Naibu Spika akataa ombi la wabunge kukatwa posho kuichangia Yanga

Naibu Spika wa Bunge, Dk.Tulia Ackson, amekataa ombi la Mbunge wa Nkasi, Ally Kessy (CCM) kuhusu wabunge kukatwa sehemu ya posho zao kuichangia Klabu ya Yanga.

Baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali bungeni mjini Dodoma asubuhi ya leo, mbunge huyo alisimama na kuomba mwongozo wa Kiti cha Spika, wabunge wakatwe Sh. 100,000 kila mmoja katika posho yao ya leo ili kuichangia klabu hiyo inayokabiliwa na ukata.

Hata hivyo ombi hilo lilikataliwa na Naibu Spika baada ya wabungwe waliokuwa wengi kupinga hoja hiyo

Wanayanga wameendelea kufanya juhudi za kuichangia timu yao ili kuiwezesha kupita salama katika kipindi cha mpito

Yanga yarejea Dar kutoka Mtwara, kuunganisha Mwanza kesho

Kikosi cha Yanga kimewasili salama jijini Dar es salaam leo kikitokea mkoani Mtwara ambapo jana kililazimishwa sare ya bao 1-1 na Ndanda Fc

Vinara hao wa ligi kuu wanatarajia kukwea pipa kurejea mkoani Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya African Lyon

Mchezo huo utapigwa April 08 katika uwanja wa CCM Kirumba

Dk Kigwangala mgeni rasmi mchezo wa Simba vs TP Mazembe

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla atakuwa mgeni rasmi wa mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba dhidi ya TP Mazembe

Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi, April 06 2019 katika uwanja wa Taifa saa kumi kamili jioni

Dk Kigwangala ambaye ni mdau mkubwa wa klabu ya Simba ataungana na maelfu ya mashabiki wa timu hiyo ambao kesho watafurika kuujaza uwanja wa Taifa ili kushuhudia mtanange huo

Kagere, Chama hawaendi kokote – Mo

Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji ‘Mo’ amesema wachezaji Meddie Kagere na Clatous Chama wataendelea kubaki Msimbazi kwa kuwa timu hiyo inawahitaji kufikia malengo yake ya kupata mafanikio makubwa kwenye soka la Afrika

Simba inadaiwa kuwa na ofa nyingi mezani kutoka kwa vilabu vikubwa barani Afrika kutaka huduma za wachezaji hao ambao wamekuwa chachu ya mafanikio ya kikosi cha Simba hasa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu huu

“Simba bado tunajenga timu, Meddie Kagere na Clatous Chama bado wanamikataba, ni kweli Simba tunahitaji pesa lakini tunahitaji ushindi na mafanikio kuliko pesa,” amesema Mo

“Kwa mwaka huu bonus tutakazotoa kwa wachezaji zitafika zaidi ya Billion 1. Mara nyingi unaweza kuona tumejaza uwanja lakini asilimia kubwa ya hizo pesa zinakwenda kwenye bonus za wachezaji kama tungefikiria pesa zaidi hizo bonus tungeshusha lakini sisi tunataka tuwape ari zaidi wachezaji wetu ili tupate mafanikio zaidi.”

“Kwa hiyo kwa hao wachezaji wawili mimi sio kocha lakini naimani kocha atataka kuendelea nao, kwa hiyo itakuwa ngumu kuwatoa Simba labda iwe kwa bei kubwa sana ili sisi tuweze kupata wachezaji wengine, hiyo itakuwa ni habari nyingine.”

Mo awaita mashabiki ‘kwa Mkapa’ kushuhudia kipigo cha TP Mazembe

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mohammed Dewji ‘Mo’ amewataka mwashabiki wa Simba na wazalendo wote wa soka nchini kujitokeza kwa wingi kesho katika uwanja wa Taifa wakati mabingwa hao wa nchi wakipepetana na TP Mazembe katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mo amesema kikosi cha Simba kimefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo, sehemu iliyobaki ni ya mashabiki kujitokeza kwa wingo uwanjani ili kuwaongezea wachezaji morali ya ushindi

“Tumejipanga vizuri sana, ari ya wachezaji wetu ni kubwa na Mungu akitujalia basi kesho tutafanya maajabu. Mimi kilichonileta hapa ni kuwaomba mashabiki wa Simba, Watanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani,” amesema Mo

“Kujitokeza kwa mashabiki kuna faida kuu mbili, moja unawaongezea nguvu wachezaji wetu na wao wanaona kuwa Watanzania wapo nyuma yao, lakini pili inawaogopesha wapinzani wetu”

Mo amesema mashabiki wa Simba wameifanya timu hiyo iandike rekodi ya kuwa timu namba moja kwa kujaza uwanja katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu

