


































Mabao ya Simba yalipatikana kwenye kipindi cha pili yakiwekwa kambani na beki Paul Bukaba (51′) huku bao la pili likifungwa na Meddie Kagere kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 55 baada ya Adam Salamba kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems alifanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake leo akiwapumzisha baadhi ya nyota waliocheza mchezo wa ligi ya mabingwa mwishoni mwa wiki
Aidha bao alilofunga Kagere leo limemfanya afikishe mabao 13 sasa akishika nafasi ya pili nyuma ya Salim Aiyee wa Mwadui Fc mwenye mabao 16
Simba inaendelea kushika nafasi ya tatu ikiwa imefikisha alama 54, alama tano nyuma ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili huku Yanga ikiongoza ikiwa na alama 67
Hata hivyo Azam Fc na Yanga zimecheza michezo saba zaidi ya Simba
Baada ya juzi kuitoa Tanzania kimasomaso kwa kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, kikosi cha Simba kesho Jumanne kitakuwa dimba la Taifa kuikabili Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa moja jioni
Simba inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 51
Hata hivyo ina michezo tisa ya viporo hivyo kuwa na nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wake kama itashinda yote


Kabla ya msimu huu, Tanzania ilikuwa nafasi ya 26 na pointi zake 3 zilizotokana na Yanga kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, 2016 na 2018.
Kufuzu kwa Simba robo fainali msimu huu, kumeipatia nchi yetu pointi 15 ambazo zikichanganywa na zile 3 za Yanga, tunakuwa na pointi 18
POINTI
CAF hupima viwango vya nchi kupitia mafanikio ya vilabu vyake, kwenye mashindano ya Afrika, kwa kipindi cha miaka mitano.
Viwango vipya vitakavyotoka vikijumuisha mafanikio ya Simba 2018/19, vitaanzia 2015.
Mwaka wa karibuni zaidi huwa na thamani kubwa zaidi (maksi 5) kuliko mwaka wa nyuma zaidi (maksi 1).
Thamani ya mwaka wa mashindano huzidishwa na pointi ambazo klabu huzipata kutokana na mafanikio yake kwenye mashindano husika, na kuwa pointi za nchi.
KOMBE LA SHIRIKISHO
Klabu itakayoshika nafasi ya 4 kwenye makundi, hupewa pointi 0.5. Nafasi ya 3, pointi 1, robo fainali, pointi 2, bingwa pointi 5.
Yanga ilifuzu hatua ya makundi mwaka 2016 na 2018, na kumaliza ya 4 mara zote mbili.
Thamani ya mwaka 2016 ni maksi 2, maana yake ni 0.5 × 2 = 1. Thamani ya mwaka 2018 ni maksi 4, maana yake ni 0.5 × 4 = 2.
Kwa hiyo Tanzania ilivuna pointi 3 kutokana na mafanikio ya Yanga, 2016 na 2018!
LIGI YA MABINGWA
Kufuzu makundi tu ni pointi 0.5 na kufika robo fainali ni pointi 3. Simba imefika robo fainali 2018/19 ambao thamani yake ni maksi 5. Maana yake ni 3X5=15.
Pointi hizi 15 zikijumlishwa na zile 3 za Yanga, Tanzania inakuwa na pointi 18.
Hata hivyo, pointi hizi zitaingia kwenye mahesabu kuanzia msimu ujao kwa ajili ya matumizi ya msimu wa mbele yake, yaani 2020/2021.
Hakuna uwezekano wa pointi zetu kuvukwa na nchi nyingine kwa sababu walio chini yetu hawana timu zilizopo kwenye mashindano.
Pia ukiangalia hapo kwenye mchoro, utaona pointi zetu zimewekewa alama ya ≥…hii ina maana kwamba zinaweza kuongezeka, endapo Simba watasonga mbele zaidi.
2020/21 tutaingiza timu nne michuano ya vilabu barani Afrika!
Beki wa klabu ya Simba Sc Erasto Nyoni ameitwa kunako kikosi cha timu ya Taifa kuchukua nafasi ya Andrew Vicent anaesumbuliwa na majeraha tayari kwa mchezo wa Jumapili March 24 dhidi ya Uganda
Full Time.
Everton 2-0 Chelsea
Richarlison ⚽
Sigurdsson ⚽
#Epl

