Nahodha wa kikosi cha Yanga Ibrahim Ajib hajasafiri na timu hiyo kuelekea mkoani Mwanza ambapo keshokutwa Jumamosi itashuka katika uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Alliance Fc kwenye mchezo wa robo fainali, kombe la FA
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema Ajib hakujumuishwa katika kikosi kwa kuwa bado hajawa ‘fit’ tangu apone majeraha ya misuli
Zahera amesema Ajib anahitaji muda zaidi wa kufanya mazoezi ili aweze kuwa tayari kurejea dimbani
Akizungumzia mchezo huo, Zahera amesema wamejiandaa kikamilifu kuikabili Alliance Fc ambayo inaonekana kupania zaidi mchezo huo
“Tunaufahamu ubora wa Alliance Fc na hata udhaifu wao pia tunaujua, hatuna wasiwasi kuelekea mchezo huo,” amesema Zahera
Mcongoman huyo aliyerejea usiku wa kuamkia jana na kuungana moja kwa moja na kikosi cha Yanga, amesema atatumia siku ya leo na kesho kufanya maandalizi ya mwisho tayari kwa mchezo huo utakaopigwa Jumamosi March 30 katika dimba la CCM Kirumba
Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba kesho Ijumaa wanaelekea mkoani Morogoro tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbao Fc
Mchezo huo utapigwa siku ya Jumapili, March 31 katika uwanja wa Jamhuri
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wamedhamiria kutetea ubingwa wao, hivyo wanahitaji kushinda mchezo huo
“Tulipoteza mechi ya kwanza na Mbao Mwanza na sasa tumejipanga kuchukua pointi hizo tatu na kuhakikisha tunaanza kuutumia vyema uwanja wetu wa Jamhuri ambao tunaanza nao katika mchezo huo,” amesema Aussems
Hata hivyo licha maboresho yaliyofanywa, uwanja wa Jamhuri bado hauko katika kiwango bora, hali itakayomfanya Aussems alazimike kubadili mbinu ili kwendana na hali ya uwanja huo
“Kutumia Uwanja wa Jamhuri kama nyumbani hatuna jinsi, kutokana na tayari uwanja wa Taifa umefungwa, lakini kuna tofauti kubwa kati ya viwanja hivi”
“Tutajiandaa kucheza kufuatana na hali ya uwanja, muhimu tunahitaji ushindi”
Aussems amesema kikosi chake kitafanya mazoezi kwenye uwanja wa Jamhuri kesho jioni na pengine Jumamosi asubuhi kabla ya kuikabili Mbao Fc Jumapili
Simba inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 54, huku ikiwa na michezo nane kibindoni
Hesabu za kutetea ubingwa kwa kocha Aussems zinakwenda sawa mpaka sasa kwani kama Simba itashinda michezo yake yote ya viporo, itaizidi Yanga inayoongoza ligi hiyo kwa alama nane
ACHANA na Clatous Chama ambaye alifunga bao lililoipeleka Simba kwenye hatua ya makundi na vilevile akapachika lililoivusha robo fainali.
Kwenye Simba kafanya vizuri lakini Zambia timu yake ya Taifa imechemka. Wameenda kuishukia Namibia mabao kibao yote kazi bure.
Kuna mtu mmoja anaitwa John Bocco. Anastahili heshima ndani ya ardhi ya Tanzania, ameweka rekodi ambayo hata Chama imemshinda pamoja na mbwembwe zake zote.
Ameweka rekodi ya kipekee baada ya kuzisaidia timu mbili za Simba na Taifa Stars kufanya makubwa mwaka huu na kurejesha heshima ya Tanzania.
Bocco ambaye amefunga mabao tisa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, hadi sasa amehusika kwenye kutengeneza mabao matatu muhimu kuliko wachezaji wengine wote wa Tanzania.
