Wakati dirisha la usajili Tanzania Bara likitarajiwa kufunguliwa Novemba 15, mwaka huu, imebainika kwamba wachezaji mbalimbali wa kimataifa kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wameomba kusajiliwa katika klabu hiyo inayonolewa na Mbelgiji Patrick Aussems.
Wachezaji hao wameomba kusajiliwa Simba kutokana na klabu hiyo kwa sasa kumwaga fedha za usajili kutokana na uwepo wa mwekezaji wake, Mohammed Dewji.
Akizungumza jana kwenye mkutano mkuu wa klabu hiyo, Kaimu Rais aliyemaliza muda wake, Salim Abdallah ‘Try Again’ amesema kwamba wamepokea meseji mbalimbali kutoka kwa wachezaji wa kimataifa wakiomba kusajiliwa katika klabu hiyo.
“Kuna wachezaji mbalimbali ambao wameomba kusajiliwa katika klabu yetu katika kipindi hiki. Nimekuwa nikipokea meseji za wachezaji kutoka sehemu mbalimbali za Afrika wakiomba nafasi ya kusajiliwa ndani ya timu yetu,” alisema Try Again.
Licha ya wachezaji hao kuomba kusajiliwa na Simba klabu hiyo kwa sasa ina wachezaji nane wa kimataifa. Wachezaji hao ni Emmanuel Okwi (Uganda), Claytous Chama (Zambia), Pascal Wawa (Ivory Coast), Meddie Kagere (Rwanda), Nicholaus Gyan (Ghana), Asante Kwasi (Ghana), Juuko Murshid (Uganda) na James Kotei (Ghana).
Wakati huohuo jana Simba walitangaza kutenga kiasi cha milioni 750 kwa ajili ya kufanya usajili kwa ajili ya kukiimarisha kikosi hicho.
Katika hatua nyingine, Try Again amesema kwamba klabu hiyo tayari imekamilika na wanajua watasajili wachezaji gani kwenye dirisha la usajili ambapo usajili huo utasimamiwa na mwekezaji, Mohammed Dewji ‘Mo’.
Pia klabu hiyo imesajili wachezaji 17 kwenye kikosi cha vijana cha klabu hiyo U20 pamoja na kusajili wachezaji 10 wanaocheza kwenye timu ya taifa ya wanawake kwa ajili ya Simba Queens.
Category: usajili
SIMBA: Kumtoa kwa mkopo Marcel
Kocha wa klabu ya Simba Sc Patrick Aussems amesema tayari ametoa mapendekezo ya kumtoa kwa mkopo mchezaji wao Marcel Kaheza kwenda klabu atakayopata nafasi ya kucheza kwa kipindi cha miezi 6 tuu.
Kocha huyo amefika mbali zaidi na kusema hawezi akaruhusu nyota huyo wa zamani wa MajiMaji Fc kuuzwa kwa kuwa ana uwezo wa hali ya juu, kutokana na upana wa kikosi cha Simba Sc ndio maana hapati nafasi ya kucheza na kuonyesha ubora wake #sokaonlineUpdates
YANGA: Kumsajili Kiungo Huyu
Dirisha dogo la usajili linafunguliwa Novemba 15, ni wazi kwamba kila timu sasa inahaha kuhakikisha inaziba mapengo ambayo yamejitokeza katika Ligi Kuu inayoendelea.
Yanga nayo haichezi mbali, inasaka wakali ambao wanaweza kuwapaisha na kutikisa katika ligi ikiwa ni pamoja na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa.
Yanga waliibuka na straika Heritier Makambo katika dirisha la usajili lililopita, lakini wamegundua kwamba mchezaji huyo hajafikia kiwango thabiti walichokuwa wakikihitaji na sasa wameamua kumtafuta winga wa kumlisha raia huyo wa DR Congo.
Wanajangwani hao wamefanikiwa kumshawishi winga Ruben Bomba raia wa DR Congo, ambaye tayari ameshakubali kutua katika klabu hiyo.
Juzi kati Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera aliweka wazi kwamba anataka kuletewa winga mmoja matata atakayekuwa na kazi ya kuwalisha washambuliaji, ni wazi karibia azma yake itatimia.
