HAJI MWINYI: Ajiandaa na Maisha Nje ya YANGA

Beki Haji Mwinyi ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao inamalizika baada ya mchezo wa mwisho wa ligi

Beki huyo aliyeitumikia Yanga kwa zaidi ya miaka minne, atakuwa huru baada ya Yanga kuumana na Azam Fc wiki ijayo

Amezikaribisha timu zinazohitaji huduma yake kwa ajili ya msimu ujao

“Mkataba wangu na Yanga unamalizika msimu huu. Baada ya hapo nitakuwa huru”

“Nakaribisha klabu yeyote inayohitaji huduma yangu kwa msimu ujao waje tukae mezani tuzungumze, lakini kuhusiana na ofa nilizonazo mezani hadi sasa siwezi kuweka wazi hadi hapo nitakapomaliza msimu wangu kwa michezo miwili iliyobaki,” Mwinyi aliiambia Mwanaspoti

“Sikuwa na namba kikosi cha kwanza, lakini hiyo haina maana kwamba kiwango changu kimeshuka, nipo vizuri na nina uwezo wa kupambana. Kutokana na uzoefu nilionao na naweza kucheza timu yeyote”

Haji Mwinyi hakuwa na wakati mzuri msimu huu katika kikosi cha Zahera akishindwa kutamba mbele ya Gadiel Michael aliyekuwa chaguo la kwanza

Yanga imepanga kutowaongezea mikataba wachezaji ambao hawakucheza angalau nusu ya michezo ya ligi kuu msimu huu

YANGA DIMBANI LEO KUIVAA MBEYA CITY

Kikosi cha Yanga leo kinashuka uwanja wa Uhuru kuikabili Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu raundi ya 37

Baada ya Simba kutwaa ubingwa hapo jana, mchezo huo ni wa kukamilisha ratiba tu ambapo mabingwa hao wa kihistoria watakuwa wakilinda heshima yao

Jana Yanga ilifanya maandalizi ya mwisho kwenye uwanja wa Uhuru
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema lengo lao ni kumaliza ligi kwa kushinda michezo yote miwili iliyobaki
Ushindi katika michezo miwili iliyobaki utawafanya wafikishe alama 89 ambazo hata hivyo tayari zimeshapitwa na Simba yenye alama 91

Lakini pia hata kama Yanga itapoteza michezo yote iliyobaki, itaendelea kubaki nafasi ya pili kwani hakuna timu nyingine inayoweza kufikisha alama hizo
Yanga leo inatarajiwa kuwakosa wachezaji saba ambao wanaugua Malaria

Hata hivyo Zahera amesema wachezaji watakaopata nafasi ya kucheza, anaamini wataweza kuipa timu hiyo ushindi
Baada ya mchezo wa leo, Yanga itashuka tena dimbani wiki ijayo May 28 kumaliza msimu kwa kuumana na Azam FC

ZAHERAC: Amlilia AJIBU Kwenda TP MAZEMBE

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amemwambia nahodha na mshambuliaji wa klabu hiyo Ibrahim Ajibu kufikilia mara mbili kuhusu kuihama klabu hiyo mwisho wa msimu huu. Imeelezwa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Zahera amedai Ajibu ni kiongozi wa wenzake na hapaswi kuwa na mawazo ya kuondoka Yanga na kuwaacha wenzake.

Mkataba wa Ajibu na Yanga unaisha mwisho wa msimu huu na inadaiwa kuwa atajiunga na klabu ya Simba baada ya mkataba wake kuisha na Yanga.

Taarifa za Ajibu kuondoka Yanga zimeanza muda mrefu uliopita na kuleta sintofahamu kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kutokana na namna mwenendo wa klabu ulivyo.

Zahera amemuomba Ajibu afikirie zaidi ya mara moja kuhusiana na kuondoka kwake kwa manufaa ya Yanga maana anaheshimu mchango wake.

AJIBU Kutimkia TP MAZEMBE

TP Mazembe itamsajili kiungo wa Yanga Ibrahim Ajib Migomba akitarajiwa kujiunga na timu hiyo Julai 01 2019

TP Mazembe imeiandikia barua Yanga kuitaarifu juu ya nia ya kutaka kumsajili kiungo huyo.

