Crescentiua Magori: CEO Simba SC

Klabu ya Simba ambayo imeingia rasmi kwenye mfumo mpya wa uendeshaji wa kampuni, imemtangaza Crescentius Magori kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa kampuni ya Simba Sports Club.

Magori ametangazwa kuwa CEO wa SSC katika Mkutano Mkuu wa klabu hiyo unaoendelea Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, Posta jijini Dar es salaam.

Magori amewaahidi wanachama wa klabu ya Simba kuwa ataifanya klabu hiyo kuwa ya kisasa

Amesema ataifanya Simba kuwa klabu yenye mafanikio sio Tanzania tu, bali Afrika nzima

KICHUYA: Arejeshwa TAIFA STARS

Shirikisho la soka nchini (TFF) limeweka hadharani Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachotarajia kucheza mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Lesotho Novemba 18,2018 Mjini Maseru,Lesotho.

Kiungo wa Simba Shiza Kichuya amerejeshwa katika kikosi hicho na kocha Emmanuel Amunike baada ya kukosa mchezo uliopita

Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Jonas Mkude na John Bocco pia wameitwa.

YANGA 1-1 NDANDA FC

Yanga imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ndanda Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa uwanja wa Taifa.

Ndanda Fc ilitangulia kufunga bao la kuongoza kwenye dakika ya 16 mfungaji akiwa Nasor Hasimu baada ya timu hiyo kufanya shambulizi la kushitukiza.

Yanga ilirejea mchezoni kwenye dakika 24 ilipofanikiwa kusawazisha kwa bao la kichwa lililofungwa na kiungo Jaffar Mohammed aliyeichezea yanga kwa mara ya kwanza leo kwenye ligi

Bao hilo lilitokana na mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajib aliyerejea kwenye kikosi cha Yanga leo baada ya kukosa michezo miwili iliyopita akisumbuliwa na maumivu ya mgongo

Ndanda iliyocheza kwa kujihami zaidi, ilitumia mashambulizi ya kushitukiza ambayo mara kwa mara yalipelekea hatari langoni kwa Yanga na kumlazimu mlinda lango Beno Kakolanya kufanya kazi ya ziada

Kwenye kipindi cha pili Yanga ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi na kupeleka mashambulizi mfululizo langoni kwa Ndanda lakini kukosekana umakini kwa safu ya ushambuliaji iliyoongozwa na Heritier Makambo kuliikosesha Yanga mabao

Matokeo hayo yanaibakisha Yanga katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi licha ya kuwa na alama 26 sawa na Simba inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao.

Banka Afungiwa miezi 14 soka

Kamati ya Kuzuia na Kupambana na Dawa Zisizoruhusiwa Michezoni ya Kanda ya Tano Afrika ( RADO ) imetoa hukumu ya kumfungia mchezaji wa Yanga, Mohamed Issa ‘Banka’ kutokana na matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo alisema Banka amefungiwa miezi 14 kwa kukutwa na hatia hiyo.

Anasema Banka amekuwa na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu aina ya bangi akiwa nchini Kenya.

“Banka alikutwa na hatia hiyo akiwa pale Machakos Kenya katika mashindano ya CECAFA Challenge Cup na kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar, ” alisema.

“Hukumu yake hiyo itaanzia Desemba 9, 2017 ambapo alichukuliwa kwenda kufanyiwa vipimo na itamalizika Februari 2, 2019.

“Banka baada ya kupimwa alikubali kweli alitumia kwa kupitia kwa maandishi yaani barua na baada ya kukutwa na hatia ilitakiwa kufungwa maisha lakini baada ya kukubali alipunguziwa.

“Banka atakiwi kufanya mazoezi ya mbeli ya watu lakini kama atatumikia vizuri adhabu hiyo miezi miwili ya mwisho ataruhusiwa kufanya mazoezi na timu yake, ” alisema.

BANGI Yampozna kiungo wa Yanga Afungiwa Miezi 14

Kamati ya Kuzuia na Kupambana na Dawa Zisizoruhusiwa Michezoni ya Kanda ya Tano Afrika ( RADO ) imetoa hukumu ya kumfungia mchezaji wa Yanga, Mohamed Issa ‘Banka’ kutokana na matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo alisema Banka amefungiwa miezi 14 kwa kukutwa na hatia hiyo.

Anasema Banka amekuwa na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu aina ya bangi akiwa nchini Kenya.

“Banka alikutwa na hatia hiyo akiwa pale Machakos Kenya katika mashindano ya CECAFA Challenge Cup na kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar, ” alisema.

“Hukumu yake hiyo itaanzia Desemba 9, 2017 ambapo alichukuliwa kwenda kufanyiwa vipimo na itamalizika Februari 2, 2019.

