ESPERANCE DETUNIS: BINGWA MPYAA KLABU BINGWA AFRICA

Mabingwa wapya wa klabu bingwa barani afrika ni klabu ya @esperance_sportive_detunis :🛑Esperance wamefanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa kuwachabanga Al Ahly [3-1]: :
:
🔄Mchezo wa kwanza ulifanyika Misri kwa Al Ahly kushinda bao 3-1 mchezo ambao mwamuzi alillamikiwa sana kwa kufanya maamuzi ya kutatiza kwa kutoa penati ambazo zimelalamikiwa sana.

Huu ni ubingwa wa 3 katika 7 walizocheza:
🎯1994
🎯2011
🎯2018
❌1999❌2000, ❌2010, ❌2012

Manchester United vs Manchester City Jumapili hii

#ManchesterDerby – Kuelekea mchezo wa Derby ya Jiji la Manchester jumapili hii – tuangalie umuhimu wa Maroune Fellaini ‘Kipenzi cha Jose Mourinho’ katika timu ya United.
:
Fellaini ambaye alikuwa ameumia kwa wiki kadhaa kabla ya kurudi katika mchezo dhidi ya Juventus ambapo alichangia kwa kiasi kikubwa kuirudisha United Uingereza na ushindi vs Juventus.
:
Kocha wa Juventus Massimiliano Allegri alisema hawakuweza kupambana na Fellaini alipoongia – aliwazidi kwenye kucheza mipira ya juu na aliwaletea madhara yaliyoenda kusababisha mashambulizi mengi langoni mwao.
:
Mourinho amekuwa akimzungumzia Fellaini kwa kumuita ‘Plan B’ pindi mipango yake ya mwanzo inapogoma na amekuwa akiisaidia sana United pindi aingiapo dimbani.
:
Takwimu zinaonyesha United inafunga magoli kwa wastani Fellaini anapokuwepo dimbani kuliko ambapo anakuwa hayupo. :
Kuelekea mchezo vs City, United wanamhitaji sana Fellaini awe kwenye kiwango bora kwa maana kiuhalisia United hawawezi kupambana na City kwa kucheza mpira chini – wanahitaji mbinu mbadala na uwepo wa Fellaini kikosini utaongeza ubora wa mbinu ya tofauti ya kuweza kuiletea madhara defence ya City. :
Manchester Derby ya kwanza ya msimu itachezwa jumapili hii majira ya saa 1:30 usiku – itaonyeshwa live kupitia @dstvtanzania pekee

RATIBA ya KLABU BINGWA AFRICA

Droo ya ratiba ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu wa 2018/19 ilifanyika nchini Morocco Novemba 03, 2018 lakini haikuwa imetangazwa rasmi na Shirikisho la soka Barani Afrika CAF.

Ratiba hiyo imetangazwa rasmi leo ambapo Simba sasa itachuana na Mbabane Swallows, mabingwa wa ligi kuu ya Swaziland.

Taarifa za awali kuwa Simba ingechuana na timu ya Ngozi inayomilikiwa na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza hazikuwa sahihi na zilitokana na mkanganyiko wa ratiba hiyo

Mchezo wa kwanza utapigwa kwenye uwanja wa Taifa mwishoni mwa mwezi huu Novemba 27-28 huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kupigwa nchini Swaziland Disemba 04-05.

Mbabane Swallows sio timu ya kubeza. Timu hiyo ndiyo aliyotokea Asante Kwasi kabla ya kuja nchini na kiungo wa Yanga Papi Tshishimbi.

Misimu miwili iliyopita Swallows iliiondosha Azam Fc kwenye raundi ya pili ya michuano ya kombe la Shirikisho na yenyewe ikafanikiwa kutinga hatua ya makundi.

