SIMBA 3-0 MBAO FC

Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba ni kama hawakamatiki baada ya leo kushinda mchezo wa 10 mfululizo kwa kuifumua Mbao Fc mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro

Mabao mawili ya nahodha John Bocco na moja la Meddie Kagere yametosha kuihakikishia Simba ushindi muhimu ambao umewasogeza karibu ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili baada ya kufikisha alama 57

Azam Fc ina alama 59 hata hivyo Simba ina michezo sita mkononi hivyo ni suala la muda tu mnyama atakaa katika nafasi yake na hatimaye kutetea ubingwa waliotwaa msimu uliopita

Mabao mawili aliyofunga Bocco leo yamemfanya afikishe mabao 11 akihitaji kufunga bao moja tu kumfikia Heritier Makambo wa Yanga

Kagere amezidi kumkaribia Salim Aiyee wa Mwadui Fc mwenye mabao 16, baada ya bao lake la mkwaju wa penati alilofunga leo kumfanya afikishe mabao 14

Baada ya ushindi wa leo kikosi cha Simba kitaendelea na maandalizi ya mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe

Simba itaendelea kujifua mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa April 06 katika dimba la Taifa

Maelezo zaidi jinsi ya kuchangia Yanga

Kwa wanaotumia MPESA maelezo haya hapa chini jinsi ya kuchangia Yanga.

Pia wachangiaji wanaweza kutuma michango yao moja kwa moja kwenda Akaunti ya CRDB ya Yanga : 0150419775800

TIGOPESA

1. Bonyeza *150*01#
2. Chagua Lipa Bili
3. Chagua Ingiza namba ya kampuni
4. Andika 101120
5. Sehemu ya kumbukumbu namba andika 1
6. Weka kiasi (2,500 na kuendelea)
7. Andika namba yako ya siri kuhakiki malipo yako

Lipuli watapata tabu sana – Zahera

Baada ya kupenya hatua ya nusu fainali michuano ya kombe la FA (ASFC), kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema mchezo wa nusu fainali dhidi ya Lipuli Fc utakuwa mwepesi, ana matumaini makubwa kuwa kikosi chake kitatinga fainali

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo jana, Zahera amesema mchezo dhidi ya Alliance ulikuwa mgumu sana na walihitaji bahati kuweza kusonga mbele

“Leo (jana) tumeteseka sana, michezo miwili tuliyocheza na Alliance hapa Mwanza tumeteseka sana lakini mchezo ujao dhidi ya Lipuli utakuwa rahisi kwetu,” alisema Zahera

“Nimewaangalia Lipuli Fc, mchezo waliotufunga tuliwazidi kila kitu lakini tulikosa bahati tu”

“Ukiacha mpira wa adhabu waliyofunga na kona moja aliyodaka Kindoki, hawakutengeneza nafasi zaidi yetu”

“Sisi tulitengeneza nafasi sita lakini hatukuzitumia. Hivyo Lipuli Fc hawatutishi, tutarejea Iringa kucheza nao “

Yanga inatarajiwa kucheza na Lipuli Fc mwishoni mwa mwezi wa nne katika mchezo wa nusu fainali utakaopigwa uwanja wa Samora, Azam Fc itacheza na KMC katika mchezo mwingine wa nusu fainali utakaopigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi

Simba vs Mbao Fc uwanja wa Jamhuri leo

Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba leo Jumapili wanashuka katika uwanja wa Jamhuri kuikabili Mbao Fc katika mchezo wa ligi utakaopigwa saa kumi kamili jioni

Simba iko mkoani Morogoro tangu juzi ikiendelea na maandalizi ya mchezo huo ambao umevuta hisia za mashabiki wa soka mkoani Morogoro na maeneo ya jirani

Kikosi cha Simba kimepania kuondoka na alama zote tatu dhidi ya Mbao Fc ambayo ilifanikiwa kushinda mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa mwaka jana jijini Mwanza

Simba inafukuzia rekodi mpya ya kushinda michezo 10 mfululizo kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wamefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo na ana matumaini makubwa kuwa wataibuka na ushindi

Ushindi utazidi kuisogeza Simba karibu ya timu zilizo juu yake, Azam Fc na Yanga

Simba yenye michezo 10 ya viporo, inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 54, Azam Fc ina alama 59 ikiwa nafasi ya pili na Yanga bado iko kileleni ikiwa na alama 67

Hata hivyo Simba inaweza kuzipiku timu hizo kama itashinda michezo yake yote ya viporo

Bocco, Kagere kuongoza maangamizi ya Mbao Fc leo

Nahodha wa kikosi cha Simba John Bocco ‘Adebayor’ yuko kwenye kiwango bora sana, leo anatarajiwa kuwaongoza mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara kuikabili Mbao Fc mkoani Morogoro

