
– Blackpool imefanya usajili wake wa kwanza Dirisha hili La Uhamisho kwa kumnasa Mshambuliaji waKimataifa wa Tanzania, Adi Yussuf. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amesaini mkataba wa miaka miwili na Kipengele cha kuongeza mwaka mwingine kuwa Mitatu; Hii imekuja baada ya mkataba wake na Klabu ya Solihull Moors kumalizika.
.
– Katika Kipindi chote cha Mwaka Mmoja na Nusu akiwa na klabu hiyo ya Daraja la tano, Alifunga mabao 21 katika mashindano yote ya Klabu hiyo.. Amejiunga na Blackpool inayoshiriki League One sawa na Daraja La tatu katika mfumo wa Mzima wa Ligi Nchini Uingereza.
.
– Akiongea Baada ya “kusinyaa” Amesema.
— “Hii ni ndoto ya kweli kwangu.” “Jitihada zangu na kufanya kazi kwa bidii, hatimae mafanikio yangu yameonekana, natoa shukrani kwa kila mtu aliyeniamini na kwa kila mmoja ndani ya Solihull, “Ninataka tena kuwa na uhusiano na kila mtu Kipindi nitakacho kaa hapa.”.
— “Nilipoweza kufanya kazi katika Solihull. Nina hakika niweza kufanya kazi katika Ligi hii” Aliongeza Yussuf.
.
– Yussuf alianza kusakata Soka katika Timu ya Pili ya Leicester City, na Mpaka anajiunga na Blackpool, katimiza jumla ya vilabu 14 tofauti katika vilabu vyote hivyo timu 5 alicheza kwa mkopo. Nyota huyo anatarajia kutua nchini Moja kwa Moja ataingia kambini katika timu ya taifa ya Tanzania kwa Maandalizi ya AFCON 2019..
#Updates #transfers
@Sokawaytz
credit: @sokawaytz




























