SIMBA vs AS VITA

Viingilio vya mchezo wa mwisho wa hatua makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club ambao tutacheza siku ya Jumamosi Machi 16, 2019. #YesWeCan #NguvuMoja

Maeneo ambayo tiketi za mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club zinauzwa.

MO Salah aahidi kujitolea Muhanga UEFA ili kuisaidia Liverpool Kushinda Pl

Mo Salah aahidi kujitolea muhanga UEFA ili kuisadia Liverpool kushinda PL
Mshambuliaji wa klaberpool na taifa la Misri Mohamad Salah amefunguka kupitia Skysports na kueleza hisia zake na matamanio yake katika ligi kuu nchini Ungereza lakini pia kwenye ligi ymabingwa barani Ulaya UEFA.

Mohamed Salah amasema yuko tayari kujitolea sadaka yeye mwenyewe kwenye Ligi ya Mabingwa ili kusaidia Liverpool kushinda taji la kwanza akiwa na Liverpool la Ligi Kuu nchini humo.
Ingawa Salah anakiri Ligi ya Mabingwa ni “ushindani mkubwa na ni muhimu” kwa ajili yake, ila atakuwa na furaha kwa Liverpool ama watashinda Ligi Kuu badala yake.”

Salah alisema: “Ngoja nikwambie ukweli, ushindani mkubwa zaidi kwangu na nia yangu kubwa ni UCL (UEFA Champions League).

“Lakini ndoto ya mashabiki wote na kwa mji mzima na klabu nzima ni kutwaa taji la ligi.

“Kwa hiyo, ninafurahia kutoa dhabihu yangu kwa ndoto zao lakini kama tunashinda yote mawili ambao utaweza kufanya hivyo na hii ndiyo tunayojaribu kufanya.”

Mfalme wa Misri alisema anatumaini kuwa viongozi wa mji watajiunga na Liverpool, na yeye mwenyewe, tayari kujitenga.

during the Premier League match between Liverpool and Brighton and Hove Albion at Anfield on May 13, 2018 in Liverpool, England.
“Ushindani ni mgumu sana na tuna michezo migumu iliyobakia na kama ilivyo,” aliongeza Salah.

“Yote unaweza kufanya ni kushinda michezo yako na nina aini kwa hakika wao Man City watashindwa mchezo hata mmoja ili tuweze kushinda taji.

“Nia yangu ni mkali na kuna shida lakini nina nguvu ya akili na tunapaswa kuendelea.

“Tutaona nini tunaweza kufanya mwishoni mwa msimu lakini kiakili niko tayari kwa kila kitu.”

Kauli ya kwanza ya Zidane baada ya kutambulishwa Real Madrid

Club ya Real Madrid leo imemtangaza rasmi kocha wao wa zamani Zinedine Zinade Zizzou kuwa ndio kocha wao mpya kwa mara nyingine tena, hiyo ikiwa ni miezi 9 imepita toka kocha huyo aamua kujiuzulu baada ya ushindi wa tatu mfululizo wa UEFA Champions League.

Zidane baada ya kutangazwa rasmi na kutambulishwa kuwa amesaini mkataba wa miaka mitatu na kuchukua nafasi ya Santiago Solari, Zidane baada ya kujiuzulu nafasi yake ile alidaiwa kuwa ni kutaka kulinda heshima yake ya kuondoka katika club hiyo kwa heshima kwani angeendelea angeweza kuboronga ila mwenyewe ameweka wazi sababu za kurudi.

“Nimerudi kwa sababu Rais ameniita nina furaha kurudi lakini haya ni majukumu makubwa kwa sababu watu wengi wanaipenda hii club, tulishinda taji la Champions League msimu uliopita lakini tumelipoteza mapema na Kombe la Ligi pia mapema sana, najua nilikosea wapi msimu uliopita na naenda kufanya kadri ya uwezo wangu kuhakikisha hii timu inafanya vizuri”>>>Zidane

SIMBA SC : DUBAI – DAR

Msafara wa wachezaji, benchi la ufundi, baadhi ya viongozi wa klabu ukiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ambaye pia ni Mwenyekiti Kamati ya Mashindano, Ahmed Mgoyi umefika salama Dubai. Leo usiku watalala kwenye Hoteli ya Kimataifa ya Dubai na asubuhi wataendelea na safari ya kurejea nyumbani Tanzania. #NguvuMoja

Zidane Is Back 🔥🔥

Club ya Real Madrid ya Hispania leo imefikia maamuzi mazito ya kumrudisha tena aliyekuwa kocha wap Zinedine Zidane ambaye alijiuzulu kuendelea kuifundisha timu hiyo baada ya kudumu nayo kwa na kuipa mataji matatu mfululizo ya UEFA Champions League.

