TETESI ZA USAJILI SIMBA LEO JUMANNE

Tetesi za usajili Simba leo 21 May 2019

Kikosi cha Simba leo huenda kikatangaza ubingwa kikicheza kwenye ardhi ya Singida katika uwanja wa Namfua, Simba inahitaji walau sare tu ili kuweza kutangaza Ubingwa mbele ya Singida United wanaohitaji ushindi ili kujihakikishia kuendelea kusalia ligi kuu.

Ukiachana na hayo ya Simba kushinda inaelezwa kuwa kikosi cha Simba kinaendelea kutafuta wachezaji wakuimarisha kikosi chao kwaajili ya msimu ujao.

Kama ulijisahaulisha, mchezaji Vitalis Mayanga wa Ndanda inaelezwa kuwa ni suala la muda tu kutua Simba kwani Simba na Ndanda walishamalizana muda tu na kijana anasubiri ligi iishe waweze kumjumuisha kikosini.

Vitalis Mayanga licha ya kuwa akitajwa kuwaniwa na baadhi ya vilabu nchini Tanzania Yanga ikitajwa lakini imebainika ni mchezaji halali wa Simba anayesubiria ligi iishe aungane na mabingwa hao wa soka nchini.
Credit: Kwataunit

MATOKEO YA MECHI ZA JANA JUMATATU.

MATOKEO YA MECHI ZA JANA JUMATATU.
Serie A
FT 3 Lazio
3 Bologna
Ligi Kuu Bara.
FT 2 Biashara United
1 Ruvu Shooting
:
RATIBA YA MECHI ZA LEO:
– Ligi kuu Bara
16:00 Mbao FC
KMC FC
16:00 Singida United
Simba SC
.
– Egypt Premier League
23:00 Al Masry
El Entag El Harby
23:00 El Geish
Al Ittihad
23:00 ENPPI
Misr Lel Makasa
23:00 Smouha
Petrojet
23:00 Wadi Degla
Haras El Hodood
.
– International – Club Friendlies.
19:30 Beitar Jerusalem
Atletico Madrid
#Updates #sokawaytz

NOEL MWANDILA OUT YANGA

NOEL MWANDILA OUT YANGA -Mwenyikiti wa klabu ya Yanga, Dr Mbette Mshindo Msolla amethibitisha kuwa wataachana na kocha msaidizi wa klabu hiyo Noel Mwandila na kuajiri kocha msaidizi mzawa ili aweze kumsaidia kocha Mwinyi Zahera. -Akiongea kuhusu kuibadili Yanga amedai wafanyakazi wote wa Yanga na watu wa bechi la ufundi isipokuwa kocha mkuu Mwinyi Zahera wanatakiwa kutuma CV zao upya kwa uongozi mpya ili kufanyiwa kazi na kila mtu afanye kazi anayostahili. -Kuhusu kocha Msaidizi Mwenyekiti alisema “Benchi la ufundi linahitaji kuwa na kocha msaidizi mwenye kiwango kizuri ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi chetu, tutaangalia zaidi kocha mzawa ili aweze kuwa sambamba na kocha Zahera kufanya kazi.” “Katika nchi za wenzetu zilizoendelea kocha mkuu amekuwa akimtumia zaidi kocha msaidizi kwa kumtuma kwa ajili ya kwenda kufuatilia wachezaji wanaowahitaji kwa ajili ya kuwasajili hata ikiwa nje ya nchi ambaye anafuatilia mechi na mazoezi anayofanya mchezaji, hivyo tunahitaji msaidizi mwenye weredi atakayeshirikiana vyema na kocha mambo mbalimbali” “Tukiachana na kazi ya kutafuta kocha, pia tutawatumia wachezaji wa zamani waliowahi kuichezea Yanga kuweza kuwatuma mikoani kwa ajili ya kusaka vipaji,”
Alisema Dr. Mshindo Msolla -Noel Mwandila alijunga na klabu ya Yanga misimu miwili iliyopita kama kocha wa viungo chini ya kocha George Lwandamina ila baada ya kuondoka kwa Lwandamina na Shadrack Nsajingwa ndio akawa kocha msaidizi wa klabu ya Yanga.
.
Cc : Yossima Sitta Jr

TANZIA: – Kocha mkuu wa Mabingwa wa Nigeria, Klabu ya Lobi Stars FC 🇳🇬, Solomon Ogbeide amefariki Dunia jioni ya leo