“Banka baada ya kupimwa alikubali kweli alitumia kwa kupitia kwa maandishi yaani barua na baada ya kukutwa na hatia ilitakiwa kufungwa maisha lakini baada ya kukubali alipunguziwa.

“Banka atakiwi kufanya mazoezi ya mbeli ya watu lakini kama atatumikia vizuri adhabu hiyo miezi miwili ya mwisho ataruhusiwa kufanya mazoezi na timu yake, ” alisema.

AJIBU kurejea Jumapili dhidi ya NDANDA FC

Mratibu wa klabu ya Yanga Hafidh Saleh amesema kiungo Ibrahim Ajib huenda akarejea kikosini kwenye mchezo wa Jumapili ijayo dhidi ya Ndanda Fc.

Ajib sambamba na Papi Tshishimbi wamekosa michezo miwili iliyopita dhidi ya KMC na Lipuli kutokana na kuwa na matatizo mbalimbali.

Wakati Ajib akisumbuliwa na maumivu ya mgongo, Tshishimbi alikuwa na matatizo ya goti.

Wawili hao walishindwa kutumika kwenye mchezo wa jana licha ya ripoti ya daktari kubainisha utimamu wa afya zao.

Yanga imefanikiwa kushinda michezo yote miwili waliyokosa viungo hao mahiri hivyo kudhihirisha kuwa timu hiyo haitegemei mchezaji mmoja tofauti na inavyodhaniwa na mashabiki wa timu pinzani

Kocha YANGA: Hakuna Mchezo Rahisi

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewapongeza vijana wake kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa jana.

Zahera amesema licha ya timu yake kuibuka na ushindi mwembamba amefurahishwa na upambanaji unaoendelea kuonyeshwa na wachezaji kwenye michezo mbalimbali ya timu hiyo

Amesema kwenye kila mchezo lengo lao la kwanza ni kuibuka na ushindi bila ya kujali idadi ya mabao watakayofunga.

Awapasha waandishi wa habari swala la Ajib

Katika hatua nyingine Zahera amewataka waandishi wa habari kulinganisha taarifa zao na sio kuandika kwa lengo la kufanya uchonganishi

Zahera amesema waandishi wa habari wamekuwa wakiandika zaidi ‘ukosoaji’ wake kwa baadhi ya wachezaji bila ya kuandika mazuri yao

“Nilisema Ibrahim Ajib ni mchezaji mwenye akili nyingi ya mpira kuliko wachezaji wenu wote hapa Tanzania, lakini sikuona mkiandika hilo”

“Mmekuwa mkiandika yale ya kukosoa tu ambayo nayo kimsingi ni ya kumjenga yeye ili awe mchezaji mkubwa,” amesema

Yanga imepanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 25, alama mbili nyuma ya Azam Fc.

Liverpool vs Cardiff City Leo: HAPATOSHI

LIVERPOOL vs CARDIFF CITY.

– Liverpool Ambao ndio vinara katika Msimamo wa Premier League wakichuana vikali na Mabingwa Watetezi Manchester City, Wikendi ya leo watakuwa nyumbani Anfield Kuwaalika Cardiff City. .
πŸ‘‰ Takwimu zao (head to head).
– Liverpool na Cardiff hawajawahi kukutana tokea msimu wa 2013-14 katika Premier League – Liverpool walishinda mechi zote, 3-1 ndani ya Anfield na wakashinda 6-3 ugenini.
.
– Mara ya mwisho Cardiff kushinda mechi Dhidi ya Liverpool katika ligi ni December 1959, Raundi ya pili waliipiga Liverpool 4-0 ndani ya Anfield, majogoo chini ya kocha Bill Shankly mwaka huo waliishia Nafasi ya tatu PL.
.
– Kuna Magoli matatu au zaidi hufungwa timu hizi zinapokutana Katika mechi 10 zilizopita, jumla zimefungana Magoli 45 Katika Mashindano yote kwenye hizo mechi 10.
.
– Liverpool wamepoteza mechi Moja tu Katika mechi 45 zilizopita wakiwa home Katika Dhidi ya timu zilizotoka kupanda Daraja (W35 D9), kipigo Pekee ni Dhidi ya Blackpool msimu wa 2010-11 – lakini wameshinda mechi zote saba chini ya kocha Jurgen Klopp ndani ya Anfield, wamefunga Magoli 21-2.
.
– Liverpool wamepoteza mechi Moja tu kati mechi 49 wakiwa home katika Premier League Dhidi ya timu Zinazoishia na β€˜City’ (W30 D18), kipigo pekee kutoka kwa Swansea City January 2017.
.
– Cardiff wamepoteza mechi 14 Kati ya 15 Dhidi ya Vilabu vya “big six” Katika Premier League (D1), wameruhusu kufungwa magoli mawili na kuendelea kwenye mechi 12 Kati ya hizo 14.
.
– Magoli matatu na Assist tatu, Mshambuliaji wa Liverpool Mohammed Salah amehusika Katika Magoli Sita kwenye mechi tano zilizopita Dhidi ya timu zilizotoka kupanda Daraja.
.
– Kocha wa Cardiff Neil Warnock akiwa Kama kocha mkuu amekutana na Liverpool Mara Nne ugenini na zote kapokea kipigo na timu aliyo iongoza haijafunga Goli hata Moja – Pia Kafungwa na makocha tofauti Souness, Houllier, Benitez ba Dalglish.
.
– Mlinda lango wa Liverpool, Alisson anatafuta kuweka rekodi ya kuwa kipa wa pili wa Liverpool Katika historia yq Premier League kuwa na clean sheets 7 kwenye mechi 10 alizoanza msimu huu baada ya Jose Reina (7). Alisson Ana Clean Sheets 6 Katika mechi 9 Mpaka Sasa..

