Kikosi cha Tanzania vs Lesotho Leo

Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inahitaji ushindi leo dhidi ya Lesotho ili iweze kufuzu kwa fainali za michuano ya AFCON 2019

Hiki hapa kikosi cha Stars kinachoshuka dimbani saa 11 jioni leo Jumapili, Novemba 18 2018.

1. Aishi Manula
2. Abdallah Kheri
3. Ali Sonso
4. Kelvin Yondani
5. Aggrey Morris
6. Erasto Nyoni
7. Himid Mao
8. Mudathir Yahya
9. Shabani Iddi
10. Saimon Msuva
11. Gadiel Michael

MO: Aitakia kheri Taifa Stars

Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji ‘MO’ ameungana na Watanzania wote kuitakia kila la kheri timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ili iweze kuibuka na ushindi huko Lesotho.

Ushindi utaiwezesha Stars kukata tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika mwakani mwezi wa sita nchini Cameroon.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, MO amesema anaamini ushindi utarudisha furaha ya Watanzania baada ya kukosa kushiriki fainali za AFCON kwa zaidi ya miaka 38.

“Nawatakiwa kila la kheri Taifa Stars katika mchezo wa leo dhidi ya Lesotho. Ushindi wa leo utarudisha furaha ya Watanzania ya kukosa kushiriki AFCON kwa miaka 38. Tunaamini mtafanya vizuri sababu nia tunayo na uwezo tunao. Mungu awe nanyi,” ameandika MO

MOURINHO: Kuwapiga Bei Mabeki Hawa

#TetesiZaUsajili Baada ya taarifa za awali kudai kuwa kocha wa Manchester United Jose Mourinho yupo tayari kuwapiga bei beki wake Marcos Rojo pamoja na Eric Baily ili kusajili beki mwingine, klabu ya PSG inataka kutumia nafasi hiyo ili kumnasa Eric Baily kipindi cha usajili wa dirisha dogo mwezi January (The Mail)

C&p #sokaonlineUpdates

KESSY : Tunawaheshimu Wapinzani Na Tunatafta USHINDI

Mlinzi wa pembeni wa Taifa Stars na Nkana FC ya Zambia Hassan Kessy amesema kwenye mchezo wa leo dhidi ya Lesotho wachezaji wa Tanzania wanaingia na mambo mawili katika mchezo huo, kuwaheshimu wapinzani na kutafuta ushindi .
.
“Jambo la kwanza tutawaheshimu wapinzani kwa sababu wapo nyumbani, la pili sisi tunataka kuweka historia yetu, wenzetu waliweka yao lakini sisi tunataka kuweka ya kwetu.”
:
“Watanzania waendelee kutuombea tuweze kufanya vizuri.”
.
Mechi itakuwa LIVE @dstvtanzania #SS7 kuanzia saa 11:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki
🇹🇿🇹🇿#TwenzetuCameroon

STARS: inahitaji Ushindi vs Losotho

Ushindi wa Uganda leo umeirahisishia zaidi Taifa Stars nafasi ya Kufuzu Afcon Mwaka huu endapo tutaibuka na ushindi kesho dhidi ya Lesotho basi moja kwa moja tutakuwa tumefuzu
.
.
Mwisho tutarudi kucheza mchezo wa mwisho na Uganda ambao tayari nao wamefuzu leo

Credit@
#sokaonlineUpdates

STARS: Safari ya Cameroon Iko mikononi Mwetu

Wakati Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania (Taifa Stars), Mnigeria Emmanuel Amunike, akisema haikuwa rahisi kuwafunga Cape Verde na kurejesha matumaini ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Cameroon mwakani, hesabu za Tanzania kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1980 ziko mikononi mwetu.

Baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Cape Verde mwezi uliyopita, uliifanya Stars ifikishe alama tano na ushindi kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Lesotho utaipeleka Stars Cameroon baada ya Uganda kuichapa Cape Verde bao 1-0 leo.

Uganda imefikisha alama 13 baada ya ushindi wa leo na kama Stars itashinda kesho itafikisha alama nane.

Alama hizo haziwezi kufikiwa na Cape Verde wala Lesotho hata zikishinda mchezo mmoja utakaokuwa umebaki.

Stars iliweka kambi nchini Afrika Kusini kwa takribani wiki nzima ikijiandaa na mchezo huo utakaopigwa kesho Jumapili Novemba 18 huko Lesotho.

Tayari iko Lesotho ambapo leo jioni itajifua kwenye uwanja utakaopigwa mchezo huo kesho.

Amunike amesema wanakwenda Lesotho wakiwa na lengo moja tu la kuhakikisha wanaibuka na ushindi ambao utawahakikishia tiketi ya kufuzu AFCON 2019

Uganda 1-0 Cape Verde : Stars inahitaji UShindi ili kufuzu

Uganda Cranes imekuwa timu ya kwanza kundi L kufuzu kwa fainali za michuano ya AFCON 2019 baada ya kuichapa Cape Verde bao 1-0 katika mchezo wa raundi ya tano uliopigwa leo nchini Uganda.

Bao pekee la Uganda lifungwa na Patrick Henry kwenye dakika ya 78.

Uganda ilikuwa inahitaji alama moja tu kujihakikishia kufuzu.

Ushindi huo umeifanya timu hiyo ifikishe alama 13 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kutoka kundi L.

Matokeo hayo pia yameipa nafasi timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kuweza kufuzu kesho kama itaifunga Lesotho katika mchezo utakaopigwa Maseru.

Ushindi utaiwezesha Stars kuwa na alama nane ambazo hazitaweza kufikiwa na Cape Verde yenye alama nne wala Lesotho yenye alama mbili.