TANZIA: – Kocha mkuu wa Mabingwa wa Nigeria, Klabu ya Lobi Stars FC 🇳🇬, Solomon Ogbeide amefariki Dunia jioni ya leo, Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Nigeria ni kwamba Ogbeide amefariki dunia kufuatia kuumwa kwa muda mfupi.
:
– Klabu ya Lobi Stars muda huu ipo Dimbani kucheza Mchezo wa Ligi dhidi ya Wikki Tourists , Baada Mchezo Klabu inatarajia kuthibitisha kifo cha kocha wao.
:
– Kocha huyo ametoka kuiongoza Klabu hiyo katika Michuano ya Klabu Bingwa Afrika ambapo wameishia hatua ya Makundi wakishika nafasi ya tatu na pointi zao Saba katika kundi A (W2,D1,L3).
RIP Ogbeide 💔
#Updates #nfpl
@Sokawaytz

Mwinyi Zahera amesema lengo la kwanza la kikosi chake msimu ujao ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema lengo la kwanza la kikosi chake msimu ujao ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu

Yanga imeshindwa katika mbio za kuwania ubingwa msimu huu na wapinzani wao Simba ambao wanahitaji alama moja tu kutoka michezo mitatu

Hata hivyo licha ya kumaliza katika nafasi ya pili, Zahera amesema timu yake imefanikiwa kulingana na mazingirwa waliyokuwa nayo

“Tulianza kwa kuwa na malengo ya kumaliza nafasi ya sita au saba, lakini baada ya kuona tunafanya vizuri licha ya kuwa na changamoto nyingi, tukasema tujaribu kuwania ubingwa,” amesema Zahera

“Bado naamini tulistahili kushinda kombe kama sio kudhurumiwa baadhi ya michezo”

“Sasa nafurahi timu imepata viongozi, nimewaambia wajipange. Hatutaki tena haya ya mwaka huu yatukute msimu ujao”

“Tunahitaji kuwa na timu imara itakayoshinda na kutwaa ubingwa mapema”

Zahera amesema huu ukiwa msimu wake wa kwanza Tanzania, umemsaidia kufahamu ushindani wa ligi, aina ya wachezaji anaowahitaji na mbinu gani atumie ili kuweza kufanya vizuri

“Tutatengeneza timu imara, tutasajili wachezaji wa kiwango cha juu ambao watafanya timu yetu iwe kali sana msimu ujao”

KENNY ALLY: Huru Kutua Jangwani #YANGA

Kiungo wa Singida United Kenny Ally ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwaniwa na Yanga kwa ajili ya msimu ujao

Kenny anaweza kutua Yanga akiwa mchezaji huru kwani mkataba wake na Singida United unamalizika mwishoni mwa msimu huu

Uongozi wa Singida United umesema hauna pingamizi kwa kiungo huyo kama atapenda kujiunga na Yanga kwa kuwa maamuzi ni yake, mkataba wake uko ukingoni

“Kenny atakuwa huru kujiunga na timu yeyote baada ya ligi kumalizika, hivyo kama Yanga wanamuhitaji wazungumze nae,” amesema Cales Katemana ambaye ni msemaji wa Singida United

Yanga imedhamiria kuunda kikosi cha ushindani kwa ajili ya msimu ujao

Tayari michakato ya usajili imeanza kimyakimya

CHIRWA: Aiwekea Ngumu Azam Arudi au Asirudi?

Mshambuliaji wa Azam Fc Obrey Chirwa amegoma kusaini mkataba mpya kunako klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu

Azam Fc imekuja na utaratibu tofauti wa kuwaongezea mikataba wachezaji wake kabla ya mikataba yao ya awali kumalizika

Timu hiyo tayari imewapa mikataba wachezaji wake waandamizi isipokuwa Chirwa aliyejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miezi sita wakati wa dirisha dogo la usajili

Hivi karibuni kocha Mwinyi Zahera alieleza kuvutiwa na kiwango cha mshambuliaji huyo raia wa Zambia

Zahera alisema Chirwa ni bonge la mchezaji, lakini alikataa kuweka wazi kama anaweza kumrejesha tena kikosini kwa ajili ya msimu ujao

Alitaja hali ngumu ya kiuchumi Yanga ilikuwa sababu ya yeye kukataa asisajiliwe aliporejea kutoka Misri mwishoni mwa mwaka jana

“Chirwa ni mchezaji mkubwa na anapambana sana katika uchezaji wake hata kwa mechi nilizomuona ana kitu ambacho wengine hawana, ila nilimkataa kwa kuwa hawezi kuvumilia matatizo,” alisema