Ratiba ya mechi ya leo Ligi Kuu Tanzania

: *BREAKING NEWS*
*SIMBA SC yatuma Malalamiko CAF Mechi dhidi ya TP MAZEMBE – LUBUMBASHI*
Tumetuma malalamiko dhidi ya @CAF_Online kwa kufanya mabadiliko ya waamuzi wa mchezo wa marudiano…..
*FULL STORY Ndani Ya SIMBA SC NEWS APP*
*Bofya link hii*👇👇👇👇
https://play.app.goo.gl/?link=https://play.google.com/store/apps/details?id=com.simba.news&ddl=1&pcampaignid=web_ddl_1
👆👆👆👆👆👆
Download App hii ya SIMBA SC NEWS kupata Habari Zote Za MICHEZO
Gusa link hyo juu
#SIMBA_SC
#Jasholadamulubumbashi
#NGUVU_MOJA

🦁🦁🦁🦁

Gadiel, Ninja waongeza nguvu Yanga

Beki kisiki wa Yanga Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amemaliza adhabu baada ya kukosa michezo mitatu hivyo yuko huru kuwatumikia vinara hao wa ligi kuu katika mchezo dhidi ya African Lyon

Kesho Jumatatu, Yanga itashuka katika dimba la CCM Kirumba kucheza mchezo wake wa kwanza wa nyumbani wakiwa nje ya jiji la Dar es salaam

Aidha beki wa upande wa kushoto Gadiel Michael Mbaga aliyekuwa Afrika Kusini kufanya majaribio kunako klabu ya Bidvest Wits, amerejea na huenda akawemo katika kikosi kitakachoikabili African Lyon kesho

Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ndanda Fc kwenye mchezo uliopita, Yanga itakuwa ikisaka matokeo muhimu ya ushindi ili kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi

Kampeni ya changia Yanga yazinduliwa kwa kishindo, mamilioni yakusanywa

Hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kuichangia Yanga iliyosimamiwa na Kamati Maalum iliyoundwa chini ya Mh Anthony Mavunde, ilifanyanyika kwa mafanikio makubwa Hotel ya Morena jijini Dodoma

Hafla hiyo iliyorushwa ‘mbashara’ na Azam Sport 2, iliwajumuisha wadau wa Yanga ambapo kupitia hafla hiyo fedha, ahadi na uhamasishaji mkubwa ulifanyika ili kuhakikisha Yanga inafikia lengo la kukusanya fedha za kutosha kwa ajili ya kukiboresha kikosi cha timu hiyo

Akifungua hafla hiyo, Mwenyekiti wa Kamati Mh Mavunde alisema Kamati imeandaa mfumo mzuri wa kuwezesha upatikanaji wa fedha zitakazofanikisha mipango ya timu hiyo

“Lengo la kamati hii ni kuandaa mfumo mzuri utakaowezesha kupatikana pesa itakayofanikisha mipango ya timu yetu ikiwemo mwalimu kusajili wachezaji wazuri kwa msimu ujao,” alisema

Mavunde aliwataja miongoni mwa wajumbe wa Kamati hiyo ambao anaamini kutokana na ushawishi wao katika jamii, wataweza kuharakakisha kukamilika kwa mpango huo

“Kamati yetu ina wajumbe takribani 28, na wengine ni watu wenye ushawishi katika maeneo mbalimbali.

“Lutawatangaza hapa kila mjumbe na mkoa atakaoratibu”

“Yupo Masoud Kipanya, Jokate Mwegelo, Said Ntimizi, Maulid Kitenge, Papaa Ndama na kipenzi cha wana Yanga Abdallah Bin Kleb na wengineo.

“Tumejipanga vema, wapenzi wa Yanga mna wajibu mkubwa wa kuinga mkono kamati hii ili kufikia malengo yaliyoanishwa”

Miongoni mwa wageni waliohudhuria hafla hiyo ni Mh Mwigulu Nchamba Rais wa klabu ya Singida United ambaye ni mdau mkubwa wa klabu ya Yanga

Nchemba ameahidi kusajili mchezaji mwingine kama alivyofanya kwa Feisal Salum na amemtaka kocha Mwinyi Zahera ampe jina la mchezaji mmoja miongoni mwa wachezaji nane wa kigeni ambao amepanga kuwasajili

“Kwa mara ya kwanza nimekaa na kuongea na Mwalimu wetu, hakika ana maono ya mbali na timu yetu,” alisema

“Naahidi kuendelea kuichangia klabu yangu na naomba mwalimu anipe jina la mchezaji mmoja ntamsajili kama nilivyomsajili Fei Toto”

