Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema Simba imetawazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Uinted

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema Simba imetawazwa rasmi kuwa mabingwa wa Ligi Kuu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Uinted

Ushindi huo uliiwezesha Simba kufikisha alama 91, alama ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine

Wambura amesema Simba walikuwa na timu imara, walionekana kudhamiria kutwaa ubingwa huo tangu mwanzoni mwa msimu

Simba itakabidhiwa kombe keshokutwa Jumamosi, baada ya mchezo dhidi ya Biashara United utakaofanyika uwanja wa Uhuru

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO ALHAMISI

Nahodha wa zamani wa England na Chelsea John Terry, ambaye kwa sasa ni naibu meneja wa Aston Villa, anashauriana na Middlesbrough kuhusu uwezekano wa kuwa maneja wao mpya.(Talksport)

Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa Ureno Joao Cancelo, 24, ambaye thamani yake inakadiriwa na Juventus kuwa euro milioni 60. (Record – in Portuguese)
Atletico Madrid na Napoli wanapania kumsajili beki wa kulia wa Tottenham na mchezaji wa kimataifa wa England Kieran Tripper, 28. (Mirror)

Spurs wameweka dau la £10m kumnunua winga wa Leeds United wa miaka 18, Muingereza Jack Clarke. (Mail)
Manchester United wanashughulikia mpango wa kumsaini Ivan Rakitic, 31, lakini Barcelona wanataka kulipwa uero milioni 48 kumwachilia nyota huyo wa kimataifa wa Croatia. (Record)

Ivan RakiticHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption Ivan Rakitic
United wanatarajiwa kuwasilisha dau la kwanza la £25m kumunua beki wa Crystal Palace, Aaron Wan-Bissaka, 21, lakini Eagles wanataka £50m kumwachilia mchezaji huyo. (Evening Standard)

Muargentina Sergio Romero, 32, huenda akapandishwa cheo kuwa kipa wa Manchester United ikiwa David de Gea, 28, ataondoka Old Trafford msimu huu wa joto. (Mail)
United tayari wamewasilisha rasmi ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21. (ESPN)
Everton, West Ham na Manchester United wamepewa nafasi ya kumsaini kwa mkopo kiungo wa kati wa Uholanzi na Marseille Kevin Strootman, 29. (Sky Sports)
Romelu LukakuHaki miliki ya pichaREUTERS
Image caption Romelu Lukaku
Antonio Conte anatarajiwa kusajili mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 26, kutoka Manchester United atakapoajiriwa kama meneja wa Inter Milan. (Times – subscription required)

Liverpool wanakaribia kukamilisha mpangowa £200,000 wa kumsajili kipa raia wa Poland Jakub Ojrzynski, 16, kutoka Legia Warsaw. (Liverpool Echo)
Wolves wanaongoza kinyang’anyiro cha kumsaini mshambuliaji Moussa Marega, 28 rai wa Mali ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £30m-kutoka Porto. (Mirror)

Wales forward Harry WilsonHaki miliki ya pichaBBC SPORT
Newcastle, Southampton na Brighton wote wanataka kusaini winga Harry Wilson, 22, lakini Liverpool wanataka kulipwa £25m kumwachilia nyota huyo wa kimataifa wa Wales. (Sky Sports)

Bournemouth wako tayari kupokea ofa ya kummuuza winga Jordon Ibe, 23 raia wa Uingereza. (Mirror)

FIFA wamebariki Qatar kuwa mwenyeji wa World Cup 2022 kwa timu 32 sio 48

Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA limetangaza kuwa imelazimika kuacha michuano ya World Cup 2022 itakayofanyika nchi Qatar kuwa na timu 32 na sio 48 kama ambavyo ilikuwa inatarajiwa awali, taarifa hizo rasmi zitatolewa June 5 2019 katika mkutano wa FIFA Paris Ufaransa.
Inaelezwa kuwa Qatar wamekuwa wakijipanga kuwa wenyeji wa timu 32 toka 2010 na hata maandalizi yao yalikuwa yanalenga kutumia viwanja nane vilivyoandaliwa tayari, hivyo kwa miaka mitatu iliyosalia Qatar hawezi kumudu ongezeko la timu kutoka 32 yaliokuwa matarajio yao hadi 48.

Rais wa FIFA Infantino

Hata hivyo wazo la timu 48 linabakia kuwa kama wazo litakaloanza kufanya kazi rasmi 2026 katika fainali za Kombe la Dunia litakalokuwa na wenyeji watatu United States, Canada na Mexico, sababu za kisiasa ndio zimeleta utata kwa Qatar kukubali ongezeko la timu na kuwa mwenyeji kwa ushirikiano na mataifa jirani.

Mwinyi Zahera amewapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City

Licha ya kuwakosa wachezaji saba wanaougua Malaria, kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City

Zahera amesema katika mchezo wa leo alitumia wachezaji wanne kutoka katika kikosi cha U20

“Tulikosa wachezaji wetu saba wanaumwa Malaria, nimetumia vijana wanne wa U20, nafurahi wachezaji wameweza kutupatia matokeo,” amesema

“Tulitengeneza nafasi nyingi, tulipaswa kufunga mabao zaidi, nafikiri leo hatukuwa na nidhamu ya mchezo”

Kuhusu maoni yake baada ya Simba kutwaa ubingwa jana, Zahera ameshikilia msimamo wake kuwa hawakustahili kutwaa ubingwa kutokana na upindishwaji mkubwa wa sheria uliofanywa kuwawezesha washinde taji hilo

“Simba waliwapa ubingwa jana, maoni yangu mie nilicheza mpira ambao uko na sheria, ule sio ubingwa,” amesema

