(TFF) imetangaza Waamuzi watakaochezesha mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa Simba dhidi ya Sevilla

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza Waamuzi watakaochezesha mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa Simba dhidi ya Sevilla ya Hispania itakayochezwa Uwanja wa Taifa Mei 23,2019.

Muamuzi wa Katikati atakua Elly Sasii,Muamuzi msaidizi namba moja Mohammed Mkono kutoka Tanga,Muamuzi msaidizi namba mbili Soud Lila wa Dar es Salaam na Muamuzi wa akiba atakuwa Jonesia Rukyaa kutoka Kagera.

Sevilla inatarajiwa kuwasili nchini kesho Jumanne tayari kwa mchezo huo wakati kikosi cha Simba kitarejea jijini Dar es salaam keshokutwa kutoka Singida baada ya mchezo dhidi ya Singida United kesho

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeingia udhamini na Kampuni ya GF Truck and Equipment

KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, imeingia udhamini na Kampuni ya GF Truck and Equipment kwa ajili ya mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) dhidi ya Lipuli Juni Mosi mwaka huu.

Mchezo huo umepangwa kufanyika Uwanja wa Ilulu, Lindi.

Zoezi la kuingia mkataba baina ya pande hizo mbili limefanyika kwenye ofisi za GF Truck, iliyowakilishwa na Mkurugenzi wake, Imran Karmali, huku Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, akiiwakilisha timu hiyo.

GF Truck ni moja ya kampuni bora, inayojihusisha na uzaaji wa magari ya FAW na mitambo ya ujenzi na uchimbaji ya XCMG, ikiwa imewekeza vilivyo kwenye sekta ya michezo.

A

zam FC imejipanga vilivyo kuelekea mchezo huo wa fainali, ikiwa imejiwekea malengo ya kutwaa taji na kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

MABAO YA MEDDIE KAGERE

Wakati akisajiliwa na Simba mwaka jana, wapo waliobeza usajili wa Meddie Kagere wakidai Simba haitanufaika na usajili wake kwa kuwa umri tayari umemtupa mkono

Hata hvyo mpaka sasa msimu unapoelekea ukingoni, hakuna hata mmoja atajitokeza kumbeza Kagere kutokana na alichokifanya katika klabu ya Simba ndani ya mwaka mmoja

Kagere ndiye kinara wa mabao kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara, jana akiitungua Ndanda Fc mabao mawili yaliyomfanya afikishe mabao 22

Kwa michezo iliyobaki, ni dhahiri Kagere ataibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwani mabao yake 22 yanamfanya aongoze kwa tofauti ya mabao sita dhidi ya wanaomfuatia, Salim Aiyee na Heritier Makambo ambaye tayari ameondoka Yanga

Kagere ameichezea Simba michezo 50 katika mashindano yote

Amefunga mabao 33 na kutoa pasi nne za mabao

Ana wastani wa kufunga zaidi ya bao moja kila mchezo

Kagere alitoa mchango mkubwa kwa kikosi cha Simba kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu, akifunga mabao sita

Kwa kushirikiana na washambuliaji wengine, John Bocco na Emmanuel Okwi, wameifanya Simba iwe moto wa kuotea mbali katika kuzifumania nyavu kwenye ligi

Watatu hao pekee wamefunga mabao 52 kati ya mabao 74 yaliyofungwa na Simba

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMATATU

Streka wa PSG na Ufaransa Kylian Mbappe, 20, amebainisha kuwa anaweza kuihama klabu yake katika kipindi hiki cha usajili. Kauli hiyo inatarajiwa kuziamsha klabu kongwe na tajiri kama Real Madrid, Barcelona na Manchester City kumgombea. (Express)

Kiungo raia wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 28, anataka kurudi mezani na klabu yake ya Manchester City kwa malengo ya kusalia klabuni hapo zaidi ya mwezi Juni 2020 ambapo mkataba wake wa sasa unaishia. (Mail)
Kocha Pep Guardiola atapewa fursa ya kusalia klabuni Manchester City walau kwa miaka mitano ijayo huku kipato chake kikifikia pauni milioni 100, baada ya mshahara wake kwa mwaka kuchupa toka pauni milioni 15 mpaka milioni 20. (Sun)

Kiungo wa kimataifa wa Ubelgiji Yannick Carrasco, 25, ambaye anakipiga kwenye ligi kuu ya Uchina, klabu ya Dalian Yifang, anataka kuhamia katika ligi ya Primia na Arsenal wanatarajiwa kumnyemelea, klabu hiyo ilikaribia kumsajili katika dirisha dogo la usajili la Januari. (Sun)

Arsenal pia wanamnyemelea beki wa kati na kinda wa timu ya Saint-Etienne na timu ya taifa ya chini ya miaka 19 ya Ufaransa, William Saliba, 18. (Goal.com)

SanchezHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption Sanchez amekuwa na wakati mgumu na United tofauti na alipokuwa Arsenal
Mshambuliaji aliyepoteza kiwango wa Manchester United na Chile Alexis Sanchez, 30, anatarajiwa kukatiza mapumziko yake ya mwisho wa msimu na kurudi klabuni ili kujifua na kujihakikishia nafasi katika kikosi cha United. (Sun)
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amemwonesha dalili za wazi winga raia wa Wales Gareth Bale, 29, kuwa muda wake katika klabu hiyo umefikia tamati, baada ya kusema kuwa asingemuingiza mchezoni kutoka benchi walipofungwa Jumapili na Real Betis hata kama kungekuwa na fursa ya kuingiza wachezaji wanne. (Eurosport)
BaleHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption Bale ‘agoma’ kuhama Real Madrid mpaka mkataba wake utakapoisha
Bale hata hivyo amewaambia wachezaji wenzake kuwa anapanga kusalia klabuni hapo mpaka kwisha kwa mkataba wake na takuwa mwenye furaha kucheza gofu endapo hatapangwa kucheza. (Radioestadio, via Mail)

