Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ amesema hivi karibuni atatoa Bilioni 20 za uwekezaji wa klabu hiyo

Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’ amesema hivi karibuni atatoa Bilioni 20 za uwekezaji wa klabu hiyo alizoahidi kuzitoa baada ya kushinda zabuni

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mo amesema changamoto ya urasimishaji wa mali za Simba imepelekea yeye kuchelewa kutoa fedha hizo

“Simba haikuwa na nyaraka halisi zake yakiwemo majengo na uwanja wa Bunju. Uongozi ulilazimika kufanya kazi ya ziada kupata hati halisi kwa mujibu wa sheria, ” alisema Mo

“Lakini pia Simba ilikuwa na madeni Mamlaka ya Mapato (TRA), klabu ilitakiwa kupeleka hesabu kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu. Kwa sasa zoezi hilo limekamilika na hata hati halisi za mali za klabu zimekamilika hivyo kukamilisha mchakato wa kufanikisha zoezi la uwekezaji”

Mo alisema anatarajia kuanza kutoa fedha zilizomo ndani ya mkataba wa uwekezaji muda mfupi ujao baada ya mchakato wa uwekezaji kukamilika

Tangu Simba ilipofanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wake, Mo amekuwa akitoa fedha zote za kuiendesha timu hiyo ikiwemo kulipa mishahara ya wachezaji pamoja na mambo mengine yanayohusu fedha

Baada ya ligi kumalizika, Mo ameahidi kukiboresha kikosi cha Simba ambapo amesema fedha zitakazotumika kwenye usajili ni zaidi ya zile zilizotumika msimu uliopita

Msimu uliopita Simba ilitumia Tsh Bilioni 1.3 katika usajili

MO Ataka Bodaboda ziwanufaisge wachezaji wa SIMBA

Ukiachilia mbali zawadi nyingi ambao uongozi wa klabu ya Simba utawapa wachezaji baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa pili mfululizo, jana Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji ‘Mo’ aliahidi kuwapa kila mchezaji Bodaboda yenye thamani ya Tsh Mil 2.4

Mo alisema zawadi hiyo itawasaidia wachezaji na familia zao kwani ni kitega uchumi kizuri

“Zawadi hii ya Bodaboda kwa kila mchezaji naitoa mimi mwenyewe. Nimewaambia wachezaji watumie Bodaboda hizo kama kitega uchumi na kuwapa ndugu zao ili kujiingizia kipato kila siku,” amesema Mo

“Wanaweza kuingia mikataba na ndugu zao ambao hawana kazi na kujipatia Tsh 15,000/- mpaka pale mikataba hiyo inapomaliza”

“Nimefarijika na mafanikio tuliyopata msimu huu. Umoja na Mshikamano baada ya kuanza uongozi mpya ni chachu ya mafanikio haya”

“Nimethamini kilichofanywa na wachezaji wetu msimu huu ndio maana nimeamua kuwapa zawadi hiyo kila mmoja”

Bilionea huyo amesema msimu ujao wamejipanga kupata mafanikio zaidi ambapo safari hii timu inatarajiwa kwenda kuweka kambi Ureno au Marekani

Simba inatarajiwa kuingia kambini mara tu baada ya kumalizika fainali za michuano ya AFCON 2019 inayofanyika nchini Misri

Wachezaji nane wa kikosi cha Simba wanatarajiwa kushiriki michuano hiyo

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema Simba imetawazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Uinted

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema Simba imetawazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Uinted

Ushindi huo uliiwezesha Simba kufikisha alama 91, alama ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine

Wambura amesema Simba walikuwa na timu imara, walionekana kudhamiria kutwaa ubingwa huo tangu mwanzoni mwa msimu

Simba itakabidhiwa kombe keshokutwa Jumamosi, baada ya mchezo dhidi ya Biashara United utakaofanyika uwanja wa Uhuru

Simba kuweka kambi Marekani au Ureno Pre- Season

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji amesema kuwa bodi ya wakurugenzi imepanga kuipeleka timu hiyo Marekani au Ureno kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Dewji alisema hayo wakati wa kuipongeza timu hiyo kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo na zoezi wapi watakwenda itajadiliwa ndani ya wiki hii.

Alisema kuwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo ni mafanikio makubwa ambayo yametokana na ushirikiano baina ya viongozi, wanachama, mashabiki na wadau wa soka kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Dewji, Ligi Kuu ilikuwa ngumu na hasa baada ya klabu ya Yanga ilikuwa inaongoza ligi hiyo kwa pointi 21.

“Haikuwa kazi rahisi kutafuta pointi ambazo wapinzani wetu wameweza kupata. Wachezaji waliweza kupigana kiume mpaka kupata ushindi wakiwa na mechi mbili mkononi.

MO DEWJI

“Niwapongeza na kuwashukuru wachezaji wamejitolea kwa namna moja au nyingine hadi tunaupata huu ubingwa, niwashukuru wanachama na wapenzi wote wa Simba kwa kujitokeza kutushangilia.”- Mo Dewji
.

