Kikosi ambacho kitaanza leo dhidi ya TP Mazembe.

Kikosi ambacho kitaanza leo dhidi ya TP Mazembe. #CAFCL #YesWeCan #NguvuMoja

Kila la kheri Simba, hiki hapa kikosi kinachoanza mchezo dhidi ya TP Mazembe

1. Aishi Manila

2. Zana Coulibaly

3. Mohammed Hussein

4. Erasto Nyoni

5. Paschal Wawa

6. James Kotei

7. Haruna Niyonzima

8. Jonas Mkude

9. John Bocco

10. Meddie Kagere

11. Clatous Chama

SUB

Deogratius Munishi

Juuko Murshid

Emmanuel Okwi

Mzamiru Yassin

Hassani Dilunga

Adam Salamba

Rashid Juma

Mohamed Salah amerudi tena, ukame wa mabao fyekelea mbali

Usiku wa April 5 2019 club ya Liverpool ya England iliendeleza harakati zake za kupambani Kombe la Ligi Kuu England kwa kucheza dhidi ya Southampton, Liverpool walikuwa ugenini katika mchezo huu na presha ilikuwepo kutokana kuwa na utofauti mdogo sana kati yao na Man City wanaoongoza Ligi timu hizo mbili zinapocheza mchezo wake wa Ligi na wapinzania tofauti zinauona kama fainali.

Liverpool iliingia uwanjani na staa wao Mohamed Salah akiwa kacheza mechi 9 mfululizo pasipo kufunga goli kiasi cha wengi kutabiri kuwa ndio kamaliza msimu, bahati ilikuwa kwa Liverpool ambao walipamba na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-1, magoli ya Liverpool yakifungwa na Keita dakika ya 36, Mohamed Salah dakika ya 80 na Henderson dakika ya 86.

Southampto goli lao la mapema dakika ya 9 lililofungwa na Long halikuwasaidia na kuambulia kuona point tatu zikienda Liverpool, baada ya Mohamed Salah kufunga goli la leo anavunja rekodi yake ya kucheza mechi 9 mfululizo bila kufunga goli lolote, hivyo unaweza kusema Mohamed Salah kwa sasa amemaliza ukame wa magoli.

UWANJA WA UHURU

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangala wakiongozana na viongozi wengine wa Wizara na TFF, leo wametembelea ukarabati wa uwanja wa Uhuru ambao utatumika Kama uwanja wa mazoezi kwenye michuano ya Total Afcon U17 itakayofanyika kuanzia Aprili 14-28, 2019 Tanzania ikiwa mwenyeji..

Mazoezi ya mwisho kabla ya kuivaa TP Mazembe

Kikosi cha Simba leo jioni kimefanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Boko Veterans kabla ya kuikabili TP Mazembe kesho Jumamosi katika mchezo wa robo fainali michuano ya ligi ya mabingwa

Katika mazoezi hayo yaliyosimamiwa na kocha Patrick Aussems, ari ya wachezaji imeonekana kuwa juu, wakionyesha utayari wa mchezo huo