Kiungo wa Chelsea na Ufaransa N’Golo Kante, 28, anapiga hessabu za kuikacha klabu yake na kujiunga na miamba ya Ligi ya Ufaransa PSG. (Talksport)
KanteHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Manchester United watarasimisha nia yao ya kumsajili kiungo wa Lyon, Tanguy Ndombele, 22, pale tu mustakabali wa kiungo wao Paul Pogba, 26, utakapokuwa wazi. (Manchester Evening News)

Kocha wa Lille, Christophe Galtier amethibitisha kuwa winga raia wa Ivory Coast winger Nicolas Pepe, 23, ataihama klabu hiyo hivi karibuni. Mcezaji huyo anahusishwa na uhamisho na klabu kongwe za Manchester United, Arsenal na Bayern Munich. (Manchester Evening News)

TETESI ZA USAJILI YANGA LEO JUMATATU

KUNA kila dalii kwamba, endapo straika Heritier Makambo wa Yanga atakamilisha dili lake la kujiunga na klabu ya Horoya FC ya nchini Guinea, basi mkali mwingine raia wa Ghana ataziba nafasi yake.
Anayetajwa kuziba nafasi hiyo ni Mnamibia anayekipiga katika klabu ya Lusaka Dynamos ya Zambia, Petrus Shitembi, anayetajwa kuwa hatari katika nafasi ya kiungo mshambuliaji.

Kiungo huyo alisajiliwa na Lusaka Dynamos siku chake baada ya Clatous Chama kusajiliwa na Simba ili kuziba pengo lake kutokana na uwezo mkubwa alionao.

Simba walimsajili Chama kutoka klabu hiyo na kwa haraka nao hawakulaza damu, wakamchukua Shitembi ambaye naye ameingia kwenye rada za Yanga.

Kigogo mmoja wa Yanga amefunguka kuwa kiungo huyo ambaye ana uwezo mkubwa wa kutoa pasi za uhakika na kufunga mabao muhimu, ameshaingia kwenye 18 zao na kilichobakia ni kumalizana tu.
“Ni kweli Makambo ameondoka lakini hiyo haimaanishi kwamba Yanga inakufa. Tumeshaanza harakati za usajili na muda si mrefu tutamalizana na kiungo kutoka Namibia.
“Ni moja ya viungo wazuri na yeye hana tabu yoyote kuja Yanga. Nadhani ataungana na wachezaji wengine ambao tutawasajili kwani dhamira yetu ni kuisuka klabu yetu upya ili msimu unaokuja tuwakate kilimilimi wapinzani wetu,” alisema.
Alisema kiungo huyo ni moja ya wachezaji wanane wa kigeni ambao kocha wao mkuu, Mwinyi Zahera, alidai atawasajili, huku akisema kuna mastraika wengine watatu kutoka nchi tofauti.

“Wapo pia mastraika watatu tunaendelea na mazungumzo nao, hiyo kazi inafanywa na kocha wetu, nadhani baada ya kuondoka Makambo, tutashusha mashine nyingine hatari zaidi,” alisema.
Kiungo huyo alianza soka katika timu ya Rundu Chiefs ya nchini kwao Namibia kabla ya kwenda Afrika Kusini ambako alijiunga na University Of Pretoria na baadaye kwenda Ghana kuichezea Ashanti Gold kabla ya kurudi tena na kuzichezea Amazulu FC na Stellenbosch FC na baada ya kuondoka Chama akasajiliwa Lusaka Dynamos kuziba pengo lake.

Mchakato wa Usajili wa Mkambo Uko Mikono Salama -MWAKALEBELA

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema mchakato wa usajili wa mshambuliaji Heritier Makambo uko katika mikono salama

Aidha Mwakalebelea amesema Yanga imepokea ofa nyingi zinazomuhusu mshambuliaji huyo

Amesisitiza bado hakuna mkataba uliosainiwa upande wa Yanga, hivyo amewahakikishia Wanayanga kuwa Makambo bado ni mchezaji wao halali

“Suala la Makambo liko mikono salama, uongozi tunalifahamu na tulitoa baraka zetu kwake pamoja na Mwalimu kwenda Guinea ambako alitakiwa kwenda kufanyiwa vipimo vya afya,” amesema

“Ilikuwa ni lazima aende na Mwalimu kwa sababu kule wanaongea kifaransa”

“Lakini ifahamike Makambo ana ofa nyingi, sio Horoya Fc pekee wanaotaka kumsajili, Jumatatu tutakutana na wengine”

“Tunazipitia ofa zote na kufanya tathmini kabla ya kuamua. Hakuna mkataba ambao umeshasainiwa kwa upende wetu. Na kwa kawaida mkataba lazima uwe wa pande mbili”

“Mpira ni biashara, kama kutakuwa na ofa nzuri tutafanya biashara lakini kama itakuwa tofauti basi tutaendelea kubaki na mchezaji wetu”