KAPOMBE : Kinara wa kupiga Mabao SIMBA SC

Achana na burudani inayotolewa na kiungo fundi Cletus Chotta Chama ‘Triple C’, mwamba wa Lusaka katika kikosi cha Simba, beki Shomari Kapombe ndiye kinara wa ‘upishi’ wa mabao ya mabingwa hao wa Tanzania Bara.

Kapombe beki mwenye uwezo wa kupanda na kushuka kwa kasi, ametengeneza mabao matano yaliyofungwa na Simba msimu huu.

Amekuwa katika kiwango bora na hakika anastahili pongezi za kipekee.

Afisa wa Habari wa Simba Haji Manara amesifu kiwango kinachoonyeshwa na beki huyo aliyerejea Simba msimu uliopita akitoka Azam Fc.

“Cloutus Chama kiuhalisia anacheza mpira wa kwenye play station,jamaa anajua hadi anakera! Wakati tunamsajili nilivyotamba sikueleweka,now tunaelewana”, ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram

“Na hivi kweli Kapombe anacheza ligi ya Bongo bado? Anaassist kuliko mabeki wengi wanaopuyanga kwenye Premier!
Simba na Barcelona ndio vitu vinavyoburudisha zaidi Duniani kando ya Pesa!”

USAJILI: TZ Prisons kumsajili mchezaji huyu wa SIMBA P

Imeripotiwa kuwa Klabu ya Tz Prisons ya jijini Mbeya ipo mbioni kumsajili mshambuliaji wa Simba Sc Mohamed Rashid kwa mkopo mara baada ya kumalizika kwa msimu huu.
Mo ni moja ya wachezaji waliokosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Simba sc tangu kuanza kwa msimu huu.
#tanzaniapremierleague🇹🇿

UCHAGUZI: SIMBA SC

Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa bodi ya Simba Hussein Kitta amesema endapo atafanikiwa kuchaguliwa, jambo la kwanza itakuwa ni kuwaelewesha wanachama juu ya mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu hiyo.
:
KWA NINI AMECHUKUA FOMU KUGOMBEA?

Wakati umefika kwa sababu nimekuwa nikifatilia masuala ya mpira kwa siku nyingi, nimekuwa kiongozi kwenye makundi madogomadoo kama tawi la Simba Makini, baada ya haya mabadiliko ya mfumo nimeona unaendana na fikra za Simba Makini nimeona naweza ku-fit kwenye mfumo wa sasa.
:
ATAIFANYIA NINI SIMBA?

Mambo ya kufanya ni mengi, pamoja na kutoa mchango wangu katika masuala ya mpira yapo zaidi ya mpira ambayo mimi nina uwezo nayo kwa sababu ya taaluma yangu. Kitaaluma mimi ni mwanasheria ni mhadhiri wa sheria chuo kikuu cha Dar es Salaam.
:
Kazi ya kwanza kabisa ni kuelewesha wanasimba juu ya huu mfumo mpya kwa sababu ukimsimamisha mtu barabarani ukamuuliza kuhusu huu mfumo atashindwa kukujibu kwa hiyo natakiwa kuhakikisha watu wanaelewa ili yanayokwenda kufanyika waelewe yanafanyika kwa sababu ya mfumo mpya.
:
Kule kwenye bodi ndio ambapo mikakati mikubwa inapangwa sehemu ambayo mwelekeo wa klabu na shughuli zake unatengenezwa kwa hiyo nakusudia nitakapokuwa pale kupitia uzoefu wangu katika masuala ya mpira na taaluma yangu nitavichanganya pamoja ili vitusaidie kuijenga Simba imara.
:
Anakuja mwekezaji Mohammed Dewji anaweka bilioni 20, ile bodi itakuwa na watu mchanganyiko watu kutoka upande wa klabu na wengine kutoka upande wa mwekezaji. Sitegemei mtu aweke bilioni 20 halafu alete watu dhaifu kwenye bodi kwa hiyo ninaamini nina uwezo wa kuwawakilisha wanachama wa Simba kwenye bodi katika kusimamia maslahi yao kwa hoja ambazo naweza kuzisimamia.
:
SERA ANAYOINGIA NAYO