Pia juzi Jumapili mara baada ya mechi dhidi ya Ndanda ambayo walitoka sare ya 1-1, kocha Zahera alisema kuwa kupungua makali kwa Makambo kunatokana na kutolishwa mipira ipasavyo huku wachezaji wa wake wa pembeni wakishindwa kuwa na muendelezo mzuri wa viwango vyao.
Zahera alisema nyota wake wawili Deus Kaseke na mkongwe Mrisho Ngassa bado hawajaweza kufanya anachokitaka na kuwa ndiyo maana ametaka kusajiliwa kwa mtu muafaka angalau mmoja kutoka katika eneo hilo.
“Kaseke hayuko kwenye kiwango cha juu sana kwasasa lakini Makambo naye amekuwa akikosa mabao kirahisi huku wakati mwingine hapewi mipira sahihi,”alisema Zahera.
“Ndiyo maana nataka mtu wa kuongeza nguvu tunayoitaka katika safu yetu ya ushambuliaji, ngoja tuone kipi tutafanya muda wa kusajili ukifika.”
Bomba, ndiye chaguo la kwanza la Zahera na tayari mabosi wa usajili chini ya Mwenyekiti Hussein Nyika walishaanza kazi ya kuhakikisha anatua nchini.
Taarifa kutoka ndani ya kamati inasema kwamba Bomba ameshakubali kutua Yanga ambapo raia huyo wa DR Congo anataka kuungana na Zahera ambaye pia ni Kocha Msaidizi wa timu ya taifa ya DR Congo.
“Tumeshafanya naye mazungumzo kilichokuwa kinahitajika ni utulivu ndani ya klabu yetu,”alisema bosi huyo.
“Huyu Bomba (Ruben) ni winga mzuri, tumeona kasi yake uwanjani. Akifika hapa mashabiki watakubali ninayosema.”
YANGA: Kusajili Jembe Hili
Yanga imekuwa kwenye mazungumzo na beki kisiki wa Rayon Sports, ambaye ni nahodha wa timu hiyo, Abdul Rwatubyaye
Wakala wa mchezaji huyo alikiri kuwa na mazungumzo na uongozi wa Yanga lakini pia akisema klabu ya Simba nayo imeulizia upatikanaji wa beki huyo mwenye umri wa miaka 23
Kulingana na taarifa zinazoripotiwa na vyombo vya habari nchini Rwanda, Rayon Sport iko tayari kumuachia Abdul kwa kitita cha Mil 80
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika amekuwa kwenye mazungumzo na wakala wa mchezaji huku ikielezwa tayari pande zote zimefikia makubaliano juu ya usajili wa beki huyo.
Inaelezwa uko uwezekano mkubwa kwa beki huyo kutua Yanga mapema tu dirisha la usajili litakapofunguliwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo
Yanga pia imemalizana na mshambuliaji wake wa zamani Obrey Chirwa ambaye awali aliwekewa ngumu na kocha wa timu hiyo Miwnyi Zahera
DELE ALLI:Aongeza Mkataba Tottenham
– Kiungo wa timu ya Taifa ya England, Dele Alli amesaini mkataba mpya wa miaka Sita (6) Kuendelea kuichezea Klabu yake ya Tottenham Mpaka mwaka 2024..
.
– Dele Alli Alijiunga na Spurs mwaka 2015 akitokea MK Dons, na tokea hapo akawa ni Mmoja wa Wachezaji bora Barani Ulaya chini ya kocha wake Mauricio Pochettino.
.
– Tokea ajiunge na Klabu hiyo ya London amefanikiwa kufunga Magoli 48 na Assist 41 Katika mechi 153 akiwatumikia farasi weupe.
.
– Tottenham wanawaongeza Mikataba mipya Wachezaji wao Wote Ambao ni tegemeo, kabla ya Alli walitoka kumpa Mkataba mpya Mshambuliaji wao Hary Kane ambaye alisaini mwezi juni mkataba unaofikia kikomo mwaka 2024 pia Spurs walimuongeza mkataba wa miaka mitano kocha wao mkuu Mauricio Pochettino..
.
