
credit: @sokawaytz…
– Eden Hazard amesema kuwa yeye hajali juu kutovaa jezi namba 10 au kutokuwa na majukumu ya kupiga mikwaju ya penalti katika Klabu yake mpya ya Real Madrid; Mshambuliaji huyo wa Kimataifa wa Ubelgiji alijiunga na Blancos kwa €100 (£88m / $112m) kutoka Chelsea wiki iliyopita.
.
— “Nimezungumza na Modric kwa kupitia kwa Kovacic, nikamuuliza kama angeweza kuniachia Mimi jezi No.10, alisema hapana, ni lazima nitafute namba nyingine,” alisema Hazard.
.
— Nyota huyo Pia aliongeza kuwa “Kwangu mimi namba 10 ya jezi si muhimu, lakini kucheza na jezi hii, na nembo hii inatosha”.
.
– Hazard pia amesema hatolazimisha kutaka kuchukua penati ili apige yeye ndani ya Real Madrid, kwani kawakuta wapiga wengine wengi wa penati ndani ya Klabu… Sergio Ramos msimu uliopita alipiga penati Nane Kati ya 12 za Klabu hiyo, Karim Benzema akipiga penati tatu na Gareth Bale akipiga penati moja..
#Updates
@Sokawaytz