Bocco ambaye ni mchezaji wa zamani wa Azam, alianza kazi yake hiyo kwenye mchezo wa Simba dhidi ya AS Vita Club wa kutafuta nafasi ya kucheza hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika mchezo huo, Bocco ndiye alitoa pasi ya bao la ushindi kwa timu yake katika dakika ya tisini ambapo Simba ilipata ushindi wa mabao 2-1 na kwenda robo fainali.
Alipiga pasi ambayo ilirukwa na kiungo Haruna Niyonzima na mpira ukamfikia mfungaji Clatous Chama ambaye aliifungia timu yake bao hilo muhimu na kuipeleka Simba kwenye robo fainali.
Hata hivyo, baada ya kumaliza kazi kwenye klabu yake, Bocco alifanya tena mambo makubwa kwenye mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Uganda ambapo aliipa timu hiyo ushindi tena kwa staili ileile.
Bocco alitoa pasi mbili za mabao kwenye mchezo huo ambao Taifa Stars walipata ushindi wa mabao 3-0.
Mshambuliaji huyo mwenye upeo wa kuchanganua mambo, alitoa pasi ya bao la kwanza na la mwisho, huku lile la pili likifungwa na beki Erasto Nyoni kwa mkwaju wa penalti baada ya mchezaji mmoja wa Uganda kuunawa mpira eneo la hatari.
Pasi hizo mbili ni zile za mabao ya Simon Msuva na Aggery Morris, yaliyoifanya Taifa Stars ifuzu Afcon ambapo fainali zake zinatarajiwa kufanyika nchini Misri kuanzia Juni mpaka Julai, mwaka huu.
Uongozi wa klabu ya Simba tayari umemalizana na mshambuliaji wa Gor Mahia Jacques Tuyisenge ambaye pia alikuwa akiwaniwa na AS Vita Club ya DR Congo
Baada ya kumpoteza mshambuliaji wake Jean Mark Makusu aliyetimkia nchini Morocco, Vita ilikuwa mbioni kumsajili Tuyisenge kuchukua nafasi yake
Hata hivyo Meddie Kagere aliyekuwa ‘pacha’ wa Tuyisenge katika klabu ya Gor Mahia ambaye pia ni pacha wake katika kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda, amechangia kwa kiasi kikubwa kumshawishi Tuyisenge kutua Simba
Simba imempa Tuyisenge mkataba wa awali wa miaka miwili akitarajiwa kuanza kazi mwishoni mwa msimu
Tuyisenge alikutana na mabosi wa Simba juzi usiku katika kikao ambacho kilikuwa na mafanikio kwa pande zote mbili kufikia makubaliano
Barcelona wapo tayari kuwapa Manchester United kiungo Philippe Coutinho, 26, ama Malcom, 22, kama sehemu ya ofa ya kumnasa mshambuliaji Marcus Rashford, 21. (Mundo Deportivo, via Mail)
Klabu ya Borussia Dortmund inasisitiza kuwa haina mpango wa kumuuza mchezaji wao raia wa Uingereza Jadon Sancho, 19, ambaye amekuwa akihusishwa na Manchester United. (Mirror)
Chelsea wanaweza wakasikiliza ofa za usajili za zaidi ya Pauni milioni 43 ili kumuachia mshambuliaji kinda wa Uingereza Callum Hudson-Odoi, 18. (Sport Bild, via Metro)
Leicester hawapo tayari kuwatoa mabeki wake Harry Maguire, 26, na Ben Chilwell, 22, ambao wamekuwa wakinyemelewa na vilabu vikubwa vya Manchester United na Manchester City. (Mirror)
Manchester United hawana mpango wa kumuuza mchezaji wao anayepokea mshahara mkubwa zaidi, Alexis Sanchez, 30, licha ya kutoonesha makali uwanjani na ripoti kuwa suala la mshahara wake linatatiza mapatano ya mkataba mpya na kipa David De Gea. (London Evening Standard)