Wengine waliotoa ahadi kubwa ni pamoja na Mh Hussein Bashe ambaye ameahidi kutumia vyombo vyake vya habari kuitangaza bure kampeni ya kuichangia Yanga

Mh Bashe pia alichangia Fedha Taslim kiasi cha Tsh Milioni 10

Mdau mwingine wa Yanga Cyprian Musiba alichangia Mil moja huku pia akiahidi kuitangaza bure kampeni ya kuichangia katika vyombo vyake vya habari

Yanga huenda ikakusanya zaidi ya Mil 500 baada ya hafla ya jana kutokana na fedha taslim na ahadi zilizotolewa

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ni miongoni mwa wageni walioalikwa kwenye hafla hiyo

Uzinduzi Changia Yanga kufanyika Dodoma leo

Kamati maalumu ya uzinduzi na uhamasishaji inayoongozwa na Mwenyekiti Mh Anthony Mavunde, leo itazindua rasmi kampeni ya kuichangia Yanga katika hafla itakayofanyika Hoteli ya Morena jijini Dodoma

Hafla hiyo itahudhuriwa na wabunge, wafanyabiashara, wasanii na watu maarufu ambao ni wadau wakubwa wa klabu Yanga

Itaanza saa 12 jioni

Naibu Spika akataa ombi la wabunge kukatwa posho kuichangia Yanga

Naibu Spika wa Bunge, Dk.Tulia Ackson, amekataa ombi la Mbunge wa Nkasi, Ally Kessy (CCM) kuhusu wabunge kukatwa sehemu ya posho zao kuichangia Klabu ya Yanga.

Baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali bungeni mjini Dodoma asubuhi ya leo, mbunge huyo alisimama na kuomba mwongozo wa Kiti cha Spika, wabunge wakatwe Sh. 100,000 kila mmoja katika posho yao ya leo ili kuichangia klabu hiyo inayokabiliwa na ukata.

Hata hivyo ombi hilo lilikataliwa na Naibu Spika baada ya wabungwe waliokuwa wengi kupinga hoja hiyo

Wanayanga wameendelea kufanya juhudi za kuichangia timu yao ili kuiwezesha kupita salama katika kipindi cha mpito

Nasumbuliwa na nyonga, hayo mengine tuyapuuze – Ajib

Nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib amesema kukosekana kwake kikosini kunatokana na maumivu ya nyonga ambayo yamekuwa yakimsumbua siku za hivi karibuni

Ajib hakujumuishwa kwenye kikosi cha Yanga ambacho kiko Mtwara kesho kikitarajiwa kucheza na Ndanda Fc. Pia alikosa mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Alliance Fc

Aidha kuhusu taarifa zinazotawala katika vyombo vya habari kuwa yuko mbioni kurejea Simba, Ajib amesema ukweli au uongo wa taarifa hizo utafahamika msimu ukimalizika

“Mimi nina mkataba na klabu ya Yanga, nitaendelea kuitumikia timu yangu. Hizo taarifa za mimi kusajiliwa na Simba ukweli au uongo wake utafahamika mwishoni mwa msimu”

“Mimi ni mchezaji wa Yanga ni vyema nikaulizwa mambo yanayoihusu Yanga, hayo mengine tuwaachie wanaotumia kalamu zao kujinufaisha kwa kuuza magazeti lakini ifahamike mimi ni mchezaji wa Yanga,” Ajib amenukuliwa na Mwanaspoti

Kwa siku za karibuni baadhi ya magazeti yameripoti kuwa Ajib tayari amemalizana na mabosi wa Simba ambao wamemtengea mkataba wa miaka miwili

Hata hivyo hivi karibuni kaka yake Athumani Ajib ambaye ndiye wakala wake, alikanusha taarifa hizo huku akibainisha kuwa wamefanya mazungumzo ya mkataba mpya na Yanga lakini wamekubaliana ni vyema wakasubiri mpaka mwishoni mwa msimu ndio aweze kusaini mkataba mpya

Ni kawaida kwa wachezaji wa soka Tanzania kusubiri mikataba yao imalizike kabisa kabla ya kusaini mikataba mipya.

Utaratibu huo wamekuwa wakiutumia ili kujiongezea thamani hasa inapotokea timu zaidi ya moja zimewasilisha ofa ya kutaka kuwasajili

Gadiel arejea kutoka Afrika Kusini

Beki wa pembeni wa Yanga Gadiel Michael amerejea nchini mapema baada ya kumaliza majaribio yake katika klabu ya Bidvest Wits inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini

Gadiel aliondoka wiki iliyopita kwenda Afrika Kusini baada ya kupata mwaliko kutoka Bidvest

Bado hakuna taarifa iliyotolewa kama amefuzu majaribio hayo au la