– Spurs Sasa wanahakikisha wanawafunga Wachezaji wao muhimu Kwa Mikataba ya muda mrefu kabla ya kufikia mwaka 2019 na ndio mwaka Ambao wataamia rasmi Katika Uwanja wao wa White Hart Lane uliokuwa Katika ukarabati wa Kuongeza ukubwa ambapo kwasasa wanatumia Uwanja wa Taifa “Wembley Stadium”
USAJILI: TZ Prisons kumsajili mchezaji huyu wa SIMBA P
Imeripotiwa kuwa Klabu ya Tz Prisons ya jijini Mbeya ipo mbioni kumsajili mshambuliaji wa Simba Sc Mohamed Rashid kwa mkopo mara baada ya kumalizika kwa msimu huu.
Mo ni moja ya wachezaji waliokosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Simba sc tangu kuanza kwa msimu huu.
#tanzaniapremierleague🇹🇿
MKATABA WA DDG UNAVYOWAUMIZA KICHWA MAN U
Mkataba wa DDG unavyowaumiza kichwa United – Juventus huenda wakamsaini buree.
:
:
Jose Mourinho amesema hana uhakika juu ya golikipa wake David De Gea kusaini mkataba mpya, DDG mkataba wake na United unaishia mwishoni mwa msimu ujao na taarifa mpya zinadai Juventus ambao wana uzoefu na kusajili wachezaji ‘huru’ wameanza kuvizia saini ya De Gea
.
.
Golikipa huyo mwenye miaka 27 mkataba wake wa sasa unaishia mwishoni mwa msimu wa 2019/20, na sasa inaonekana wazi kwamba Juventus wapo tayari kumsubiri amalizane na United na kumsaini bure kama ilivyokuwa kwa Paul Pogba mwaka 2012
.
.
De Gea amekuwa akitegemewa kusaini mkataba mpya na United kwa muda mrefu sasa tangu Thibaut Courtois alipojiunga na Real Madrid wakati wa kiangazi, lakini mpaka sasa hajasaini mkataba mpya na Mourinho leo amesema hana uhakika na kukamilika kwa dili jipya na United na taarifa mpya zinadai Juventus ambao wameshinda Serie A kwa miaka 7 mfululizo wapo katika nafasi nzuri ya kumshawishi DDG kuhamia Italia
.
.
Chanzo cha karibu na Manchester United kimesema: “De Gea amecheza dhidi ya waajiri wake wajao jumanne iliyopita. Endapo United hawatomuuza dirisha kubwa likifunguliwa, basi Juventus watasubiri mpaka mkataba wake umalizike.”
.
Inaelezwa DDG ambaye alishindwa kuhamia Madrid miaka 3 iliyopita kutokana fax machine ya Madrid kusumbua, ameshindwa kusaini mkataba mpya na United kwasababu anaona muelekeo wa klabu sio mzuri, umri wake unasogea na hakuna mafanikio ya maana aliyopata, hivyo sasa anaangalia machaguo tofauti kabla ya kuamua kukubali au kukataa kusaini mkataba mpya na United.
:
Juventus ambayo imetoka kumsaini Cristiano Ronaldo kwa dau la £99m wana utayari wa kuwalipa United ikiwa klabu hiyo itakubali kumuuza DDG, au watamsubiri mpaka mkataba wake umalizike na kumsaini bure ili aje kuziba pengo liloachwa wazi na Gigi Buffon aliyejiunga na PSG.
:
Katika miaka ya hivi karibuni, Juventus imefanikiwa kusajili bure wachezaji wakubwa ambao wameisadia kwa kiasi kikubwa kuirudisha katika listi ya vilabu bora duniani.
:
Wachezaji waliosajiliwa bure na Juventus
✅ 2009: Fabio Cannavaro
✅ 2011: Andrea Pirlo
✅ 2012: Paul Pogba
✅ 2013: Fernando Llorente
✅ 2014: Kingsley Coman
✅ 2015: Sami Khedira
WACHEZAJI WENYE HISTORIA LIVERPOOL

Wachezaji wawili pekee katika historia ya Liverpool wamefanikiwa kufunga magoli 50 chini ya mechi 80 walizocheza .
.
🔴 Mohamed Salah (65)
🔴 Fernando Torres (72)
Salah the fastest ever. 🙇♂







