
credit: @sokawaytz…
– Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi ndiye Mwanamichezo anaelipwa mkwanja zaidi duniani, akijiingizia $127m (£99.8m) katika miezi 12 iliyopita, kulingana na takwimu zilizo tolewa na Forbes; Nyota wa Juventus ya Ureno, Cristiano Ronaldo ni wa pili akijiinguzia $109m (£85.6m) na Mbrazili wa Paris St-Germain, Neymar anafuatia wa tatu kwa $105m (£82.5m).
.
– Kinara wa mwaka jana alikuwa ni Mwana masumbwi, Floyd Mayweather ambaye ameshuka katika orodha hii; Mcheza Tennis, Serena Williams ni mwanamke pekee aliye juu top 100, akipata dola 29.2m (£22.9m)…Bingwa Mara tano wa Dunia wa mbio za Magari ya Langa langa “Formula 1”, Lewis Hamilton na bingwa wa zamani wa uzito wa Juu katika Ndondi, Anthony Joshua ndio wanaopata mkwanja Mrefu Kama Wanamichezo wa Uingereza wakiwa nafasi ya 13 wakijiinguzia $55m (£43.2m).
.
– Gazeti hilo La biashara la Marekani limehesabu mapato ya wanamichezo na kuongeza fedha zao za mshahara kati ya Juni 2018 na Juni 2019.. Top 100 ni pamoja na wanamichezo kutoka nchi 25 na $4bn (£3,1bn) ndio mapato yao kwa pamoja yakiongezeka kwa 5% kutoka mwaka uliopita, wakati Mayweather alikuwa kinara mwa $285m (£224m).
.
– Messi ni Mchezaji wa Soka wa nane tofauti kuchukua nafasi ya kwanza katika Orodha hii ambapo takwimu zake zilianza rasmi mwaka 1990.. Pia ni mara ya kwanza kwamba ni wanasoka wote wameshikilia tatu bora…Messi ni mmoja Kati ya Wanamichezo 38 wasiokuwa Raia wa kwenye orodha… Paul Pogba kiungo wa Manchester United ni mchezaji Anaeongoza kutoka Ligi Kuu Uingereza akiwa katika nafasi ya 44 akijiingizia $33m (£25.9m).
✋🏻 TOP 10 inasimama hivii
1. Lionel Messi $127m (£99.8m)
2. Cristiano Ronaldo $109m (£85.6m)
3. Neymar $105m (£82.5m)
4. Canelo Alvarez $94m (£73.8m)
5. Roger Federer $93.4m (£73.3)
6. Russell Wilson $89.5m (£70.3m)
7. Aaron Rodgers $89.3m £70.1m)
8. LeBron James $89m (£69.9m)
9. Stephen Curry $79.8m (£62.7m)
10. Kevin Durant $65.4m (£51.3m)..
#Updates #forbessportsmoney #forbes
@Sokawaytz