“Ninapoishi nakaa na watu wa Simba, wananiambia kweli hata kama mpira wetu tunapenda Simba, tunaona kama sio hivyo”

“Tunapata kikombe lakini ukiangalia sheria kabisa mwaka huu hatungepata kikombe”

Wadau mbalimbali wametoa maoni tofauti juu ya ubingwa wa Simba

Wakati wengine wakiamini kuwa Simba ilistahili ubingwa huo, wapo wanaoamini mazingira yaliyotengenezwa na TFF kwa kuiacha timu hiyo isicheze mpaka michezo 12 wakati nyingine zikiendelea na ligi, yameirahisishia timu hiyo kutwaa ubingwa

“Simba walikuwa na michezo 12 ya viporo. Walikuwa wanafahamu matokeo ambayo wanatakiwa wapate ili watwae ubingwa, pengine hali ingekuwa tofauti kama wangecheza sambamba na timu nyingine,” amesema Rajabu Issa kutoka Buguruni

“Umeona wapi na ligi gani duniani ambapo timu moja inakuwa na michezo ya viporo 12? kushiriki ligi ya mabingwa haitoshi kuwa sababu ya kurundikiwa michezo mingi kiasi hicho mbona timu walizokuwa wakishindana nazo zilikuwa zikicheza ligi zao?”

“Hawa Simba baada ya kutolewa kombe la FA walipanga mkakati na TFF kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa ligi kuu kupitia ratiba na hujuma kwa Yanga”

“Angalia mchezo dhidi ya KMC ilikuwa wafungwe lakini refa akawatafutia ushindi kwa nguvu halafu baadae TFF wanatangaza kumfungia mwamuzi wakati mpango umeshakamilishwa”

Simba kuweka kambi Marekani au Ureno Pre- Season

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji amesema kuwa bodi ya wakurugenzi imepanga kuipeleka timu hiyo Marekani au Ureno kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Dewji alisema hayo wakati wa kuipongeza timu hiyo kutwaa ubingwa kwa mara ya pili mfululizo na zoezi wapi watakwenda itajadiliwa ndani ya wiki hii.

Alisema kuwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara mbili mfululizo ni mafanikio makubwa ambayo yametokana na ushirikiano baina ya viongozi, wanachama, mashabiki na wadau wa soka kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Dewji, Ligi Kuu ilikuwa ngumu na hasa baada ya klabu ya Yanga ilikuwa inaongoza ligi hiyo kwa pointi 21.

“Haikuwa kazi rahisi kutafuta pointi ambazo wapinzani wetu wameweza kupata. Wachezaji waliweza kupigana kiume mpaka kupata ushindi wakiwa na mechi mbili mkononi.

FT: Yanga 1-0 Mbeya City

Yanga imeendeleza umwamba wake katika dimba la Uhuru baada ya kuichapa Mbeya City bao 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa 37

Bao pekee la Yanga lilipatikana kwenye dakika ya 26 likiwekwa kimiani na Heritier Makambo aliyeunganisha kwa kichwa krosi ya Haji Mwinyi

Hilo ni bao la 17 kwa Makambo, akishika nafasi ya pili sawa na Salim Aiyee katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu nyuma ya Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao 23

Licha ya kuwakosa nyota wake wengi ambao ni wagonjwa na majeruhi, Yanga ilitandaza kandanda safi na kutawala mchezo huo kwa muda mwingi

Kiungo kinda Gustapha Simon ameendelea kudhihirisha ubora wake, hakuna shaka msimu ujao atapata nafasi zaidi kwenye kikosi cha Zahera

Yanga imefikisha alama 86 sasa ikibakiwa na mchezo mmoja wa kumaliza msimu dhidi ya Azam Fc

Mchezo huo utapigwa May 28 2019

MO DEWJI

“Niwapongeza na kuwashukuru wachezaji wamejitolea kwa namna moja au nyingine hadi tunaupata huu ubingwa, niwashukuru wanachama na wapenzi wote wa Simba kwa kujitokeza kutushangilia.”- Mo Dewji
.

“Kocha ameshafikia malengo tuliyomuwekea tulikuwa tunataka ubingwa na kufika kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa, Mungu akitujalia kwenye wiki moja tutakaa nae tumuongeze mkataba … tutamueleza sehemu ambazo kuna mapungufu ili aendelee kufanyia kazi”- Mo Dewji
.
“Tunaanza kupanga maandalizi ya msimu, mimi binafsi naongea na timu za Ulaya na Marekani… kuna rafiki yangu anamiliki DC United nimeongea nae watualike tukafanye maandalizi Marekani, kuna uwezekano wa kwenda Ureno, kwenye wiki mbili zijazo tutajua timu itakwenda wapi”- Mo Dewji
.

“Kwenye mechi ambayo tutacheza kesho naomba niwashukuru sana SportPesa, hii ni mara ya kwanza kwa timu kutoka ligi kuu ya Hispania kuja kucheza Tanzania, ni historia kubwa kwa nchi yetu, tupo tayari kucheza na Sevilla, naomba mashabiki tujitokeze kwa wingi sana”- Mo Dewji
.
“Simba itakuwa kwenye soko kushindinda na Al Ahly, Zamalek, TP Mazembe kushindana kutafuta wachezaji wenye vipaji, tupo tayari kuwabakisha wachezaji ambao mwalimu atapendekeza, wengine watatoka kwa mkopo … bajeti ya mwaka huu itakuwa kubwa kuliko mwaka jana”- Mo Dewji
.

“Katika mechi ya kesho ya Sevilla nawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi ili na sisi tuweze kuwaonyesha mpira wa Ulaya”- Mwenyekiti wa klabu, Swedi Mkwabi.
#NguvuMoja #SportPesa Challenge #TukutaneMei23