UCHAGUZI: SIMBA SC

Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa bodi ya Simba Hussein Kitta amesema endapo atafanikiwa kuchaguliwa, jambo la kwanza itakuwa ni kuwaelewesha wanachama juu ya mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo.
:
KWA NINI AMECHUKUA FOMU KUGOMBEA?

Wakati umefika kwa sababu nimekuwa nikifatilia masuala ya mpira kwa siku nyingi, nimekuwa kiongozi kwenye makundi madogomadoo kama tawi la Simba Makini, baada ya haya mabadiliko ya mfumo nimeona unaendana na fikra za Simba Makini nimeona naweza ku-fit kwenye mfumo wa sasa.
:
ATAIFANYIA NINI SIMBA?

Mambo ya kufanya ni mengi, pamoja na kutoa mchango wangu katika masuala ya mpira yapo zaidi ya mpira ambayo mimi nina uwezo nayo kwa sababu ya taaluma yangu. Kitaaluma mimi ni mwanasheria ni mhadhiri wa sheria chuo kikuu cha Dar es Salaam.
:
Kazi ya kwanza kabisa ni kuelewesha wanasimba juu ya huu mfumo mpya kwa sababu ukimsimamisha mtu barabarani ukamuuliza kuhusu huu mfumo atashindwa kukujibu kwa hiyo natakiwa kuhakikisha watu wanaelewa ili yanayokwenda kufanyika waelewe yanafanyika kwa sababu ya mfumo mpya.
:
Kule kwenye bodi ndio ambapo mikakati mikubwa inapangwa sehemu ambayo mwelekeo wa klabu na shughuli zake unatengenezwa kwa hiyo nakusudia nitakapokuwa pale kupitia uzoefu wangu katika masuala ya mpira na taaluma yangu nitavichanganya pamoja ili vitusaidie kuijenga Simba imara.
:
Anakuja mwekezaji Mohammed Dewji anaweka bilioni 20, ile bodi itakuwa na watu mchanganyiko watu kutoka upande wa klabu na wengine kutoka upande wa mwekezaji. Sitegemei mtu aweke bilioni 20 halafu alete watu dhaifu kwenye bodi kwa hiyo ninaamini nina uwezo wa kuwawakilisha wanachama wa Simba kwenye bodi katika kusimamia maslahi yao kwa hoja ambazo naweza kuzisimamia.
:
SERA ANAYOINGIA NAYO

Naingia na sera ya kufanya kazi pamoja na wenzangu wa bodi kwa maslahi ya wanachama ambao wamenichagua.
:
Simba sasa hivi inakuwa kampuni (Simba Sports Club LTD) kampuni huwa zinakuwa na malengo ambayo tayari yameandikwa kwenhe document ya kuanzisha kampuni, kwa hiyo nitahakikisha nayasimamia malengo yote lakini pia kuna wanachama ambao wamenituma na Simba ina historia yake ambayo hiki chombo kimpya kinachokuja kitahakikisha pamoja na mabadiliko, haipotezi kule ilikotoka.

Simba Vs KMC : Mchezo wa sogezwa mbele

Bodi ya Ligi imesogeza mbele mchezo wetu na KMC ambao ulikuwa umepangwa kuchezwa tarehe 8/11/2018 ili kupisha maandalizi ya timu ya Taifa (Taifa Stars). Pia bodi imetangaza kwamba mchezo wetu na Lipuli FC ambao ulisogezwa mbele sasa utachezwa tarehe 21/11/2018 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.