De light atua Rasmi Paris sant Germany kwa mkataba wa miaka 5

credit: @sokawaytz…

– Rasmi!! Matthijs De Ligt leo amepokea ofa rasmi ya mkataba kutoka Klabu ya Paris Saint-Germain ambao ni Mabingwa wa Ufaransa; Ofa hiyo ni kwa Mkataba wa miaka mitano na Mshahara wa Β£350k kwa Wiki.

.

– Kwa mujibu wa @fabriziorom, Wakala Wake, Mino Raiola sasa yuko Paris, Ufaransa kuanza mazungumzo na mkurugenzi mpya wa PSG, Leonardo. Mchezaji huyo lakini bado hajaamua juu ya klabu yake ijayo wapi atatimkia, lakini PSG inatajwa kutaka kumaliza dili hilo mapemaa kabla ya Miamba wengine hawajapanda dau.. De Ligt anasubiri kama vilabu vingine (zaidi ya Barcelona, kuliko Manchester United au Liverpool ambapo hawezi kwenda) watawasilisha dau lingine Baada ya na hapo basi atatangaza uhamuzi wake.. πŸ‡³πŸ‡±πŸ”΅

#deligt #psg #mufc #lfc #barcelona #transfers

@Sokawaytz

Pogba hauzwii !!!!⚽️

credit: @simbamakini…

Manchester United imeiambia Real Madrid kuwa kiungo wao Paul Pogba hauzwi kwa dau lolote. Madrid wamepanga kuimarisha kikosi chake ili kurejesha makali yao yaliyopteza katika misimu miwili iloyopita.

Madrid itamshawishi Pogba kuomba barua ya kuondoka (Transfer request) ili kupata nafasi ya kumsajili la sivyo haitawezeka kupata saini yake kwakua United imewakomalia.

Rwandamila Amtaka Beno kakolanya zesco united

credit: @sokaonline_…

Klabu ya Zesco Utd rasmi imeanza harakati za kuinasa saini ya golikipa aliyeachana na Yanga Beno Kakolanya ikiwa ni pendekezo la kocha wa timu hiyo George Lwandamina. .

.

Lwandamina ameithibitishia @sokaonline_ kuwa ni kweli anamhitaji kwa kuwa anatambua uwezo wake tangu akiwa Yanga hivyo endapo watafikia makubaliano basi atahakikisha anatua klabuni hapo. .

.

Lakini huenda Zesco Utd wakapata wakati mgumu kumpata kutokana na Simba Sc nao kuhitaji huduma yake.

Bernado silva atangazwa kua mchezaji bora wa Eufa national league

credit: @sokawaytz…

– Bernardo Silva πŸ‡΅πŸ‡Ή ametangazwa kuwa Mchezaji bora wa Mashindano ya UEFA Nations League yaliyofikia tamati jana kwa upande wao Kuwa Mabingwa.. Kiungo huyo Msimu huu kwa Klabu @mancity na timu ya taifa @portugal πŸ”₯

:

🏟 58 Games

⚽ 14 Goals

🎯 17 Assists

πŸ₯‡ UEFA Nations League

πŸ₯‡ Premier League

πŸ₯‡ FA Cup πŸ₯‡ League Cup

πŸ… @UEFAEURO Nations League Player of the Tournament.

πŸ… @ManCity POTY.

#NationsLeague #Updates

Portugal (ureno) yatwaa ubingwa wa Eufa national league

credit: @sokawaytz…

OFFICIAL: Ureno wametwaa Ubingwa wa Michuano ya UEFA Nations League Baada ya kuibuka na Ushindi wa Goli 1-0 katika Mchezo wa fainali dhidi ya Uholanzi.. Ureno wametwaa Kombe hili katika Ardhi yao ya nyumbani… Goli Pekee la GonΓ§alo Guedes limewapa Ubingwa πŸ‡΅πŸ‡Ή.

.

– Ureno wamekua mabingwa mara mbili kwenye mashindano manne yaliyopita waliyoshiriki, Baada ya kubaba UEFA EURO 2016, na Mwaka huu 2019 wametwaa kombe hili La UEFA Nations league.

.

– Portugal imekuwa timu ya kwanza kutoka Ulaya kuandaa na kushinda Ubingwa wa Mashindano makubwa ya Ulaya tangu Ufaransa walipotwaa Ubingwa wa Dunia 1998 wakiifunga Brazil 3-0..

.

– Netherlands Sasa wamepoteza fainali Nne Kati ya tano za Mashindano makubwa yaliyopita kwa wao kufika fainal.. 3⃣ Kombe La Dunia na 1⃣ Nations League..Netherlands pia wameendelea kuwa dhaifu mbele ya Portugal wakuwa huko huko Portugal.. D2, L4 katika games 6⃣ walizokutana..

#NationsLeague #Updates

@Sokawaytz

Simba na yanga zajitoa mashindano ya cecafa ,yatakayofanyika Rwanda mwaka huu

credit: @sokawaytz…

✍🏻 Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amesisitiza kuwa mashindano ya Kombe la Kagame yatafanyika kama ilivyopangwa licha ya vilabu kujitoa kwa Sababu Mbalimbali; Mabingwa wa Tanzania, Simba SC, walikuwa wa kwanza kutangaza kujitoa katika Mashindano hayo wiki iliyopita, na leo Jumapili wapinzani wao, Yanga SC pia wamethibitisha kuwa hawatoshiriki katika mashindano hayo ya kikanda.. Jana Mabingwa wa Burundi, Agle Noir FC waliandika barua ya kujitoa.

.

– Mechi za Mashindano haya zinatarajiwa kufanyika jijini Kigali, Rwanda kuanzia Julai 7 mpaka Julai 21..

πŸ—£ (Simba na Yanga) “Haishangazi hata wanapopigwa katika mashindano ya CAF, mara zote hupoteza kwa 5-0 au hata 6-0, hatufadhaiki wala haitukwamishi kwa kujitoa kwao”… Alisema Musonye ambapo Pia amesisitiza kuwa tayari wana timu kadhaa kutoka Kenya, Uganda, Rwanda na DR Congo ambazo zitakuja na kujaza nafasi hizo timu mbili za Tanzania.

πŸ—£ “Mashindano hayawezi kushindwa kufanyika kwa sababu ya Yanga na Simba hawapo, na tayari tumezungumza na timu Mbalimbali kuja kushiriki badala yao, Lengo letu ni kuwa na mashindano ya timu 16 na tutasimamia yawe hivyo” Musonye amesema.

.

✍🏻 Zesco United ya Zambia, AS Vita Club na DC Motema Pembe za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wao tayari wamethibitisha ushiriki wao pamoja na Azam FC ya Tanzania… Mashindano huleta timu kutoka Kenya, Rwanda, Burundi, Djibouti, Eritrea, Sudan, Somalia, Sudan Kusini, Ethiopia, Uganda, Tanzania na Zanzibar… Mshindi wa mashindano haya atarejea nyumbani kwake na kitita cha pesa ya thamani ya US$30,000..

#Updates #kagameCup

@Sokawaytz

Kamusoko aitwa Kikosi cha Zimbabwe Afcon

credit: @sokawaytz…

– Hongera kwao Viungo mahiri, @kamusoko_13 na @tafadzwakutinyu kwa kuwepo katika Kikosi cha mwisho cha Wachezaji 23 ambao watapeperusha Bendera Zimbabwe katika fainali za Mataifa ya Afrika AFCON mwezi huu nchini Misri.. Vijana hao wa kocha Sunday wapo kundi La A pamoja na mataifa ya Uganda, DR Congo na wenyeji Misri.

#TotalAFCON2019 #AFCON2019