Matokeo Mechi za Leo Ligi Kuu Tanzania

Michezo sita ya ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa 14 imepigwa leo katika viwanja mbalimbali.

Alliance Fc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa pili mfululizo baada ya kuilaza Mtibwa Sugar bao 1-0.

Baada ya kuchezea vichapo vizito kwenye michezo miwili iliyopita, leo Ruvu Shooting imezinduka na kufanikiwa ‘kuipapasa’ Stand United mabao 2-1

Haya hapa matokeo ya michezo yote iliyopigwa leo;

Ligi hiyo itaendelea kesho Alhamisi kwa mechezo mmoja kupigwa kati ya Mbeya City dhidi ya JKT Tanzania.

Timu za Yanga, Simba na Azam Fc zinaendelea ‘kurundika’ viporo baada ya michezo yao kuahirishwa kutokana na kuwa na wachezaji wengi kwenye timu ya Taifa

CAF Awards 2018 Vipengere vyote

– Shirikisho la Soka Barani Afrika “CAF” limetoa vipengele vinavyowaniwa tuzo za mwaka huu Kwa Mashindano Mbalimbali yaliyofanyika “CAF Awards 2018”, Hivi ndivyo vipengele vilivyotajwa baada ya kukaliwa kwa kikao jijini Dakar nchini Senegal..
.
.
1. African Player of the Year (Mchezaji Bora Afrika wa Mwaka).
2. Women’s Player of the Year (Mchezaji Bora wa mwaka kwa Wanawake Afrika).
3. Youth Player of the Year (Mchezaji Bora Kijana wa Mwaka Afrika).
4. Men’s Coach of the Year (Kocha Bora wa mwaka Afrika wa Kiume).
5. Women’s Coach of the Year (Kocha Bora wa mwaka Afrika wa kike).
6. Men’s National Team of the Year (Timu Bora ya Taifa Kwa Wanaume ya mwaka).
7. Women’s National Team of the Year (Timu bora ya Taifa Kwa Wanawake ya mwaka).
8. Goal of the Year (Goli Bora la Mwaka).
9. Africa Finest XI (Kikosi Bora Afrika Cha Mwaka).
.
👉 Kipengele cha Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa kiume na wa Kike, kura zake zitapigwa na..
– Kamati ya Ufundi ya CAF na Waandishi wa Habari za Michezo.
– Wachezaji wakongwe wa Afrika (Legendary).
– Makocha wa Vilabu waliozifikisha timu Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho na Klabu Bingwa Afrika, Makocha wa timu za Taifa zote 54 member wa CAF na Manahodha wake.
.
👉 Kipengele Cha Tuzo ya Mchezaji bora kijana, Kocha Bora wa kiume wa Mwaka, Kocha Bora wa kike wa mwaka, timu ya taifa bora ya mwaka ya Kiume na ya Kike, kura zake zitapigwa na..
.
– Kamati ya Ufundi ya CAF na Waandishi wa Habari za Michezo.
– Wachezaji wakongwe wa Afrika (Legendary).
– Makocha Ambao wamevifikisha Vilabu hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na Klabu Bingwa Afrika.
– FIFPro itatolewa kulingana na uwezo wa mchezaji alioonesha kwa mwaka ndio ataingia kikosi Bora cha Afrika.
– Goli Bora la Mwaka litapigiwa kura, lenye kura nyingi ndio litatangazwa kuwa bora.
.
– Ili kuwa mshindi wa tuzo hizo ni kulingana na kiwango bora zaidi kuanzia Mwezi February 2018 Mpaka mwezi November 2018.
.
– Sherehe ya kutangaza washindi wa tuzo hizo kulingana na kura pamoja uteuzi Kwa mwaka huu 2018 zitafanyika Siku ya Jumanne ya January 08,2019 nchini Senegal ndani ya jiji la Dakar. – Instagram

Kikosi Cha SIMBA Klabu Bingwa Africa

Klabu ya @simbasctanzania imetuma majina ya Wachezaji 25 wa kunako shirikisho la mpira wa Miguu Afrika CAF kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika (Caf Champions League)
Majina hayo ni kama ifuatavyo

Makipa (2)
1-Aishi Manula
2-Deo Munishi Dida
Mabeki (9)
3-Shomary Kapombe
4-Mohammed Hussein
5-Asante Kwasi
6-Paschal Wawa
7-Erasto Nyoni
8-Juuko Murshid
9-Yusufu Mlipili
10-Paul Bukaba
11-Salim Mbonde

Viungo (10)
12-Jonas Mkude
13-James Kotei
14-Clatous Chama
15-Hassan Dilunga
16-Mohammed Ibrahim
17-Said Ndemla
18-Haruna Niyonzima
19-Mzamiru Yassin
20-Shiza Kichuya
21-Rashid Juma

Washambuliaji (4)
22-John Bocco
23-Meddie Kagere
24-Emmanuel Okwi
25-Adam Salamba

#sokaonlineUpdates

Nafasi ya MANJI kujazwa January 13 2019

Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la soka nchini (TFF) ambayo ilipewa jukumu na BMT ya kusimamia mchakato wa uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi katika klabu ya Yanga, imetangza rasmi kuanza kwa zoezi hilo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ally Mchungahela amesema zoezi la kutolewa fomu kwa wagombea wa nafasi hizo ikiwemo ya Mwenyekiti wa Yanga litaanza rasmi Alhamisi, Novemba 08, 2018

Aidha, Mchungahela ametangaza tarehe ya uchaguzi kuwa ni Januari 13 2019.

