

































Kikosi cha Yanga Sc kinatarajia kuondoka jijini Dar Es Salaam leo Asubuhi kuelekea mkoani Iringa tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Lipuli Fc utakaopigwa Jumamosi hii March 16 katika uwanja wa Samora mkoani humo.
#UCL



Full Time.
Barcelona 5-1 Lyon
(Messi ⚽⚽, Coutinho ⚽, Pique ⚽, Dembele ⚽ | Tousart ⚽) #UCL

Simba iliyorejea jana kutoka Algeria inajifua kwenye uwanja wa Boko Veterans

Nyoni na Okwi hawakusafiri na Simba ilipokwenda nchini Algeria kumenyana na JS Saoura kutokana na kuwa majeruhi
Wachezaji hao leo wamejumuika na wachezaji wengine wakihusika katika program zote za mazoezi hivyo kuongeza matumaini kuwa wako tayari kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi


Kikosi cha As Vita kutoka Congo kimeondoka nchini humo kuja Tanzania tayari kwa mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika dhidi ya Simba Sc utakaopigwa March 16 jijini Dar Es Salaam



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya wataalamu wa Tanzania na Morocco wanaoshughulikia ujenzi wa uwanja wa michezo katika Jiji la Dodoma, unaotarajiwa kujengwa kwa msaada wa Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI.
Balozi wa Morocco hapa nchini aliyeongoza ujumbe wa wataalamu kutoka Morocco Mhe. Abdelilah Benryane amesema pamoja na kuzungumzia uhusiano mzuri wa Tanzania na Morocco wamejadiliana kuhusu utekelezaji wa miradi iliyokubaliwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco hapa nchini mwaka 2016 ikiwemo ujenzi wa Msikiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) unaojengwa Jijini Dar es Salaam na kuanza kwa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu Jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale amesema uwanja huo utajengwa jirani na eneo la Nanenane kando ya barabara ya Dodoma – Morogoro, utajengwa kwa mfano wa mlima Kilimanjaro na utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji kati ya 85,000 na 100,005.
Leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mchezaji wetu Paul Bukaba.
Andika ujumbe wako kumtakia heri katika siku hii muhimu kwake. #SSC #NguvuMoja