“Niwashukuru mashabiki wa Simba, niwapongeze ukiangalia takwimu za mechi za Ligi ya Mabingwa hakuna timu ambayo imejaza uwanja wake kama Simba Sports Club, Simba inaongoza kwa kujaza uwanja kwenye mechi zake”

“Nawaomba sana mashabiki ikitokea bahati mbaya ya hapa na pale, tuendelee kushabikia sio tu mpaka tukipata goli, naomba sana tubadilike kwenye hilo, tushangilie Simba tangu mwanzo hadi mwisho”

“Hapa hatushiriki tu, tunajiamini kwamba tunaweza na tunataka kwenda mbali zaidi ya hapa”

“Shabaha yetu sio tu kufanikiwa mwaka mmoja, tunataka kushinda kombe kila mwaka ili tushiriki Ligi ya Mabingwa kila mwaka, tunataka kushinda kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika, mimi naamini uwezo tunao, tumtangulize Mungu”

MO DEWJI: Atoa NENO – SIMBA vs TP MAZEMBE

“Tumejipanga vizuri sana, ari ya wachezaji wetu ni kubwa na Mungu akitujalia basi kesho tutafanya maajabu. Mimi kilichonileta hapa ni kuwaomba mashabiki wa Simba, Watanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani”- Mo Dewji.
.
“Kujitokeza kwa mashabiki kuna faida kuu mbili, moja unawaongezea nguvu wachezaji wetu na wao wanaona kuwa Watanzania wapo nyuma yao, lakini pili inawaogopesha wapinzani wetu”- Mo Dewji.
.
“Niwashukuru mashabiki wa Simba, niwapongeze ukiangalia takwimu za mechi za Ligi ya Mabingwa hakuna timu ambayo imejaza uwanja wake kama Simba Sports Club, Simba inaongoza kwa kujaza uwanja kwenye mechi zake”- Mo Dewji.
.
“Nawaomba sana mashabiki ikitokea bahati mbaya ya hapa na pale, tuendelee kushabikia sio tu mpaka tukipata goli, naomba sana tubadilike kwenye hilo, tushangilie Simba tangu mwanzo hadi mwisho”- Mo Dewji.
.
“Hapa hatushiriki tu, tunajiamini kwamba tunaweza na tunataka kwenda mbali zaidi ya hapa”- Mo Dewji.
.
“Shabaha yetu sio tu kufanikiwa mwaka mmoja, tunataka kushinda kombe kila mwaka ili tushiriki Ligi ya Mabingwa kila mwaka, tunataka kushinda kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika, mimi naamini uwezo tunao, tumtangulize Mungu”- Mo Dewji.

#TukutaneTaifa #YesWeCan #NguvuMoja

USAJILI : Simba hawashindwi wanasa moja ya beki bora Afrika

Katika kuhakikisha inasajili wachezaji wanaoendana na mashindano wanayoshiriki, klabu ya Simba Sc imeanza kuwania saini ya beki wa kati wa As Vita Yannick Bangala Litombo (24) ili kuongeza nguvu katika kikosi chao msimu ujao. .

.
Mchezaji huyo ni beki wa kati mwenye umri wa miaka 24 lakini April 14 atakuwa anafikisha miaka 25 anaurefu wa mita 1.88 uraia wake ukiwa ni wa Congo.
Mchezaji huyo amewahi kucheza Les Stars ya Congo, Dc Motema Pembe na kisha akajiunga na As Vita ambayo amecheza nayo kwa mafanikio na kutajwa mara kadhaa kama moja ya mabeki bora wa kati barani Afrika kwasasa.

ambapo mkataba wake unatarajia kumalizika 30 Juni 2019

.
.
Mbali na hilo Litombo ni moja ya mabeki wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ya Congo chini ya kocha Florent Ibengé akisaidiana na Mwinyi Zahera.
#sokaonline

.
.
Mbali na hilo Litombo ni moja ya mabeki wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ya Congo chini ya kocha Florent Ibengé akisaidiana na Mwinyi Zahera.
#sokaonline

TP Mazembe yaingia mchecheto kuikabili Simba

Ni kama TP Mazembe imeingiwa hofu kuelekea mchezo wa Jumamosi baada ya timu hiyo kukataa kutumia basi walilopewa na Simba

Aidha timu hiyo imetoa tuhuma lukuki ikidai haitasita kupeleka malalamiko CAF kama itafanyiwa matendo yasiyo ya kiungwana

Uongozi wa timu hiyo umedai kuwa na taarifa za matukio zilizofanyiwa timu zilizokuja kucheza na Simba jijini Dar es salaam

Hata hivyo Afisa Habari wa Simba Haji Manara ameitaka timu hiyo isianze kutoa visingizio mapema na badala yake wakacheze mpira uwanja wa Taifa

Manara amesema baadhi ya timu zinajiona kuwa na haki ya kushinda zaidi kuliko timu nyingine jambo ambalo sio sahihi

Simba tayari imerejea jijini Dar es salaam kufanya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchin