Yanga yasaka alama tatu dhidi ya African Lyon leo

Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga leo watakuwa uwanja wa CCM Kirumba kuikabili African Lyon

Huo utakuwa mchezo wa kwanza wa nyumbani kwa Yanga kuchezwa nje ya jiji la Dar es Salaam msimu huu

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema baada ya kulazimishwa sare mchezo uliopita dhidi ya Ndanda Fc, leo wanahitaji alama zote tatu

Viingilio vya mchezo huo ni Tsh 3,000/- kwa majukwaa ya kawaida na Tsh 10,000/- upande wa VIP

Ratiba ya mechi ya leo Ligi Kuu Tanzania

: *BREAKING NEWS*
*SIMBA SC yatuma Malalamiko CAF Mechi dhidi ya TP MAZEMBE – LUBUMBASHI*
Tumetuma malalamiko dhidi ya @CAF_Online kwa kufanya mabadiliko ya waamuzi wa mchezo wa marudiano…..
*FULL STORY Ndani Ya SIMBA SC NEWS APP*
*Bofya link hii*👇👇👇👇
https://play.app.goo.gl/?link=https://play.google.com/store/apps/details?id=com.simba.news&ddl=1&pcampaignid=web_ddl_1
👆👆👆👆👆👆
Download App hii ya SIMBA SC NEWS kupata Habari Zote Za MICHEZO
Gusa link hyo juu
#SIMBA_SC
#Jasholadamulubumbashi
#NGUVU_MOJA

🦁🦁🦁🦁

Simba kuifuata TP Mazembe Alhamisi ijayo

Kikosi cha Simba kitaondoka jijini Dar es salaam Alfajiri ya Alhamisi, April 11 2019 kuelekea DR Congo tayari kwa mchezo wa marudiano, robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe


Uongozi wa Simba umewaalika wapenzi, mashabiki na wanachama wa timu hiyo ambao wangependa kusafiri na kikosi cha Simba nchini Congo, kujiandikisha

Simba inayo nafasi ya kufanya maajabu Congo

Katika michezo minne ya robo fainali ya ligi ya mabingwa iliyopigwa jana, ni Mamelodi Sundowns pekee iliyotumia vyema uwanja wake wa nyumbani kwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Al Ahly

Horoya ililazimishwa suluhu ya bila kufungana na Wydad Casablanca kama ilivyokuwa kwa Simba dhidi ya TP Mazembe

CS Constantine ilikubali kipigo cha mabao 3-2 nyumbani dhidi ya mabingwa watetezi Esperance

Michezo ya marudiano inatarajiwa kupigwa wiki ijayo April 13

Wawakilishi wa Tanzania, Simba watasafiri Lubumbashi DR Congo kuikabili TP Mazembe itakayokuwa nyumbani

Kwenye mchezo huo wa marudiano Simba inahitaji matokeo ya aina mbili ili iweze kutinga nusu fainali

Ushindi au sare yoyote ya mabao itaihakikishia Simba kuingia nusu fainali

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wanao uwezo wa kufuzu ugenini baada ya kufanya tathmini ya mchezo wa jana

Amesema watajipanga wakapambane ugenini kuhakikisha wanapata matokeo yanayoweza kuwapeleka hatua ya nusu fainali

Nitarejea uwanjani karibuni – Wawa

Beki kisiki wa Simba Serge Paschal Wawa jana alilazimika kutoka kwenye dakika ya sita mchezo dhidi ya TP Mazembe baada ya kupata maumuvu ya mguu

Wawa amesema maumivu hayo yalimfanya ashindwe kuendelea na mchezo hata hivyo aliwapongeza wachezaji wenzie kwa kufanikiwa kumaliza mchezo huo bila ya kuruhusu bao

Wawa amesema atarejea kikosini hivi karibuni lakini huenda akaukosa mchezo wa marudiano utakaopigwa wiki ijayo Lubumbashi, DRC

“Nilitoka uwanjani na kuiacha timu yangu inapambana, walinihitaji lakini sikuweza kuendelea kutokana na maumivu niliyokuwanayo hata wakati natembea nilikuwa napata maumivu makali,” alisema Wawa

“Ingawa ninamaumivu makali namwachia Mungu, naamini nitarejea uwanjani hivi karibuni.

“Mchezo wa marudiano utakuwa mgumu lakini ninaimani na wachezaji wenzangu na timu nzima kwa ujumla”

Baada ya Wawa kutoka, nafasi yake ilichukuliwa na Juuko Murshid ambaye alicheza vyema sambamba na kiraka Erasto Nyoni

Bocco asilaumiwe kwa kukosa penati – Aussems

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema matokeo ya suluhu waliyopata dhidi ya TP Mazembe jana yalitokana na timu hiyo kukosa bahati na hakuna jambo jengine

Aussems amesema wachezaji wake jana walicheza kama alivyowaelekeza walitengeneza nafasi nyingi, lakini walikosa bahati

Akizungumzia tukio la nahodha John Bocco kukosa mkwaju muhimu wa penati ambayo huenda ingeiweka Simba katika mazingira mazuri ya kuibuka na ushindi, Aussems amesema Bocco hawezi kulaumiwa kwa kukosa penati kwa kuwa hiyo ni sehemu ya mchezo

“Huwezi kumlaumu mchezaji kwa kukosa penati kwani, hilo ni pigo la bahati pia,” alisema

“Wachezaji wote duniani huwa wanakosa penati hivyo hapaswi kulaumiwa”

Nae msemaji wa Simba Haji Manara amewashukia baadhi ya mashabiki wa timu hiyo ambao wamemshambulia Bocco baada ya mchezo wa jana

Manara amesema Bocco ndiye mchezaji ambaye yuko katika kiwango bora zaidi katika kikosi cha Simba kwa sasa

Kwa siku za karibuni Bocco ameifungia Simba mabao mengi kwenye ligi pamoja na kutoa pasi muhimu bila kusahau amekuwa na rekodi nzuri ya kufunga mikwaju ya penati

“Kumlaumu Bocco kwa kukosa mkwaju wa penati kunasababisha na ugeni wa baadhi ya mashabiki kwenye soka,” amesema Manara

“Bocco huyu ndiye anayefunga penati nyingi za Simba. Hata tulipocheza na Nkana kule Kitwe Zambia, ni Bocco aliyefunga penati muhimu ambayo baadae ilitusaidia kupata matokeo ya kuingia hatua ya makundi”

“penati ni pigo la bahati na halina mwenyewe”

Gadiel, Ninja waongeza nguvu Yanga

Beki kisiki wa Yanga Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amemaliza adhabu baada ya kukosa michezo mitatu hivyo yuko huru kuwatumikia vinara hao wa ligi kuu katika mchezo dhidi ya African Lyon

Kesho Jumatatu, Yanga itashuka katika dimba la CCM Kirumba kucheza mchezo wake wa kwanza wa nyumbani wakiwa nje ya jiji la Dar es salaam

Aidha beki wa upande wa kushoto Gadiel Michael Mbaga aliyekuwa Afrika Kusini kufanya majaribio kunako klabu ya Bidvest Wits, amerejea na huenda akawemo katika kikosi kitakachoikabili African Lyon kesho

Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ndanda Fc kwenye mchezo uliopita, Yanga itakuwa ikisaka matokeo muhimu ya ushindi ili kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi