Habari za Michezo na Burudani zilizopamba kurasa za mbele na nyuma za Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 28 2018.
Category: michezo
Mtibwa sugar 4-0 Dynamo
Mtibwa Sugar imeanza vyema michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) baada ya kuilaza Northern Dynamo kutoka Shelisheli kwa mabao 4-0.
Jaffar Kibaya amefunga mabao matatu ‘hat-trik’ kwenye mchezo huo huku bao la nne likifungwa na Riphat Msuya
Matokeo hayo yameiweka Mtibwa Sugar katika nafasi nzuri ya kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo ambapo wiki ijayo itasafiri kwenda Shelisheli kurudiana na timu hiyo.
Kesho Jumatano itakuwa zamu ya mabingwa wa Tanzania Bara, Simba ambao watashuka kwenye dimba la Taifa kuikabili Mbabane Swallows kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa(CAF CL), hatua ya awali
Mashabiki wa Simba na Watanzania wazalendo wanausubiri kwa hamu mchezo huo ambao matokeo ya ushindi yatahitajika zaidi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga raundi ya kwanza kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa huko Uswatini wiki ijayo
Mashabiki wa Yanga Wajitokeza Kuisapoti MTIBWA
Idadi kubwa ya mashabiki wa Yanga wameungana na Watanzania wengine waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam kuipa sapoti Mtibwa Sugar inayochuana na Northern Dynamo kutoka Shelisheli katika mchezo wa kombe la Shirikisho hatua ya awali.
Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0, Jaffar Kibaya akifunga mabao matatu ‘hat-trik’ huku bao la nne likifungwa na Riphat Msuya
Baadhi ya mashabiki wa Yanga wameingia uwanjani na mabango yanayobainisha kuwa uzalendo huo utaishia kwa Mtibwa Sugar leo tu lakini kwa siku ya kesho, Simba watapambana na hali yao!
Simba itashuka dimba la Taifa kesho Jumatano kuumana na Mbabane Swallows katika mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa.
Kama ilivyo kwa mashabiki wa Simba ambao hushangilia timu pinzani zinapokuja kuchuana na Yanga, kwa uzoefu uliopo, hali itakuwa hivyo hivyo kwa upande wao kesho kwa mashabiki wengi wa Yanga kuiunga mkono Mbabane Swallows.
Simba vs mbabane swallows
Watanzania na Wanasimba wote wameaswa kufurika kwa wingi Uwanja wa Taifa kesho kuishangilia Simba itakapokuwa ikiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali.
Simba itachuana na Mbabane Swallows kutoka Uswatini katika mchezo unatarajiwa kuanza saa kumi jioni.
Ni mchezo ambao Simba inahitaji kuibuka na ushindi mnono ili kuwa katika nafasi nzuri ya kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo
Mchezo wa marudiano baina ya timu hizo utapigwa huko Uswatini (zamani Swaziland) wiki ijayo.
MICHEZO: Magazeti ya leo Nov 27
Orodha ya Wafungaji Ligi Kuu TANZANIA


Orodha ya Wafungaji Ligi Kuu TANZANIA


SIMBA: Mbabane Swallows wametuponza vs Lipuli
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema mawazo ya mchezo wa ligi ya mabingwa kwa wachezaji wake, yamechangia wasifanye vizuri kwenye mchezo wa jana dhidi ya Lipuli fc.
Jana Simba ililazimishwa suluhu ya bila kifungana na Lipuli Fc kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa uwanja wa Taifa.
Aussems amesema wachezaji wake walitekwa na mawazo ya mchezo wa ligi ya mabingwa utakaopigwa Jumatano ijayo dhidi ya Mbabane Swallows
“Tulipoteza umakini leo, nadhani wachezaji wangu walitekwa zaidi na fikra za mchezo wa ligi ya mabingwa,” amesema Aussems
Aussems anaamini matokeo ya jana hayataathiri morali ya kikosi chake kuelekea mchezo huo muhimu utakaopigwa Jumatano ijayo kwenye uwanja wa Taifa
Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Nov 23
Msimamo wa Ligi baada ya mechi ya leo #tanzaniapremierleague🇹🇿


YFF: Mambo Atakayoanza nayo NINJE
MAMBO ATAKAYOANZANAYO NINJE.
.
Mkurugenzi wa ufundi TFF Ammy Ninje amesema ataanza kufanyia kazi vitu vitatu vya msingi, falsafa ya mpira wetu, kuongeza makocha wenye sifa kufundisha ligi yetu ya juu, na kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni.
:
“Kitu cha kwanza nataka kutengeneza philosophy ya mpira wa Tanzania, sisi tunataka tucheze mpira wa aina gani kwa sababu wamepita walimu wengi tangu miaka ya 1980 lakini hadi leo hatuna philosophy . Nadhani hiyo ni sababu kubwa kwa nini watazania hatufanikiwi.”
:
“Tunaelekea vizuri ukiangalia timu zetu za U20 na U17 lakini tunakwama kwa sababu vijana hawapewi nafasi kwenye vilabu vyao, hicho kitu nitakisisitiza sana vijana wa U20 wacheze kwenye vilabu vyao.”
: “Kwenye club licence nitasisitiza kuwa na academies nimeshakuja na program, kwa sababu mimi nimekaa kwenye academies karibu miaka 12 naomba vilabu walete ushirikiano niwasaidie.”
:
“Nadhani tuna walimu 7 kati ya timu 20, kwangu mimi sio kitu kizuri na majukumu yangu mimi ni kuwasaidia walimu wazawa ili tupate walimu wazuri watakaofundisha timu zetu.”
:
“Wakati nipo South Africa 1996 tulikuwa na wachezaji watano wa kigeni, watatu wanaanza wawili wanakaa kwenye benchi kwa hiyo ongezeko la wachezaji wengi wa kigeni nitalikataa nataka watano kwa kuanza kwa hiyo watu wanaofikiria kusajili wachezaji wengi katika dirisha hili dogo walifikirie hilo”


