Wakati TFF ikitangaza hayo, hali si shwari upande wa klabu ya Yanga ambayo kupitia viongozi wa Matawi wa klabu hiyo, wametangaza kupinga uchaguzi wa timu hiyo kusimamiwa na TFF.

BMT iliipa Kamati ya uchaguzi ya TFF jukumu la kusimamia uchaguzi huo baada ya kubaini Kamati ya uchaguzi ya Yanga ina mapungufu.

Wanachama hao pia walipinga uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wakiutaka uongozi wa klabu hiyo kwanza uwahakikishie kama kweli Mwenyekiti wao Yusufu Manji amekataa kurejea katika nafasi yake.

Nafasi zinazotarajiwa kujazwa kwenye uchaguzi huo ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na nafasi nne za wajumbe wa Kamati ya Utendaj

NIYONZIMA: Atoswa Timu Ya Taifa RWANDA

Kiungo wa Simba Haruna Niyonzima hajajumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda kinachojiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON 2019 dhidi ya Afrika ya Kati.

Mchezo huo utapigwa nchini Rwanda Novemba 18.

Niyonzima amekuwa kwenye mgogoro na uongozi wa Simba uliopelekea afanye migomo ya mara kwa mara na hivyo kuondolewa kwenye kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Tanzania Bara.

Wakati Niyonzima akiondolewa kwenye kikosi hicho cha Rwanda, Meddie Kagere kinara wa mabao kwenye kikosi cha Simba ameitwa.

Idadi kubwa ya wachezaji wa Simba wameitwa kwenye timu za mataifa yao kwa ajili ya michuano ya AFCON.

Emmanuel Okwi na Juuko Murshidi wao wameitwa timu ya Taifa ya Uganda, wakati Cleotus Chama ‘CCC’ yeye ameitwa timu ya Taifa ya Zambia.

Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Shiza Kichuya na John Bocco wao wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayotarajiwa kusafiri leo kwenda kuweka kambi nchini Afrika Kusini.

Hawa Hapa VIONGOZI WAPYA SIMBA SC

Jana baada ya Mkutano Mkuu, wanachama wa klabu ya Simba waliingia kwenye zoezi la uchaguzi kuwapata Mwenyekiti na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.

Zoezi la uchaguzi lilikwenda mpaka usiku na matokeo yake kutangazwa usiku wa kuamkia leo.

Hawa hapa washindi wa nafasi mbalimbali;

MWENYEKITI
Swedi Khamisi Mkwabi

WAJUMBE BODI YA WAKURUGENZI
1. Asha Baraka
2. Hussein Mlinga
3. Dk Zawadi Kadunda
4. Seleman Said
5. Mwina Kaduguda

Nyota Wailili wa GorMahia Mikononi mwa Aussems

Uongozi wa Simba umeanza kuichokoza Gor Mahia ya Kenya baada ya kukabidhi majina mawili ya Philemon Otien na Ephrem Guikan kwa kocha Mbelgiji Patrick Aussems.
Aussems anataka kuimalisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji kutoka nje wakati wa dirisha dogo litakapofunguliwa Novemba 15.
Aussems amekabidhiwa majina ya nyota hao wawili wa Gor Mahia, Mkenya Otien (26) anayecheza nafasi ya kiungo mkabaji au mshambuliaji wakati Guikan anacheza katika nafasi ya ushambuliaji tangu alivyotua hapo msimu mmoja uliopita akitokea katika klabu ya AS Port Louis ya nchini Mauritius.
Guikan (24) raia wa Ivory Coast ailijiunga na Gor Mahia mwanzo wa msimu uliopita kwa maana hiyo mkataba wake umebaki mwaka mmoja na ameweza kuifungia timu yake mabao 17 msimu mzima katika mashindano yote.
Simba wanaingia katika vita ya kumuania Guikan dhidi ya timu mbili kubwa Afrika ambazo ni Free State Stars ya Afrika Kusini na Nkana Fc inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Zambia.
Wakala wa Guikan, George Bwana aliweka wazi kuwa amezungumza na uongozi wa Simba na kweli wameonesha nia ya kumtaka nyota wake huyo ambaye amebakisha mwaka mmoja wa kuitumia klabu ya Gor Mahia ambayo kesho Jumanne inacheza na Everton nchini Uingereza.
Bwana alisema aliwasiliana na kiongozi wa juu wa Simba ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi kuwa wanamuhitaji Guikan, lakini bado hawajafikia uamuzi ya mwisho ya kumchukua kwani bado wapo katika majadiliano.
“Kiongozi huyo wa Simba aliniambia wanamtaka mchezaji wangu Guikan, lakini anasubiri wa kufanya uamuzi wamalizana naye,” alisema.
“Kwangu sina shida nawasubiri Simba maana ni timu nzuri, lakini hapa mkononi nipo na ofa kutoka Nkana na Free State zinamtaka mchezaji wangu nimewambia wasubili kwanza nioni hili la Simba tutalimaliza vipi,” alisema Bwana.
Kocha wa Simba, Aussems awali aliweka wazi kwamba yupo na orodha ya wachezaji watano mpaka sita ambayo atawapatia kamati ya usajili ili waweze kumsajili nyota mmoja na kama wao watapenda kumuongeza mwingine mwenye uwezo halitakuwa na shida kwake.
“Nataka straika mwenye uwezo wa kufunga kama waliokuwa sasa au zaidi yao lakini awe na uwezo wa kutengeneza nafasi za kufunga kwa wenzake,” alisema Aussems.
Sifa hizo ambazo Aussems ameziweka hapo kwa straika ambaye anamuhitaji zinapatikana kwa Guikan na huenda Simba wakaingia miguu miwili kumalizana na straika huyo.