


Category: usajili
Yanga wanasa chuma kingine Rwanda

– Klabu ya Yanga SC imefikia Makubaliano ya kuingia Mkataba wa Miaka Miwili na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda, Issa Bigirimana.
.
– Bigirimana Mzaliwa wa Burundi lakini anaitumikia timu ya taifa ya Rwanda, amemwaga wino wa Mkataba wa Miaka Miwili kuwatumikia Miamba wa Mitaa ya Jangwani akitokea katika Klabu ya APR FC ya Ligi Kuu Nchini kwao Rwanda.
.
– Bigirimana 23, anakuwa Mchezaji wa Pili kusinyaa Baada ya Jana, Kiungo Ambaye Pia ni wa Rwanda kutoka Klabu ya Mukura Victory, Patrick Sibomana kumwaga wino.. Haya yote ni kuijenga Yanga mpya ya Ushindani kwa msimu ujao 2019/20..
#transfers #Updates
@Sokawaytz
credit: @sokawaytz

Kiungo wa zamani wa Barcelona xavi awa kocha mkuu wa al sadd sc nchini quatar

– Kiungo wa zamani wa Klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Xavi Rasmi ametangazwa kuwa kocha mkuu wa Klabu ya ligi Kuu nchini Qatari , Al Sadd SC kwa Mkataba wa Miaka miwili.
.
– Xavi 39, amecheza game zaidi ya 100 akiwa na Al Sadd kabla ya kutangaza kustaafu mwishoni mwa msimu wa 2018-19, Miaka Mitatu tangu ajiunge na Klabu hiyo.
.
– Xavi, katwaa Ubingwa wa Kombe La Dunia 2010 akiwa na Hispania, Mataji Nane ya Laliga, Mataji Manne ya Champions League Kipindi akiwa na FC Barcelona… 👏👏👏
#Updates
@Sokawaytz
credit: @sokawaytz
Usajili ulaya




Adi Yusuf mchezaji wa kitanzania aliyesajiliwa blackpool uingereza

– Blackpool imefanya usajili wake wa kwanza Dirisha hili La Uhamisho kwa kumnasa Mshambuliaji waKimataifa wa Tanzania, Adi Yussuf. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amesaini mkataba wa miaka miwili na Kipengele cha kuongeza mwaka mwingine kuwa Mitatu; Hii imekuja baada ya mkataba wake na Klabu ya Solihull Moors kumalizika.
.
– Katika Kipindi chote cha Mwaka Mmoja na Nusu akiwa na klabu hiyo ya Daraja la tano, Alifunga mabao 21 katika mashindano yote ya Klabu hiyo.. Amejiunga na Blackpool inayoshiriki League One sawa na Daraja La tatu katika mfumo wa Mzima wa Ligi Nchini Uingereza.
.
– Akiongea Baada ya “kusinyaa” Amesema.
— “Hii ni ndoto ya kweli kwangu.” “Jitihada zangu na kufanya kazi kwa bidii, hatimae mafanikio yangu yameonekana, natoa shukrani kwa kila mtu aliyeniamini na kwa kila mmoja ndani ya Solihull, “Ninataka tena kuwa na uhusiano na kila mtu Kipindi nitakacho kaa hapa.”.
— “Nilipoweza kufanya kazi katika Solihull. Nina hakika niweza kufanya kazi katika Ligi hii” Aliongeza Yussuf.
.
– Yussuf alianza kusakata Soka katika Timu ya Pili ya Leicester City, na Mpaka anajiunga na Blackpool, katimiza jumla ya vilabu 14 tofauti katika vilabu vyote hivyo timu 5 alicheza kwa mkopo. Nyota huyo anatarajia kutua nchini Moja kwa Moja ataingia kambini katika timu ya taifa ya Tanzania kwa Maandalizi ya AFCON 2019..
#Updates #transfers
@Sokawaytz
credit: @sokawaytz

Dondoo za usajili ulaya



Yanga yakamilisha usajili wa kiungo mnyaruanda Patrick papy sibomana

✍🏻 Kumekucha Jangwani, Klabu ya Yanga SC Imekamilisha Usajili wa kiungo wa Kimataifa wa Rwanda, Patrick Papy Sibomana kwa Mkataba wa Miaka Miwili akitokea Klabu ya kwao Rwanda, Mukura Victory.
:
✍🏼 Sibomana 22, Aliwahi kuitumikia Klabu ya APR FC ya kwao Rwanda, mwaka 2017 akasaini Mkataba wa kuitumikia Klabu ya Shakhtyor Soligorsk ya Nchini Belarus kisha kurejea Rwanda mwaka huu na kutua Mukura na kisha Sasa Yanga SC ya Tanzania.
:
✍🏼 Nyota huyu ni Miongoni mwaka Wachezaji wanaounda timu ya taifa ya Rwanda “Amavubi” akiichezea timu hiyo tangu mwaka 2013 mpaka Sasa, Kafunga Magoli mawili na Moja ya Goli lake aliifunga Taifa Stars katika Mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki Tanzania ikipoteza 2-0 mwaka 2015 ndani ya Dimba La Amahoro Stadium, Kigali..
#Updates #transfers
@Sokawaytz
credit: @sokawaytz

Klabu ya Arsenal yainyemelea saini ya goalkeeper wa Ac Milan Gianluigi Donnarumma kurithi mikoba ya Peter Cech

Klabu ya Arsenal imeanza kuwania saini ya Golikipa wa Ac Milan Gianluigi Donnarumma ili kurithi mikoba ya Peter Cech aliyetangaza kustaafu baada ya fainali ya Europa League (Daily Star)
credit: @sokaonline_
Adrian Rabiot kwenda liverpool


Tetesi za usajili ulaya leo