Hakika wanastahili pongezi kwa mafanikio hayo
Watani zetu wametufundisha jambo kubwa sana, ili kuweza kufanikiwa tunahitaji uwekezaji wa fedha, akili, muda, hali na mali pasipo kukata tamaa
Kama Simba wangekata tamaa baada ya kupigwa zile dozi za tano tano sidhani kama wangekuwa na ubavu wa kushinda michezo yao miwili waliocheza nyumbani dhidi ya vigogo wa soka Barani Afrika
Lakini pia nyuma ya mafanikio hayo yupo mwekezaji wao Mohammed Dewji ‘Mo’ ambaye alimwaga fedha za kutosha kutengeneza kikosi ambacho leo kimewafanya waweze kutembea kifua mbele
Simba ndio klabu pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya ligi ya mabingwa
Wana Yanga yatupasa kupambana juu chini kuhakikisha nasi tunafanya mabadiliko katika timu yetu ili tuweze kuwavutia wawekezaji walete fedha
Mpango huu wa kuchangia uliopendekezwa na kocha Mwinyi Zahera sio wa kudumu, utaisaidia Yanga kusimama wakati ikijiweka sawa
Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ndio kila kitu, kwani mabadiliko waliyofanya Simba tumeona jinsi yalivyokuwa na faida kwao
Uwekezaji aliouweka Mo katika kipindi cha misimu miwili kwenye klabu ya Simba umekuwa na faida kubwa kwake na kwa Simba pia
Kwa kutinga hatua ya robo fainali tu Simba itavuna zaidi ya Bil 1.5 fedha ambazo ni zaidi ya fedha walizotumia kukijenga kikosi chao(bil 1.3)
Ukiongeza na fedha walizovuna kupitia mashabiki ambao waliujaza uwanja wa Taifa katika michezo yote mitatu waliocheza jijini Dar es salaam pamoja na mauzo ya jezi, timu hiyo itakuwa imetengeneza fedha nyingi sana
Simba wametuonyesha kumbe haya yote yanawezekana, ukijipanga vizuri na ukafanya uhamasishaji wa kutosha unaweza kufanya mambo makubwa kuliko wengi tulivyokariri
Nani alitegemea kama Simba itaweza kuifunga Al Ahly, mabingwa mara nane barani Afrika? Al Ahly ambayo ilicheza fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu uliopita
Nani alidhani kama Simba itapata ushindi dhidi ya Vita jana? Hawa Vita walicheza fainali ya kombe la shirikisho msimu uliopita
Simba haikupewa nafasi ya kupenya katika kundi D lililozijumuisha JS Saoura, Al Ahly na Vita lakini wamepita
Hivi kuna atakayeshangaa tena kama Simba itatwaa ubingwa wa Afrika? kwani hatua waliyofikia lolote linaweza kutokea.
Jambo la muhimu kwa Wana Yanga ni kupata somo kutokana na mafanikio haya. Kama hatua hazitachukuliwa, Yanga haiwezi kushindana na Simba katika nyanja zote.
Ni wazi msimu ujao huenda ukawa mgumu zaidi kupambana na Simba kwani watakuwa bora mara dufu kuliko walivyo sasa.
Sababu mpaka hapa walipofikia wameyajua mapungufu yao na tayari wanao ushawishi wa kumsajili mchezaji yeyote wanayemtaka kutokana uwepo wa fedha na mafanikio waliyopata
Itakuwa muujiza kwa Yanga yetu hii kushindani na wenzetu ambao kimsingi mpaka sasa wameshatuacha mbali sana

Baada ya kuwa nje tangu mwezi Januari, Nyoni alirejea kikosini jana kuwakabili Vita Club na hakika alidhihirisha kwa nini mashabiki walihitaji sana urejeo wake
Licha ya kutocheza kwa muda mrefu Nyoni hakuonyesha dalili yoyote ya kutokuwa ‘fit’ akiwadhibiti ipasavyo washambuliaji wa Vita walio-ongozwa na Makusu
Nyoni alifanya kazi ya ziada kwenye safu ya ulinzi ya Simba akiwa kiongozi aliyesaidia kuwapanga wenzake katika kuhakikisha wapinzani hawalifikii lango
Juzi kocha Mkuu wa Taifa Stars Emmanuel Amunike alimrejesha katika kikosi cha timu ya Taifa kuchukua nafasi ya Andrew Vicent wa Yanga
Unapozungumzia ushindi wa mabao 2-1 iliyopata Simba dhidi ya Vita Club jana, unazungumzia juhudi na kujituma kwa wachezaji wa Simba, Nyoni akiwa mmoja wa wachezaji waliocheza vizuri sana