msimu uliopita katika michezo 6 walishinda 5 na kutoka sare mmoja. Tena walifanya maajabu kwa kumfunga Real Madrid aliyekwenda kutwaa ubingwa mabao matatu. Katika michezo 6, walishinda mabao matatu katika michezo minne.

Msimu huu katika michezo mitatu wanadaiwa mabao matatu. Wamefunga mabao matano wameruhusu manane. Aibu. Hili kundi bado ni gumu sana kwa Inter pamoja na Tottenham katika kupata nafasi ya kusonga mbele.

Tottenham mchezo ujao anakutana na PSV, Tottenham wanapaswa kushinda mchezo huo ili angalu wafikie alama 4. Inter anazo alama 6. Inter ana wakati mgumu kidogo kumfunga Barcelona akiwa kwake ingawa anahitaji hata sare. Inter kama watafungwa watabakiwa na alama zao 6 kama atashinda watapa alama 9 na hii itakuwa balaa zaidi kwa Tottenhan. Lakini faida kubwa waliona nayo Inter watawakaribisha PSV vibonde nyumbani. Hapo watahitaji alama 3 ili wafikishe alama 9. Wakati huo Tottenham atakuwa Camp Nou kama wakifanikiwa kutoka salama basi wakatoe sadaka.

Safari ya Tottenham kufuzu inatiwa dosari na shimo la Camp Nou. Mbaya zaidi Inter watawasubiri Barcelona Guissepe de Meazza kwa hiyo uwezekano wa kuambiwa sare upo. Faida pekee wanayotegemea Tottenham ni mchezo wao wa mwisho na Inter kwenye uwanja wao wa nyumbani. Kwa mawazo yangu Tottenham yupo kwenye wakati mgumu zaidi na bila shaka Chelsea na Arsenal wote kwa pamoja kwa mikono miwili wampokee ndugu yao kutoka London. Hivyo wajiandae kisaikolojia kumkaba Harry Kane.

#UCL Tottenham #hawatoboiii

UEFA : PSG wakiendea hivi Hawatoboi

KUNDI C:
PSG WAKIENDELEZA MPIRA WAO WA KUPAKA PODA HAWATOBOI

Liverpool alama 6, Napoli alama 5, PSG alama 4. Hivi Neymar ataficha wapi sura yake na pesa zote zile alizonunuliwa takribani Paund 222M kama ikitokea wametolewa hatua ya makundi?

Kama kuna kundi gumu mwaka huu basi hili kundi ni la kukata na shoka. Huyu Napoli kama Masikhara vile anaweza akashangaza wengi licha ya kutopewa nafasi kabisa. Tusishangae kuona hawa matajiri wakirudi mtaani kwao kucheza na watoto wenzao huko league 1.

Nahisi mchezo ufuatao wa Napoli na PSG ndio utakaotoa dira haswa kwamba tuendelee kusubiria mvua iishe au tutoke na mwamvuli.

Nafasi ya PSG kusonga mbele bado ipo, Nafasi ya Napoli vivyo hivyo, Liverpool ndo kwanza yupo kilele.

Mpaka sasa PSG na Barcelona ndio timu zilizofunga mabao mengi [10] kwa hiyo lolote laweza kutokea. PSG wana mchezo wa marudiano dhidi ya Liverpool pale Parc des princess nahisi kwa mchezo waliocheza mechi iliyopita kama hawatabadilika basi wanaweza kupigwa nje ndani, lakini Napoli watakaribishwa Anfield. Najiuliza hapa inawezekana Napoli wakatibua vibe lote la Majogoo pale Anfield kweli? Napoli mpaka sasa katika mechi 3 wamefunga mabao 3, bado kwa takwimu hizi ni ngumu sana kumwekea dhamana kupata ushindi pale Anfield kirahisi.
Mechi iliyobakiwa kwa PSG kukata tiketi ni Belgrade ambayo nina amini hata kama itachezwa Kinesi PSG atashinda sio chini ya bao 3.

Uwezekano wa yeyote kati ya Liverpool na PSG au Napoli kutolewa bado upo wazi hasa ukitazamia wote wamepishana alama 1 tu huku michezo ikibakia mitatu.. #UCL Ila hapa PSG wakiendeleza ubishoo #hawatoboiii

Arsenal 1-0 Sporting CP

#EUROPA2018/19

Arsenal wamefanikiwa kupata ushindi Ugenini wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Sporting CP bao pekee la Danny Welbeck mnano dakika ya 77. .
.

Welbeck sasa anakuwa mchezaji wa kwanza wa Arsenal kuifunga timu ya Ureno ugenini ambaye jina lake la pili sio Campbell .
.
.
⚽ Danny Welbeck (2018/19)
⚽ Sol Campbell (2009/10)
⚽ Kevin Campbell (1991/92)

Samatta Azidi Kung’ara KRC GENK

SAMATTA Ameweka wavuni mara mbili na kutengeneza bao moja. Genk sasa wanaongoza kundi wakiwa na alama 6 baada ya kushinda michezo miwili na kupoteza mmoja. .
.
Kufikia sasa Genk imefunga mabao 7 na kuruhusu matano. Samatta amecheza mechi 8 za Europa na kufunga mabao 9 [Hatua ya makundi na kufuzu] .
.
.
.
Katika hatua ya Makundi Samatta ana mabao matatu kwenye mechi 3. .
Kufikia hivi sasa Samatta amehusika katika magoli 11 katika michezo 8 [Magoli 9 na asisst 2 .

Takwimu za Jumla za Samatta msimu huu amehusika magoli 18 kwenye michezo 18. [Magoli 16 na assists 2]
Mpaka sasa Samatta amehusika mabao 63 katika michezo 130, [Mabao 50 na Asissts 13].

Sasa Samatta ni miongoni mwa wafungaji waliowahi kufikisha mabao 50 ndani ya klabu ya Genk.

Mbwana Samatta ndiye mfungaji bora namba 6 wa klabu ya Genk

Mbwana Samatta ndiye mfungaji bora wa Genk kutoka bara la afrika 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
#Hainakufeli #Sokaupdates