Msafara wa wachezaji, benchi la ufundi, baadhi ya viongozi wa klabu ukiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambaye pia ni Mwenyekiti Kamati ya Mashindano, Ahmed Mgoyi umewasili salama mjini Algiers, Algeria na kupokelewa na Balozi wa Tanzania wa Algeria, Omary Mzee. #NguvuMoja
MBWANA SAMMATA : Azidi kukimbiza ULAYA
Mchezaji MBWANA SAMMATA Ameingia kwenye Top 5 ya waliofunga magoli mengi Kwenye Michuano Yote


Credit: #Sokaonline
TANZANIA U17 3-2 AUSTRALIA U17
Full Time. Well Done Boys 🔥#UEFAASSIST
KAGERE: Aibuka Mchezaji BORA | Mwezi Februari | TUZO
Mshambuliaji wa timu ya Simba, Meddie Kagere amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019.

Kagere raia wa Rwanda ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Salim Aiyee wa Mwadui na Salum Kimenya wa Prisons alioingia nao fainali.

Kamati ya Tuzo pia imemchagua Kocha wa Prisons ya Mbeya, Mohamed Rishard kuwa Kocha Bora wa mwezi Februari akiwashinda Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems na Kocha Mkuu wa Mwadui, Ally Bizimungu.
Aliyemshika ‘MAKALIO’ Gadiel Michael Apewa ADHABU HI
Maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ALLIANCE FC
YANGA vs ALLIANCE FC : Robo Fainali ASFC
Hii itakuwa mara ya tatu kwa Yanga kuchuana na Alliance Fc msimu huu, mara ya pili kwa timu hizo kuchuana uwanja wa CCM Kirumba kwenye mwezi huu wa tatu
Kagera Sugar itakuwa nyumbani kuchuana na Azam Fc katika mchezo mwingine wa robo fainali wakati KMC itakuwa mwenyeji wa African Lyon.
Mchezo mwingine ni kati ya Lipuli Fc itakayokuwa nyumbani kupepetana na Singida United
Juuko ana kadi tatu za njano, Okwi mgonjwa, Nyoni hayuko ‘fit’
Wakati Okwi aliondolewa kikosini kutokana na kuwa hajapona vizuri majeraha yake, Juuko anatumikia adhabu ya kadi za njano
Baada ya mchezo dhidi ya Stand United, kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems alitaja sababu ya kutomtumia beki Erasto Nyoni ambaye ameanza mazoezi hivi karibuni akitoka kwenye majeraha ya goti
Aussems alisema Nyoni bado ‘hayuko fit’ na atahitaji muda zaidi ili kuweza kurejea kwenye kiwango chake.
Kutokana na umuhimu wa mchezo dhidi ya JS Saoura, Aussems amelazimika kusafiri na wachezaji ambao wana utimamu wa mwili kwa asilimia 100
Msafara wa Simba walala Dubai, kuendelea na safari leo

Simba inakwenda Algeria kuumana na JS Saoura kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa raundi ya tano utakaopigwa Jumamosi March 09, saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki
Magazeti ya leo, Jumatano, March 06 2019

















Magazeti
Baada ya kutolewa Champions League, Real Madrid wamepata pigo jingine
Wakatia club ya Real Madrid pamoja na mashabiki wao wakiwa katika majonzi mazito kutokana na timu yao kuondolewa mapema katika michuano ya UEFA Champions League msimu wa 2018/2019 tofauti na ilivyozoeleka, kuna habari mbaya pia imeripotiwa leo kuhusiana na moja kati ya wachezaji wao ambaye wanamtegemea pia.

Club ya Real Madrid leo imepokea taarifa za kuthibitika kuwa itamkosa kwa miezi miwili Vinicius Jr, hiyo inatokana na staa huyo kupata majeraha wakati wa mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League dhidi ya Ajax mchezo ambao umemalizika kwa Real Madrid kuvuliwa Ubingwa na kuaga rasmi michuano hiyo 4-1 (agg 5-3).

Jeraha alilolipata Vinicius Jr mwenye umri wa miaka 18 kitaalam linajulikana kwa jina la torn ligaments, kama utakuwa unakumbuka vizuri Vinicius Jr alijiunga na Real Madrid 2018 akitokea Flamengo lakini amepata jeraha kubwa litakalomuweka nje kwa kipindi cha miezi miwili









