Yanga hakuna kulala, yajifua kuikabili Kagera Sugar

Licha ya kushuka dimbani jana, vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga wanakabiliwa na mchezo mwingine dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa keshokutwa Alhamisi April 11 2019 kwenye uwanja wa CCM Kirumba

Kikosi cha Yanga leo kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa CCM Kirumba kujiandaa na mchezo huo

Kocha Mwinyi Zahera amesema watahakikisha wanashinda michezo yote nane iliyobaki ili kujiwekea mazingira ya kutwaa ubingwa kwani anaamini upo uwezekano mkubwa kwa Simba kupoteza baadhi ya michezo kutokana na ugumu wa ratiba itakayowakabili kama TFF haitawapendelea

Hawa hapa waliochukua fomu za kuwania uongozi Yanga

Jana April 07 2019 ndio ilikuwa siku ya mwisho kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika klabu ya Yanga kurudisha fomu.

Wagombea 28 walichukua na kurudisha fomu ndani ya muda uliopangwa

Hii hapa orodha ya wagombea wote kulingana na nafasi zao;

MWENYEKITI

Dk Mshindo Msolla

Lucas Mashauri

Elias Mwanjala

MAKAMU MWENYEKITI

Mh Janeth Mbena

Samwel Lukumay

Thobias Lingalangala

Fredrick Mwakalebela

WAJUMBE

Ally Sultan

Saady Mohammed

Hassan Hussein

Siza Lymo

Dminick Albinus

Seko Kingo

Hamad Islam

Shafiru Makosa

Eng Leonard Malango

Cyprian Musiba

Eng Bahati Mwaseba

Nasoro Ally Matuzya

Abdallah Chikawe

Hussein Nyika

Rdgers Gumbo

Said Ntimizi

Palina Conrad

Elias Mkumbo

Suma Mwaitenda

Seif Hassan Seif

Haruna Batenga

NB:

Orodha hii haijumuishi wagombea waliopitishwa kwenye mchakato wa mwanzo wa kujaza nafasi zilizowazi

Simba ina malalamiko ya msingi kubadilishwa kwa waamuzi

Kikosi cha Simba kikiendelea na maandalizi ya kujifua kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya TP Mazembe itakayochezwa Lubumbashi DR Congo uongozi wa timu hiyo ulipokea taarifa ya ghafla na kushtushwa.

Uongozi wa Simba umepokea taarifa hiyo kutoka kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwa wamebadilisha waamuzi waliopangwa hapo awali kuchezesha mchezo wa marudiano kati ya TP Mazembe na Simba utakaochezwa Aprili 13.

Awali CAF ulitangaza waamuzi wa mechi ya kwanza kati yao ambayo ilichezwa hapa Dar es Salaam Aprili 6, na wengine ambao watachezesha mchezo wa marudianio.

Waamuzi wa awali waliopangwa na CAF, kuchezesha mchezo wa marudiano TP Mazembe na Simba ni Bamlak Tessema mwamuzi wa kati kutoka Ethiopia, Temesgin Samuel msaidizi namba moja kutoka Ethiopia, Gilbert Kipkoech Cheruiyot msaidizi namba mbili kutoka Kenya.

Wengine ambao walipangwa awali na CAF, mwamuzi wa akiba Peter Waweru kutoka Kenya.

Katika barua ambayo ilionyesha inatoka CAF, ambayo uongozi wa Simba uliipokea Aprili 7, ilisema kuwa waamuzi hao walibadilishwa kwa sababu ya kiiufundi ingawa hawakuziweka wazi.

Baada ya CAF kufanya mabadiliko waamuzi wapya waliopangwa Janny Sikazwe kutoka Zambia atayekuwa mwamuzi wa kati, Berhe Tesfagiorgis kutokea Eritrea atakuwa msaidizi namba moja, Romeo Kasengele kutokea Zambia atakuwa msaidizi namba mbili, Audrick Nkole kutokea Zambia atakuwa mwamuzi wa akiba.