Aidha timu hiyo msimu uliopita ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa ikipangwa kundi moja na Etoile Du Sahel, Zesco United na 1st De Agosto

Ilimaliza nafasi ya mwisho ikiwa na alama nne katika kundi D ambalo timu ya 1st De Agosto ilifanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano hiyo inayofikia tamati leo kwa mchezo wa marudiano wa fainali kati ya Esperance dhidi ya Al Ahly ambayo ilishinda kwa mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita

Wawakilishi wengine wa Tanzania, kutoka upande wa Zanzibar, JKU wao wataanzia ugenini katika mchezo dhidi ya Al Hilal ya Sudan

Kama Simba itafuzu hatua ya awali, raundi ya kwanza ikachuana na mshindi kati ya UD Songo ya Msumbiji dhidi ya Nkana Fc ya Zambia

CHIRWA: Sina Kinyongo na ZAHERA

Baada ya kutua Azam Fc mshambuliaji wa zamani wa Yanga Obrey Chirwa amesema hana kinyongo na kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera aliyemuwekea ngumu kurejea Jangwani.

“Kocha alisema mimi simtaki Chirwa sababu ana tabia ya kugoma. Ni kweli mimi niko hivyo hivyo na siwezi kubadilika,” Chirwa aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kutambulishwa na Azam Fc.

“Mpira ni kazi yangu, kama silipwi stahiki zangu lazima nidai kwa njia yoyote. Na kama nikishindwa nitavunja mkataba”

“Sina tatizo na kocha wala klabu ya Yanga, ninamtakia kila la kheri aweze kuipa mafanikio Young Africans,” amesema

Katika hatua nyingine Chirwa ameeleza kushangazwa na wachezaji wengi hapa nchini kutokana na kushindwa kuwa na misimamo jambo ambalo linawafanya waendelee kuzipigania timu zao bila kulipwa chochote.

“Unajua wachezaji wengi hapa nchini wamekosa msimamo wa kulinda mikataba yao, niko tayari kuvunja mkataba wangu na kwenda mahala pengine ninapoona stahiki zangu hazilipwi kwasababu nina familia na inanitegemea” alisema.

OKWII: Nikiachana Na SOKA nitakua Wakala Wa Wachezaji

Mshambuliaji wa Simba na timu ya taifa ya Uganda Emanuel Okwi amesema akiachana na soka anataka kuwa wakala wa wachezaji ili kuwasaidia wanufaike na vipaji vyao wasipite katika matatizo ambayo yeye na wachezaji wengine wegi wa sasa wanapitia.
:
“Baada ya kuacha mpira malengo yangu ni kuwa agent wa wachezaji wa baadaye kwa sababu nataka wafaidike na wafurahie mpira.”
:
“Nitapambana kuhakikisha wanapita katika njia sahihi ili wasipate matatizo ambayo sisi tumepata”.

OKWI: Aibuka Mchezaji Bora mwezi OCTOBER

Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi ametangazwa na Kamati ya Tuzo ya TFF kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa mwezi wa 10.

Okwi ameshinda tuzo hiyo baada ya kuifungia Simba mabao saba katika mwezi huo.

Wakati huo huo Kamati ya Tuzo imemchagua Kocha wa Azam FC, Hans Pluijm kuwa Kocha Bora wa mwezi Oktoba akiwashinda Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems na Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhan Nsazwarimo

Stars Yazidi Kujifua AFRIKA KUSINI

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo Jumatano imefanya mazoezi asubuhi na jioni kwenye Uwanja wa Celtic Bloemfontein nchini Afrika Kusini kujiandaa na mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu Fainali za AFCON dhidi ya Lesotho utakaofanyika Maseru Novemba 18,2018.

Kikosi cha Stars kimetua jana nchini Afrika Kusini kuweka kambi hiyo maalum ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha timu hiyo inafuzu kwa fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika nchini Cameroon.

Stars inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi L ikiwa imejikusanyia alama tano baada ya kushuka dimbani mara nne.

Uganda inayoongoza kundi L, iko katika nafasi nzuri zaidi ya kufuzu ikiwa na alama 10 wakati Cape Verde iko nafasi ya tatu ikiwa na alama nne.

Lesotho inashika mkia katika msimamo wa kundi L ikiwa na alama mbili.

Tanzania, Lesotho na Cape Verde zinawania nafasi ya pili.

Kama Stars itapata ushindi dhidi ya Lesotho halafu Cape Verde ikafungwa na Uganda basi Stars itafuzu sambamba na Uganda.