Wanachama YANGA: Wamtaka MANJI ajitokeze Hadharani..

Wanachama wa klabu ya Yanga wamemtaka Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusufu Manji ajitokeze hadharani kumaliza utata baada ya Baraza la Michezo (BMT) kuitaka klabu hiyo ijaze nafasi yake.

Jana Wanachama wa Yanga kupitia viongozi wa Matawi walimtaka Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini Mzee George Mkuchika kuitisha Mkutano Mkuu wa dharura ili kumaliza utata wa sakata la Manji

Katibu wa Matawi hayo Boaz Ikupilika alisema kwa kuwa wanachama wa Yanga ndio waliomchagua Manji na baadae kuikataa barua yake ya kujiuzulu, basi ni vyema ukaitishwa Mkutano huo ambao Manji ataalikwa ili kuwaeleza wanachama waziwazi kama amejitoa kwenye uongozi wa Yanga ili wafanye uchaguzi kama ilivyoagizwa na BMT

Yanga imepewa mwezi mmoja kuhakikisha imefanya uchaguzi.

Hata hivyo kumetokea mvutano baina ya wanachama wa klabu hiyo ambapo wengine wametaka kufanyika kwa uchaguzi kama ilivyoagizwa na BMT huku wengine wakipinga uchaguzi kwa kuwa bado wanamtambua Manji kuwa Mwenyekiti wa Yanga

YANGA 1-1 NDANDA FC

Yanga imelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ndanda Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa uwanja wa Taifa.

Ndanda Fc ilitangulia kufunga bao la kuongoza kwenye dakika ya 16 mfungaji akiwa Nasor Hasimu baada ya timu hiyo kufanya shambulizi la kushitukiza.

Yanga ilirejea mchezoni kwenye dakika 24 ilipofanikiwa kusawazisha kwa bao la kichwa lililofungwa na kiungo Jaffar Mohammed aliyeichezea yanga kwa mara ya kwanza leo kwenye ligi

Bao hilo lilitokana na mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajib aliyerejea kwenye kikosi cha Yanga leo baada ya kukosa michezo miwili iliyopita akisumbuliwa na maumivu ya mgongo

Ndanda iliyocheza kwa kujihami zaidi, ilitumia mashambulizi ya kushitukiza ambayo mara kwa mara yalipelekea hatari langoni kwa Yanga na kumlazimu mlinda lango Beno Kakolanya kufanya kazi ya ziada

Kwenye kipindi cha pili Yanga ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi na kupeleka mashambulizi mfululizo langoni kwa Ndanda lakini kukosekana umakini kwa safu ya ushambuliaji iliyoongozwa na Heritier Makambo kuliikosesha Yanga mabao

Matokeo hayo yanaibakisha Yanga katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi licha ya kuwa na alama 26 sawa na Simba inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao.

YANGA: Kusajili Jembe Hili

Yanga imekuwa kwenye mazungumzo na beki kisiki wa Rayon Sports, ambaye ni nahodha wa timu hiyo, Abdul Rwatubyaye

Wakala wa mchezaji huyo alikiri kuwa na mazungumzo na uongozi wa Yanga lakini pia akisema klabu ya Simba nayo imeulizia upatikanaji wa beki huyo mwenye umri wa miaka 23

Kulingana na taarifa zinazoripotiwa na vyombo vya habari nchini Rwanda, Rayon Sport iko tayari kumuachia Abdul kwa kitita cha Mil 80

Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika amekuwa kwenye mazungumzo na wakala wa mchezaji huku ikielezwa tayari pande zote zimefikia makubaliano juu ya usajili wa beki huyo.

Inaelezwa uko uwezekano mkubwa kwa beki huyo kutua Yanga mapema tu dirisha la usajili litakapofunguliwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo

Yanga pia imemalizana na mshambuliaji wake wa zamani Obrey Chirwa ambaye awali aliwekewa ngumu na kocha wa timu hiyo Miwnyi Zahera

YANGA: Yatoa tamko kuhusu BANKA

Baada ya TFF kubainisha kuwa kiungo Mohammed Issa Banka amefungiwa miezi 14 baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kusisimua mwili (bangi), uongozi wa Yanga unasubiri barua rasmi kutoka TFF ili uweze kutoa tamko.

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema baada ya kutolewa kwa taarisa hiyo leo, wanasubiri barua rasmi kutoka TFF ili waweze kutoa tamko la timu.

“Taarifa imetoka leo, hivyo tunasubiri barua rasmi kutoka TFF ili tuzungumze”

“Hata hivyo, hatuwezi kusema kama Banka ameonewa au la kutokana na mazingira ya kesi hiyo. Kwani ushahidi ukiwemo vipimo vilichukuliwa pamoja utetezi wa mchezaji mwenyewe ambaye amekiri kosa”

Banka ametua Yanga akitokea Mtibwa Sugar hata hivyo hakuwahi kujiunga na timu hiyo.

Adhabu yake imeanza Disemba 2017 na itamalizika Februari 02, 2019.

Wakati anajiunga Yanga alisaini mkataba wa miaka mitatu. Anaweza kuanza kutumikia Yanga baada ya miezi minne.

Hata hivyo anaweza akaruhusiwa kuanza kujifua na Yanga kuanzia mwezi Disemba

Banka Afungiwa miezi 14 soka

Kamati ya Kuzuia na Kupambana na Dawa Zisizoruhusiwa Michezoni ya Kanda ya Tano Afrika ( RADO ) imetoa hukumu ya kumfungia mchezaji wa Yanga, Mohamed Issa ‘Banka’ kutokana na matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo alisema Banka amefungiwa miezi 14 kwa kukutwa na hatia hiyo.