Wakati Aimable Habimana kutokea Burundi atakuwa Kamishna, Salah Ahmed kutokea Sudan atakuwa msimamizi wa waamuzi.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori alisema wanafahamu miongoni mwa wamiliki wa timu hiyo Moise Katumbi shughuli zake nyingi huwa anafanya nchi Zambia ambapo waamuzi wa wapya waliopangwa kuchezesha mchezo huo wanatoka nchini humu.

Magori alisema awali walishapangwa waamuzi wa kuchezesha mechi zote mbili inakuaje baada ya mchezo wa kwanza umeshachezwa na matokeo yake kufahamika ndio wabadili waamuzi waliopangwa kuchezesha mechi ya marudiano.

Alisema tumeandika barua CAF, kuwalalamikia kuwa hatujalisishwa na jambo hili na atukubali kabisa kwa hali ya kawaida jambo hilo la kubadili waamuzi na kulinganisha ukubwa wa mechi na matokeo ya kwanza yalivyokuwa lazima timu yoyote itakuwa na mashaka.

“Kwa hali ya kawaida ukaribu wa Ndola Mji ambao ata mwamuzi mpya Sikazwe ambaye amepangwa kuchezesha mchezo wetu anatumia saa mbili tu kwa gari mpaka kuingia Lubumbashi DR Congo ambapo tutacheza mechi ya marudiano.

“Ukaribu huu wa waamuzi wapya kiukweli uongozi wa Simba umefikisha malalamiko CAF, ili kuweza kulishuhurikia jambo hili kabla ya mchezo wetu wa marudiano,” alisema Magori.

Cc: Mwanasport

SIMBA – Shabiki Aliyetembea MBEYA -DAR Apata Shavu

Shabiki Ramadhan Mohamed ambaye alikuja Dar es Salaam akitokea Mbeya kwa miguu ili ashuhudie mchezo wa robo fainali ya #CAFCL dhidi ya TP Mazembe, leo amekutana na viongozi, wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na sekretarieti ambapo amehaidiwa kugharamiwa na klabu kwenda Lubumbashi kuangalia mchezo wa marudiano ambao utachezwa Jumamosi Aprili 13, 2019. #NguvuMoja

Kikosi : Yanga Vs African Lyon, TPL

Hiki hapa kikosi cha Yanga mchezo dhidi ya African Lyon

1. Klaus Kindoki

2. Juma Abdul

3. Gadiel Michael

4. Andrew Vicent

5. Kelvin Yondani

6. Faisal Salum

7. Mrisho Ngasa

8. Haruna Moshi

9. Heritier Makambo

10. Papy Tshishimbi

11. Pius Buswita

SUB

Ramadhani Kabwili

Said Juma

Jaffar Mohammed

Thabani Kamusoko

Amissi Tambwe

Raphael Daudi

Mohammed Issa

SIMBA Yatuma malalamiko CAF – Mabadiliko ya Marefa

Klabu ya Simba kupitia kwa Mtendaji wake Mkuu Crescentius Magori, imeliandikia barua Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) kufuatia mabadiliko ya waamuzi wa mchezo wa pili wa robo fainali ligi ya mabingwa kati ya TP Mazembe dhidi ya Simba

Mapema leo CAF ilitoa taarifa juu ya mabadiliko hayo ambayo yamefanyika siku tano kabla ya mchezo utakaopigwa April 13 Lubumbashi, DR Congo

TP Mazembe ndio iliyoomba kubadilishwa kwa waamuzi hao

Simba imeeleza hofu yake kwa mabadiliko hayo ya kushitukiza kuwa yasije yakawa na lengo baya

“Tumetuma malalamiko dhidi ya @CAF_Online kwa kufanya mabadiliko ya waamuzi wa mchezo wa marudiano wa #CAFCL ambao tutacheza Jumamosi. / We have formally lodged a complaint against CAF for the abrupt change in referees ahead of match against TP Mazembe in this Saturday in DRC”