Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Klabu ya Simba, Mohammed Dewji leo Jumatano Mei 22, 2019 saa 8:00 mchana ataongea na waandishi wa habari kwenye ofisi za MeTL Group zilizopo jengo la Golden Jubilee Towers, ghorofa ya 20
Category: simba
SEVILA YAWASILI BONGO
Kikosi cha Sevilla kimewasili jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo tayari kwa mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Tanzania Bara Simba
Sevilla ilikaribishwa nchini kwa burudani ya Msanii maarufu Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ aliyetumbuiza uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati timu hiyo ilipowasili

Wapinzani wao Simba wanatarajiwa kurejea leo Dar kutoka mkoani Singida ambako jana walitwaa ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuifunga Singida United mabao 2-0
Baada ya mchezo jana, Simba ilielekea mkoani Dodoma ambako leo inatarajiwa kuunganisha kwa usafiri wa Ndege kurudi jijini Dar es salaam
REKODI UBINGWA SIMBA vs YANGA


NIYONZIMA: Azidi Kuweka REKODI
– Kiungo wa Kimataifa wa Rwanda na Klabu ya @simbasctanzania ameendelea kuweka rekodi zake ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuwa Mchezaji wa kigeni kutwaa Makombe mengi zaidi ya Ligi Kuu Tanzania Bara; Baada ya kunyakua Ubingwa wa msimu huu 2018/19, Niyonzima Sasa kabeba Ubingwa Mara tano mfululizo Pia kwa jumla ni Mara ya Sita anatesa Ubingwa wa Tanzania 🇹🇿 akiwa na vilabu viwili tofauti na vikongwe nchini.
🏆2012/13 (Yanga)
🏆2014/15 (Yanga)
🏆 2015/16 (Yanga).
🏆 2016/17 (Yanga).
🏆 2017/18 (Simba).
🏆 2018/19 (Simba).
.
– Licha ya Bongo tu, Niyonzima Ana medali tatu za Ubingwa wa Kwao Rwanda 🏆 2008/9, 🏆 2009/10, 🏆 2010/11… Medali tatu za Ubingwa wa Kombe La FA kwao Rwanda 🏆 2007/8, 🏆 2009/10, 🏆 2010/11 na Medali Moja ya Ubingwa wa Kombe La FA nchini 🏆 2015/16.
#LigiKuuTanzaniaBara #TPL
@Sokawaytz
SHAMRASHAMRA ZA UBINGWA NAMFUA
Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida United, wachezaji wa Simba walizianza shamrashamra za kutwaa ubingwa wa pili mfululizo katika uwanja wa Namfua
Picha za matukio ya sherehe za ubingwa;







MO DEWJI APONGEZA UBINGWA SIMBA
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mohammed Dewji ‘Mo’ ameipongeza timu hiyo kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa pili mfululizo
Mo amesema mafanikio hayo yamepatikana kutokana na juhudi zilizofanywa na wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na wadau wote wa klabu ya Simba kila mmoja kwa nafasi yake
“Mungu mkubwa. Pongezi kwa wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, wanachama, mashabiki, na wapenzi wote wa SIMBA, tumeshinda! Najivunia mafanikio haya,” amesema Mo
Naye Msemaji wa Simba Haji Manara amewapa shukrani za kipekee wachezaji, benchi la ufundi pamoja na mashabiki wa timu hiyo kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwa mafanikio ya Simba msimu huu
“Tumshukuru Mungu muweza aliyetaka Simba iwe Bingwa tena”
“Tuwapongeze sana Wachezaji wetu wote, Benchi la ufundi chini ya kocha Patrick Aissems, lakini kipekee tuwashukuru nyie Wanachama na Washabiki wetu ambao mimi nnaamini ndio chachu ya huu ubingwa”
“Kwangu shujaa wa kwanza Simba ni Mshabiki wetu, Tunawashukuru sana”
Simba imetwaa ubingwa leo baada ya kuifunga Singida United mabao 2-0
Mabao ya Meddie Kagere na John Bocco yalitosha kuihakikishia Simba ubingwa baada ya kufikisha alama 91 kwenye msimamo wa ligi
Alama hizo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote katika michezo iliyobaki
Simba imeibuka na ubingwa huku ikiwa na michezo miwili mkononi
BREAKING NEWS: SIMBA WATWAA UBINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA 2018/2019
SIMBA BINGWA LIGI KUU TANZANIA 2018/2019
Simba imefanikiwa kutetea ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo baada ya leo kuichapa Singida United mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Namfua
Mabao ya Meddie Kagere na John Bocco yalitosha kuihakikishia Simba ubingwa wake wa 20
Simba imefikisha alama 91 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine hata kama zitashinda michezo yote iliyobaki

Wachezaji, benchi la Ufundi na viongozi wa Simba wanastahili pongezi kwa mafanikio haya ya kikosi cha Simba
Ubora wa timu, ushirikiano baina ya Wana Msimbazi ndio sababu kubwa iliyopelekea kuibuka na ubingwa wa pili mfululizo
Msimu haukuwa mwepesi kutokana na Simba kushiriki katika mashindano mengi, lakini juhudi za wachezaji zimewezesha kupatikana kwa mafanikio haya
Simba imejihakikishia tiketi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao, mashindano ambayo tayari imepata uzoefu mkubwa msimu baada ya kufika hatua ya robo fainali
Hongera Wachezaji, Hongera Benchi la Ufundi, Hongera Viongozi, Hongera Mashabiki wa Simba……!
Kikosi ambacho kitaanza leo dhidi ya Singida United.
Kikosi ambacho kitaanza leo dhidi ya Singida United. #NguvuMoja #SportPesaChallenge #TukutaneMei23 #TPL


SHEREHE ZA UBINGWA SIMBA KUANZA LEO SINGIDA
Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba wako mkoani Singida ambapo leo watashuka katika uwanja wa Namfua kuikabili Singida United katika mchezo ambao huenda wababe hao wa soka la Tanzania watatawazwa mabingwa
Simba inayoongoza ligi ikiwa na alama 88, inahitaji alama moja tu katika mchezo huo ili iweze kurudi na kombe jijini Dar es salaam
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wataingia katika mchezo huo kusaka ushindi ingawa wanafahamu pointi moja itatosha kutimiza lengo la kutwaa ubingwa
“Tuko hapa kwa ajili ya kusaka ushindi, Nawakaribisha mashabiki wetu waje kwa wingi uwanjani kutuunga mkono ili tuweze kutimiza lengo la kutwaa ubingwa leo,” amesema Aussems