Baada ya kufanya kazi kubwa ya kuivusha Simba hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vita, kisha akaivusha Stars fainali za AFCON 2019 katika mchezo dhidi ya Uganda kwa kutengeneza mabao mawili kati ya matatu yaliyofungwa na Stars, Bocco leo atakuwa dimbani kufanya kazi maalum ya kuitafutia Simba alama tatu muhimu

Aidha kinara wa upachikaji mabao katika kikosi cha Simba, Meddie Kagere naye atakuwa na nafasi ya kuongeza mabao yake na kumkaribia Salum Aiyee wa Mwadui Fc mwenye mabao 16

Kagere yuko nafasi ya pili kwenye orodha ya vinara wa upachikaji mabao akiwa na mabao 13

Bocco na Kagere wamerejea kikosini baada ya kutumikia timu zao za Taifa wakiwa ‘fit’ na hakuna shaka Aussems anazihitaji silaha hizi kuweza kuimaliza Mbao Fc baadae leo

FT : Alliance 1-1 Yanga, mikwaju ya penati 4-3 yaipeleka Yanga nusu fainali

Mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga wametinga nusu fainali ya kombe la FA (ASFC) baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 4-3 kufuatia matokeo ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Alliance Fc


Yanga ilitangulia kupata bao la kuongoza kwenye dakika ya 39 likiwekwa kambani na Heritier Makambo kwa kombora la nje ya 18
Alliance Fc iliyokuwa kwenye kiwango bora ilisawazisha bao hilo kwenye dakika ya 62 kupitia kwa Joseph James
Baada ya kumalizika kwa dakika 90 huku matokeo yakiwa 1-1, changamoto ya mikwaju ya penati ikatumika kuamua mshindi

Deus Kaseke, Paulo Godfrey, Thabani Kamusoko na Haruna Moshi ndio waliofunga penati za Yanga
Yanga sasa itachuana na Lipuli Fc kwenye mchezo wa nusu fainali

Kikosincha Yanga vs Alliance FC

1. Klaus Kindoki

2. Paulo Godfrey

3. Gustavo Simon

4. Said Juma

5. Kelvin Yondani

6. Feisal Salum

7. Mrisho Ngasa

8. Papi Tshishimbi

9. Heritier Makambo

10. Amissi Tambwe

11. Pius Buswita

SUB

Ibrahim Hamid

Jaffar Mohammed

Andrew Vicent

Haruna Moshi

Thabani Kamusoko

Raphael Daudi

Deus Kaseke

Zahera awafungulia mlango wanaotaka ‘kusepa’

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema amezisikia tetesi zinazowahusu wachezaji wake wanaowaniwa na timu nyingine na ametoa ruhusa kwa mchezaji yeyote anayetaka kuondoka, aondoke

Zahera ambaye yuko Mwanza na kikosi cha Yanga ambacho leo kinatarajiwa kushuka uwanja wa CCM Kirumba kuumana na Alliance Fc katika mchezo wa robo fainali kombe la FA, amesema hana wasiwasi kama wachezaji hao wataondoka kwa kuwa amedhamiria kuisuka upya Yanga kwa ajili ya msimu ujao

Aidha Zahera amesema Yanga ya sasa sio tegemezi, haiwezi kutetereka kama wachezaji hao wataondoka hata leo

“Watu wananipigia simu kuniuliza kuhusu wachezaji wa Yanga hasa Yondani, Tshishimbi, Ajibu na Feisal kutakiwa na timu nyingine.”

“Tangu mwanzo wa ligi ukiangalia kuna mechi mingi tulizocheza, angalia mechi ngapi tuilicheza bila Kevin ngapi tulicheza bila Tshishimbi bila Ajibu na Feisal. Kuna mechi tulicheza bila watatu kati yao ndani ya mechi moja na tulishinda,” amesema Zahera

“Nikisikia leo Yanga hakuna mchezaji hata mmoja kwenye timu ninaweza kulia lakini mchezaji mmoja akikosa siwezi kukosa usingizi.”

“Mchezaji yeyote anayetaka kuondoka anaweza kuondoka, hakuna hata mchezaji mmoja anaweza kuniogopesha kwakuwa timu fulani inamtaka lakini najua msimu ujao wa ligi timu hii itabadilika sana.”

“Yanga sio team ya mchezo, Yanga ni timu kubwa na inawachezaji wakubwa. Yanga ina wachezaji wazuri lakini msimu unaokuja nadhani Yanga itakuwa na wachezaji wakubwa saana.”