Anasema Banka amekuwa na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu aina ya bangi akiwa nchini Kenya.

“Banka alikutwa na hatia hiyo akiwa pale Machakos Kenya katika mashindano ya CECAFA Challenge Cup na kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar, ” alisema.

“Hukumu yake hiyo itaanzia Desemba 9, 2017 ambapo alichukuliwa kwenda kufanyiwa vipimo na itamalizika Februari 2, 2019.

“Banka baada ya kupimwa alikubali kweli alitumia kwa kupitia kwa maandishi yaani barua na baada ya kukutwa na hatia ilitakiwa kufungwa maisha lakini baada ya kukubali alipunguziwa.

“Banka atakiwi kufanya mazoezi ya mbeli ya watu lakini kama atatumikia vizuri adhabu hiyo miezi miwili ya mwisho ataruhusiwa kufanya mazoezi na timu yake, ” alisema.

BANGI Yampozna kiungo wa Yanga Afungiwa Miezi 14

Kamati ya Kuzuia na Kupambana na Dawa Zisizoruhusiwa Michezoni ya Kanda ya Tano Afrika ( RADO ) imetoa hukumu ya kumfungia mchezaji wa Yanga, Mohamed Issa ‘Banka’ kutokana na matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo alisema Banka amefungiwa miezi 14 kwa kukutwa na hatia hiyo.

Anasema Banka amekuwa na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu aina ya bangi akiwa nchini Kenya.

“Banka alikutwa na hatia hiyo akiwa pale Machakos Kenya katika mashindano ya CECAFA Challenge Cup na kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar, ” alisema.

“Hukumu yake hiyo itaanzia Desemba 9, 2017 ambapo alichukuliwa kwenda kufanyiwa vipimo na itamalizika Februari 2, 2019.

“Banka baada ya kupimwa alikubali kweli alitumia kwa kupitia kwa maandishi yaani barua na baada ya kukutwa na hatia ilitakiwa kufungwa maisha lakini baada ya kukubali alipunguziwa.

“Banka atakiwi kufanya mazoezi ya mbeli ya watu lakini kama atatumikia vizuri adhabu hiyo miezi miwili ya mwisho ataruhusiwa kufanya mazoezi na timu yake, ” alisema.

AJIBU kurejea Jumapili dhidi ya NDANDA FC

Mratibu wa klabu ya Yanga Hafidh Saleh amesema kiungo Ibrahim Ajib huenda akarejea kikosini kwenye mchezo wa Jumapili ijayo dhidi ya Ndanda Fc.

Ajib sambamba na Papi Tshishimbi wamekosa michezo miwili iliyopita dhidi ya KMC na Lipuli kutokana na kuwa na matatizo mbalimbali.

Wakati Ajib akisumbuliwa na maumivu ya mgongo, Tshishimbi alikuwa na matatizo ya goti.

Wawili hao walishindwa kutumika kwenye mchezo wa jana licha ya ripoti ya daktari kubainisha utimamu wa afya zao.

Yanga imefanikiwa kushinda michezo yote miwili waliyokosa viungo hao mahiri hivyo kudhihirisha kuwa timu hiyo haitegemei mchezaji mmoja tofauti na inavyodhaniwa na mashabiki wa timu pinzani

Kocha YANGA: Hakuna Mchezo Rahisi

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewapongeza vijana wake kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lipuli Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa jana.

Zahera amesema licha ya timu yake kuibuka na ushindi mwembamba amefurahishwa na upambanaji unaoendelea kuonyeshwa na wachezaji kwenye michezo mbalimbali ya timu hiyo

Amesema kwenye kila mchezo lengo lao la kwanza ni kuibuka na ushindi bila ya kujali idadi ya mabao watakayofunga.

Awapasha waandishi wa habari swala la Ajib

Katika hatua nyingine Zahera amewataka waandishi wa habari kulinganisha taarifa zao na sio kuandika kwa lengo la kufanya uchonganishi

Zahera amesema waandishi wa habari wamekuwa wakiandika zaidi ‘ukosoaji’ wake kwa baadhi ya wachezaji bila ya kuandika mazuri yao

“Nilisema Ibrahim Ajib ni mchezaji mwenye akili nyingi ya mpira kuliko wachezaji wenu wote hapa Tanzania, lakini sikuona mkiandika hilo”

“Mmekuwa mkiandika yale ya kukosoa tu ambayo nayo kimsingi ni ya kumjenga yeye ili awe mchezaji mkubwa,” amesema

Yanga imepanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 25, alama mbili nyuma ya Azam Fc.

Yanga Sc vs Ndanda Fc: Jumapili

Leo Yanga inashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Lipuli Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara raundi ya 12.

Baada ya mchezo huo, Yanga itashuka tena dimba la Taifa Jumapili, Novemba 04 kuikabili Ndanda Fc,

Awali TFF ilitangaza kufuta michezo ya Simba, Yanga na Azam iliyokuwa ipigwe wiki ya kwanza ya mwezi Novemba ili kutoa nafasi kwa wachezaji wa timu hizo walio kwenye kikosi cha Stars kujuishwa kambini nchini Afrika Kusini.

Michezo hiyo sasa itapigwa kama kawaida