Beki wa Liverpool Dejan Lovren ananyemelewa na vilabu vikongwe vya Italia, Roma, Napoli na AC Milan ili wamsajili mwishoni mwa msimu. (Mirror)
Manchester City ni miongoni mwa vilabu ambavyo vinamfuatilia kwa karibu winga wa Swansea na Wales Dan James, 21. (Sun)
Mshambuliaji kinara wa klabu ya Tottenham Harry Kane, 25, amesema anataka kucheza kwenye ligi ya Marekani NFL “ndani ya miaka 10 au 12 ijayo”. (ESPN)
Kiungo wa Liverpool na Serbia Marko Grujic, 22, ambaye yupo kwa mkopo katika klabu ya Hertha Berlin, anataka kusalia kwenye klabu hiyo ya Ujerumani walau kwa mwaka mmoja zaidi. (Liverpool Echo)
Mshambualiaji wa raia wa Paraguay Sergio Diaz, 21, atasalia Real Madrid baada ya klabu ya Corinthians ya Brazil, ambako amekuwa kwa mkopo msimu huu kuamua kuwa hawatamnunua. (Marca)
Simba imepania kwelikweli kuboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao! Hilo limedhihirika kutokana na michakato ya usajili kuanza mapema
Juzi Jacques Tuyisenge alikuwa nchini kumalizana na mabingwa hao wa Tanzania Bara akitarajiwa kujiunga nao mwishoni mwa msimu wakati huo huo nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib nae akiwa njiani kurejea nyumbani
Anayefuatia ni beki kisiki wa Azam Fc Yakubu Mohammed. Inaelezwa Yakubu tayari amefikia makubaliano ya awali na uongozi wa Simba na atamwaga wino mwishoni mwa msimu
Kakolanya nae safi
Mlinda lango wa Yanga Beno Kakolanya aliyegoma kuitumikia timu hiyo kutokana na ‘ukata’, nae anasubiri kumalizwa kwa mgogoro baina yake na uongozi wa timu hiyo
Kakolanya ameitaka Yanga ivunje mkataba wake na tayari ameliwasilisha suala hilo kwa TFF
Kakolanya anatarajiwa kujiunga na Simba akiwa mchezaji huru
Wakati huo huo Simba inaendelea kumjaribu kiungo mkabaji Jean Vital Ourega aliyetokea nchini Ivory Coast
Kiungo wa klabu ya Arsenal Granit Xhaka anatarajia kuukosa mchezo ujao wa Ligi Kuu Uingereza dhidi ya Newcastle Utd wikiendi hii kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Denmark siku ya Jumanne uliomalizika kwa sare ya mabao 3-3.
.
Xhaka alifunga bao moja katika mchezo huoCc: sokaonlineupdates
MSHAMBULIAJI wa timu ya Taifa yaya Brazil Gabriel Jesus, juzi, aliifungia timu yake mabao mawili ilipopata ushindi wa 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Czech.
Brazil walipata ushindi huo kwenye mchezo muhimu wa kirafi ki ambao Brazil walionyesha kiwango cha hali ya juu sana uwanjani.
Wakati Jesus akifunga mabao hayo staa mwingine wa timu hiyo anayeichezea klabu ya Liverpool, Roberto Firmino, alifanikiwa kuifungia timu yake bao lingine moja.
Czech walianza kwa kishindo mchezo huo baada ya kuanza kwa kuongoza kwa bao lililofungwa na David Pavelka katika dakika ya 37 ya mchezo huo.
Kiungo wa Liverpool, Roberto Firmino aliisawazishia timu yake mapema kipindi cha pili, kabla Jesus hajafunga mabao mawili kipindi cha pili cha mchezo huo.
Brazil wamerejea kwenye ushindi baada ya wikiendi iliyopita kupata sare ya bao 1-1 na Panama.
Mastaa wa Brazil, Firmino, Philippe Coutinho na kipa wa Liverpool, Alisson walionyesha kiwango cha juu sana kwenye mchezo huo.