“Kocha ameshafikia malengo tuliyomuwekea tulikuwa tunataka ubingwa na kufika kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa, Mungu akitujalia kwenye wiki moja tutakaa nae tumuongeze mkataba … tutamueleza sehemu ambazo kuna mapungufu ili aendelee kufanyia kazi”- Mo Dewji
.
“Tunaanza kupanga maandalizi ya msimu, mimi binafsi naongea na timu za Ulaya na Marekani… kuna rafiki yangu anamiliki DC United nimeongea nae watualike tukafanye maandalizi Marekani, kuna uwezekano wa kwenda Ureno, kwenye wiki mbili zijazo tutajua timu itakwenda wapi”- Mo Dewji
.

“Kwenye mechi ambayo tutacheza kesho naomba niwashukuru sana SportPesa, hii ni mara ya kwanza kwa timu kutoka ligi kuu ya Hispania kuja kucheza Tanzania, ni historia kubwa kwa nchi yetu, tupo tayari kucheza na Sevilla, naomba mashabiki tujitokeze kwa wingi sana”- Mo Dewji
.
“Simba itakuwa kwenye soko kushindinda na Al Ahly, Zamalek, TP Mazembe kushindana kutafuta wachezaji wenye vipaji, tupo tayari kuwabakisha wachezaji ambao mwalimu atapendekeza, wengine watatoka kwa mkopo … bajeti ya mwaka huu itakuwa kubwa kuliko mwaka jana”- Mo Dewji
.

“Katika mechi ya kesho ya Sevilla nawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi ili na sisi tuweze kuwaonyesha mpira wa Ulaya”- Mwenyekiti wa klabu, Swedi Mkwabi.
#NguvuMoja #SportPesa Challenge #TukutaneMei23

MO DEWJI: Apongeza UBINGWA – SIMBA, Aweka wazi Mipango ya Msimu UJAO

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mohammed Dewji ‘Mo’ amewapongeza wachezaji, viongozi na mashabiki wa timu baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mo amesema ubingwa huo matokeo ya ushirikiano na umoja ulioonyeshwa na Wanamsimbazi tangu mwanzoni mwa msimu

Aidha Mo amesema shamrashamra za ubingwa zitafanyika May 25 wakati timu hiyo itakabidhiwa kombe katika mchezo dhidi ya Biashara United

Katika hatua nyingine Mo ameipongeza Yanga kwa kuipa changamoto Simba katika mbio za kuwania ubingwa.

Amewapongeza viongozi wapya wa timu hiyo na kuwataka waimarishe timu yao ili iweze kuipa changamoto zaidi Simba kwani anaamini uimara wa timu zote utaongeza ubora wa soka la Tanzania

Aussems kuendelea kuinoa Simba

Mo amesema baada ya kocha Mkuu Patrick Aussems kutimiza masharti yote ya mkataba wake, wanakusudia kumpa mkataba mpya

Mwaka jana Aussems aliposaini mkataba wa mwaka mmoja, alipewa masharti mawili ambapo moja ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu na la pili ni kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Maboresho ya kikosi

Mo amesema Aussems leo atawasilisha ripoti ya maboresho ya Simba kwa ajili ya msimu ujao.

Aussems atapendekeza wachezaji ambao anataka waachwe/watolewe kwa mkopo pia kocha huyo anatakiwa kupendekeza wachezaji ambao anataka wasajiliwe

Mo amesema wamedhamiria kuifanya Simba iwe imara mara dufu ili kuhakikisha inafanya vizuri zaidi kwenye michuano ya CAF msimu ujao

Amesema watashindana na vilabu vikubwa barani Afrika kama Al Ahly, TP Mazembe, Zamalek nk katika kuwania wachezaji wazuri

Kuhusu Kambi

Kama ilivyokuwa msimu uliopita, Mo amesema msimu huu Simba itaweka kambi barani Ulaya katika nchi ya Ureno au nchini Marekani

BOSS – SEVILLA Aipongeza Simba kutwaa UBINGWA

Timu ya Sevilla imewasili nchini usiku wa kuamkia leo tayari kwa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Simba utakaopigwa kesho Alhamisi, saa moja jioni katika uwanja wa Taifa

Katika Mkutano na Waandishi wa habari leo, Rais wa Sevilla Jose Castro ameeleza kufurahia ujio wao hapa nchini hasa ikizingatiwa wao wanakuwa timu ya kwanza kutoka Hispania kucheza Tanzania

Aidha ameipongeza Simba kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara

“Niwapongeze sana Simba ya Tanzania kwa kuchukua ubingwa wa ligi Kuu, tumekuja kucheza na timu bora. Ni heshima sana kuja Tanzania na bila shaka tutakua ni timu ya kwanza ya Laliga kuja Tanzania,” amesema

Wakati Sevilla ikiwa tayari imewasili, wapinzani wao Simba nao watatua leo kutoka mkoani Dodoma baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa pili mfululizo