Habari za Michezo na Burudani zilizopamba kurasa za mbele na nyuma za Magazeti ya leo Ijumaa Novemba 23 2018
Category: michezo
Sababu za ZAHERA: Kutomtumia AJIBU
Kocha mkuu wa klabu ya @yangasc Mwinyi Zahera amefunguka kuhusiana na kutomtumia mshambuliaji wake Ibrahim Ajibu katika mchezo wa leo dhidi ya Mwadui Fc.
.
.
Kocha huyo amesema hakuridhishwa na mahudhurio ya nyota huyo wakati yeye akiwa kwenye majukumu ya kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Congo akiwa kama kocha msaidizi.
.
.
Aliongeza kuwa kila siku kocha msaidizi wa Yanga alikuwa akimtumia majina ya wachezaji wote ambao walikuwa hawafiki mazoezini na Ajibu hakuhudhuria siku 4 hivyo ni bora afungwe akiwa ametumia wachezaji wanaofuata kile anachoagiza kuliko kucheza ambao hawana nidhamu. .
.
Mchezo huo umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 huku nyota wake muhimu Ibrahim Ajibu na Deus Kaseke wakishuhudia mechi hiyo Jukwaani
.
#sokaonlineUpdates
Msimamo wa Ligi kuu Tanzania
Msimamo wa ligi baada ya mechi za leo #tanzaniapremierleague🇹🇿

Kikosi cha Yanga vs Mwadui Fc
1. Klaus Kindoki
2. Paulo Godfrey
3. Gadiel Michael
4. Abdallah Shaibu
5. Andrew Vicent
6. Feisal Salum
7. Mrisho Ngasa
8. Maka Edward
9. Amissi Tambwe
10. Heritier Makambo
11. Jaffar Mohammed
SUB
Ramadhani Kabwili
Juma Abdul
Cleofas Sospeter
Raphael Daudi
Thabani Kamusoko
Yusuf Mhilu
Matheo Anthony
Ratiba Ya Mechi za Leo Nov 22
Ratiba ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara leo #tanzaniapremierleague🇹🇿 #sokao Updates

YANGA: Kulipa kisasi Leo dhidi ya Mwadui
Baada ya kufungwa bao 1-0 msimu uliopita kwenye uwanja wa CCM Kambarage, Leo Yanga inashuka tena katika uwanja huo kusaka alama tatu muhimu.
Changamoto zilizoikumba Yanga mwishoni mwa msimu uliopita zilipelekea kupoteza mchezo dhidi ya Mwadui Fc uliopigwa May 19 2018 ukiwa ni mchezo wa tatu Yanga kufungwa mfululizo baada ya pia kufungwa na Prisons na Mtibwa Sugar.
Wakati huo Yanga ilikwenda Shinyanga ikiwa na wachezaji 13 tu wa kikosi cha kwanza kilichoongozwa na aliyekuwa kocha msaidizi Shedrack Nsajigwa.
Lakini hali ni tofauti msimu huu ambapo Yanga iko mkoani humo ikiwa na kikosi chake kamili sambamba na kocha wake Mwinyi Zahera
Ni mchezo ambao Yanga inahitaji kuibuka na ushindi ili kulinda rekodi yake ya kutofungwa lakini pia kujiimarisha katika mbio za kuwania ubingwa ikikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa timu za Azam Fc na Simba
Tangu kuanza kwa msimu wa 2018/19 Yanga haijapoteza mchezo wowote katika ligi na hata michezo ya kirafiki.
Kikosi hicho cha Zahera kimeweka rekodi ya kipekee kikiwa kimecheza karibu miezi mitatu bila ya kufungwa kinyume na matarajio ya wale waliokuwa wakibeza.
Mara ya mwisho Yanga kufungwa ilikuwa August 28 kwenye mchezo wa mwisho wa kombe la shirikisho hatua ya makundi dhidi ya Rayon Sport nchini Rwanda ambapo Yanga ilifungwa bao 1-0
Yanga imecheza michezo 10 kwenye ligi bila ya kupoteza ikishinda michezo nane na kutoka sare michezo miwili.
Inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 26 sawa Simba lakini Yanga ikiwa imecheza michezo pungufu
Kabwili,Ninja Kuongeza Nguvu Shinyanga | Yanga vs Mwadui
Mlinda lango Ramadhani Kabwili, walinzi Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Godfrey Paulo ‘Boxer’ wametua mkoani Shinyanga kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Yanga kinachoshuka uwanja wa CCM Kambarage leo kuumana na Mwadui FC.
Wachezaji hao walikuwa kwenye timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 23 ambayo juzi iliondoshwa kwenye michuano ya kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019 kwa ngazi ya vijana licha ya kushinda kwa mabao 3-1 dhidi ya Burundi baada ya kufungwa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza.
Kuwasili kwa wachezaji hao, kumeongeza nguvu kwenye kikosi cha Yanga ambacho kitawakosa nahodha Kelvin Yondani na mlinda lango Beno Kakolanya ambao hawakusafiri kwa sababu binafsi.
Yanga imedhamiria kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo ili kuendeza rekodi ya kutofungwa msimu huu pia kuendeleza presha kwa wapinzani wake katika mbio za ubingwa, Azam fc na Simba
MICHEZO: Magazeti Ya Leo Nov 22
MICHEZO: Magazeti Ya Leo Nov 21
Lipuli yazidi kujinoa vs Simba
From @officiallipulifc TIMU ya Lipuli Fc leo imefanya mazoezi ya mwisho ikiwa nyumbani kabla ya kesho kuanza safari kwenda Dar kwa ajili ya kuikabili Simba SC tarehe 23 Ijumaa. Mchezo huo awali ulipangwa kuchezwa tarehe 21. #tanzaniapremierleague🇹🇿 #sokaonlineUpdates










