Naingia na sera ya kufanya kazi pamoja na wenzangu wa bodi kwa maslahi ya wanachama ambao wamenichagua.
:
Simba sasa hivi inakuwa kampuni (Simba Sports Club LTD) kampuni huwa zinakuwa na malengo ambayo tayari yameandikwa kwenhe document ya kuanzisha kampuni, kwa hiyo nitahakikisha nayasimamia malengo yote lakini pia kuna wanachama ambao wamenituma na Simba ina historia yake ambayo hiki chombo kimpya kinachokuja kitahakikisha pamoja na mabadiliko, haipotezi kule ilikotoka.

Simba Vs KMC : Mchezo wa sogezwa mbele

Bodi ya Ligi imesogeza mbele mchezo wetu na KMC ambao ulikuwa umepangwa kuchezwa tarehe 8/11/2018 ili kupisha maandalizi ya timu ya Taifa (Taifa Stars). Pia bodi imetangaza kwamba mchezo wetu na Lipuli FC ambao ulisogezwa mbele sasa utachezwa tarehe 21/11/2018 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

FT : Mwadui FC 1-3 Simba


Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi kusaka mabao ya mapema lakini ililazimika kusubiri hadi dakika ya 41 kuandika bao la kwanza kupitia kwa nahodha wake John Bocco ‘Adebayor’ kwa mkwaju wa penati.

Simba ilizawadiwa penati hiyo baada ya Shiza Kichuya kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari.

Simba iliendelea kutawala mchezo huo na ilifanikiwa kuandika bao la pili dakika chache kabla ya filimbi ya mapumziko mfungaji akiwa Bocco tena.

Bocco alimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Meddie Kagere aliyewatoka walinzi wa Mwadui Fc kisha kujaza majaro ya chinichini iliyomkuta Bocco akiwa uso kwa uso na nyavu.

Simba iliyonoga kwelikweli leo iliandika bao la tatu kwenye dakika ya 50 mfungaji akiwa Meddie Kagere aliyepiga shuti kali baada ya kumhadaa mlinzi wa Mwadui FC.

Bao pekee la kufutia machozi kwa upande wa Mwadui FC lilifungwa na Charles Ilafya kwenye dakika ya 81.

Bocco alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye dakika ya 77 baada ya kumpiga ngumi Revocatus Mgunga.

Bocco ataukosa mchezo dhidi ya Yanga utakaopigwa Septemba 30.

Bocco aandika Historia

Mabao mawili aliyofunga kwenye mchezo wa leo yamemfanya John Bocco afikishe jumla ya mabao 100 tangu alipoanza kucheza ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2008/09.

Septemba 24, 2008, Bocco alifunga goli lake la kwanza Ligi Kuu Tanzania wakati Azam FC iliposhinda 2-0 dhidi ya Toto Africa ya Mwanza.

Msimu uliopita 2017/18 ulikuwa wa 10 kwa Bocco akicheza ligi kuu Tanzania bara, katika msimu huo alifunga magoli 14 na kumfanya afikishe jumla ya magoli 98

FT : Ndanda 0-0 Simba


Hii ni mara ya kwanza kwa klabu ya Ndanda kupata pointi moja dhidi ya Simba kwani tangu ipande daraja misimu minne iliyopita haikuwa imewahi kushinda wala kupata sare dhidi ya Simba.

Licha ya kumiliki mpira kwa muda mwingi washambuliaji wa Simba John Bocco, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi hawakufanikiwa kuipenya ngome ya Ndanda iliyotumia wachezaji wote 10 katika kujilinda.

Matokeo ya michezo yote iliyopigwa leo;