Zidane anarudi tena Real Madrid ambayo haina matumaini makubwa sana ya kutwa taji lolote kwa mkataba wa miaka mitatu, hiyo ikiwa ni miezi tisa toka atangaze kuondoka ndani ya club hiyo ya Real Madrid ambayo amepata nayo mafanikio akiwa mchezaji na kocha pia.

Santiago Solari

Real Madrid imemtangaza Zidane kuwa kocha wao wa tatu msimu huu baada ya kupoteza imani na Santiago Solari, mkataba huo sasa utamuweka Zidane ndani ya Real Madrid hadi 2022, tokeo 2015 Zidane akiwa na Real Madrid aliipa jumla ya mataji 9, matatu ya Champions League, Laliga 2016/2017, FIFA Club World Cup mara mbili na Super Copa Epana mara moja na UEFA Super Cup mara mbili

YANGA: Yapigwa FAINI 6 Million

🤗Klabu ya Yanga imetozwa faini ya jumla ya sh. 6,000,000 (milioni sita) kwa kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi kutoingia vyumbani na kusababisha wachezaji wakaguliwe kwenye korido, na pia kutotumia njia maalum iliyowekwa kwa ajili ya kuingia kwenye eneo la kuchezea (pitch) katika mechi hiyo iliyochezwa Februari 16, 2019 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Adhabu imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
.
.
Nini maoni yetu?

Alikufa Al Ahly uwanja Taifa, Vita ni nani

Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya JS Saoura Jumamosi iliyopita kwa kufungwa mabao 2-0, Jumamosi ijayo Simba inarejea kwenye uwanja wa Taifa kumaliza mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kwa kuikabili AS Vita Club

Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote kwenye mchezo huo ili iweze kutinga robo fainali ya michuano hiyo kwa mara ya pili katika historia yake

Simba iliwahi kutinga robo fainali ya michuano hiyo mwaka 1974

Kwenye msimamo wa kundi D JS Saoura inaongoza ikiwa imejikusanyia alama nane ikifuatiwa na Al Ahly yenye alama saba sawa na Vita Club ambayo inashika nafasi ya tatu

Simba inashika nafasi ya nne ikiwa na alama sita

Bila ya kujali matokeo kati ya Al Ahly dhidi ya JS Saoura, ushindi utaihakikishia Simba kufikisha alama tisa na kujihakikishia moja ya tiketi mbili za kutinga robo fainali

Habari njema kwa Simba ni kwamba itakuwa ikicheza mchezo huo mbele ya mashabiki wake ambapo mkakati uliopo ni kuhakikisha siti zote elfu 60 katika uwanja wa Taifa zinakaliwa

Simba imejijengea rekodi ya kipekee inapocheza uwanja wa Taifa.

Msimu huu imefanikiwa kushinda michezo yake yote iliyocheza kwenye dimba hilo katika michuano ya ligi ya mabingwa

Miongoni mwa timu ambazo zilichezea kichapo ni Al Ahly, mabingwa mara nane wa taji la ligi ya mabingwa na vigogo wa soka barani Afrika

Al Ahly iliifunga Simba mabao 5-0 katika mchezo wa duru ya kwanza lakini ilishindwa kufua dafu ilipokuja ‘kwa Mkapa’

Morali hiyo iliyotumika kwa Al Ahly ndio hiyo itakayotumika kuimaliza Vita Club ambayo pia ilishinda kwa mabao 5-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa DR Congo

Katika mchezo huo Simba haina cha kupoteza, kwani matokeo yoyote tofauti na ushindi yataiondosha mashindanoni.

Hivyo hakuna shaka vijana wa Aussems watacheza mpira wa kushambulia mwanzo mwisho

Kocha Patrick Aussems amewaalika mashabiki wote wa soka Tanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa Jumamosi ili kuweza kuandika Historia pamoja na Simba

NINJA : Afungiwa Mechi Tatu

Kamati ya Nidhamu ya TFF imemfungia mchezaji wa timu ya Yanga Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kutocheza mechi tatu mfululizo baada ya kamati hiyo kubaini kuwa mchezaji huyo ametenda kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa timu ya Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara uliochezwa mkoani Tanga

Suala la Ninja liliamuliwa juzi katika kikao cha Kamati hiyo kilichoketi jijini Dar es salaam

Ninja atakosa mchezo wake wa kwanza dhidi ya Lipuli Fc, March 16 2019

HAJI MANARA

Kuelekea mechi yetu ya jumamosi dhidi ya AS Vita leo saa sita na nusu mchana ntaongea na Wanahabari Kwenye makao makuu ya klabu yaliyopo msimbazi

Do or Die