Mazembe itamsajili Ajib baada ya kumaliza mkataba na Yanga

Aidha TP Mazembe imeiomba Yanga impe ruhusa ya siku tatu wiki hii ili aweze kwenda Congo kukamilisha taratibu za usajili

Hii ni habari njema kwa Ajib ambaye msimu huu umekuwa mzuri sana kwake

Ajib ameifungia Yanga mabao sita na kutengeneza mabao 17 kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara inayoelekea ukingoni

YANGA: Kuisimamisha DAR June 15

Harambee kubwa ya kuichangia Yanga itafanyika Juni 15 katika ukumbi wa Diamond Jubelee jijini Dar es salaam

Siku hiyo ndio itakuwa kileleni cha kampeni ya kuichangia Yanga iliyoanza takribani miezi miwili iliyopita

Wananchi wa kawaida, Wasanii, Wanamuziki, Wabunge, viongozi wa Serikali,Taasisi Binafsi na Mashirika watahudhuria hafla hiyo ambayo Kamati ya Hamasa inakusudia kukusanya zaidi ya Tsh Milioni 500

Mwana Jangwani weka kumbukumbu ya tarehe hiyo….!

TSHISHIMBI: Aipotezea Azam Fc

Wakati mkataba wake ukielekea ukingoni, kiungo Papi Kabamba Tshishimbi amesema hafikiri kujiunga na timu nyingine Tanzania kama atashindwa kufikia makubaliano na Yanga

Tshishimbi aliyetua Yanga miaka miwili iliyopita akitokea Mbabane Swallows ya eSwatini, amekuwa akihusishwa kuwaniwa na Azam Fc

Hata hivyo amesisitiza Yanga ndio timu pekee ambayo atachezea kwa hapa Tanzania

“Mimi ni mchezaji wa Yanga na hata mkataba utakapomalizika timu nitakayofanya nayo mazungumzo ni Yanga,” amesema

“Ni kweli zipo timu zimewasilisha ofa, lakini nitazungumza na Yanga kwanza kama tukishindwana basi nitazipa kipaumbele ofa za nje ya Tanzania”

Kwa siku za hivi karibuni Tshishimbi amekuwa katika kiwango bora akiwa amefunga mabao manne kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara

Hakuna shaka atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaopewa mikataba mipya katika kikosi cha Yanga

YANGA : Wachezaji wagonjwa

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema wachezaji saba wa kikosi cha Yanga hawataweza kucheza kesho mchezo dhidi ya Mbeya City baada ya kukumbwa na Malaria

Wachezaji hao ambao hawakufika kufanya mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Uhuru leo ni pamoja na Abdallah Shaibu, Andrew Vicent, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Said Makapu, Mohammed Issa na Paulo Godfrey

“Nadhani timu yetu imekumbwa na janga la Malaria, tuna wachezaji karibu saba ambao wanaugua Malari,” amesema Zahera

“Sijui ni kama walikula nini sijui”

Akizungumzia mchezo wa kesho, Zahera amesema hautakuwa mwepesi kutokana na ubora wa kikosi cha Mbeya City

“Tuliwafunga mchezo wa kwanza, lakini wachezaji ilibidi wajitume sana kuweza kupata matokeo,” amesema

“Kesho pia mchezo hautakuwa tofauti lakini nafurahi wachezaji wangu wamepata muda mrefu wa kupumzika hivyo watakuwa ‘fresh'”

“Kwa wale watakaocheza lengo letu ni moja, tumalize mechi mbili zilizobaki kwa kuibuka na ushindi”

NOEL MWANDILA OUT YANGA

NOEL MWANDILA OUT YANGA -Mwenyikiti wa klabu ya Yanga, Dr Mbette Mshindo Msolla amethibitisha kuwa wataachana na kocha msaidizi wa klabu hiyo Noel Mwandila na kuajiri kocha msaidizi mzawa ili aweze kumsaidia kocha Mwinyi Zahera. -Akiongea kuhusu kuibadili Yanga amedai wafanyakazi wote wa Yanga na watu wa bechi la ufundi isipokuwa kocha mkuu Mwinyi Zahera wanatakiwa kutuma CV zao upya kwa uongozi mpya ili kufanyiwa kazi na kila mtu afanye kazi anayostahili. -Kuhusu kocha Msaidizi Mwenyekiti alisema “Benchi la ufundi linahitaji kuwa na kocha msaidizi mwenye kiwango kizuri ili kuongeza nguvu ndani ya kikosi chetu, tutaangalia zaidi kocha mzawa ili aweze kuwa sambamba na kocha Zahera kufanya kazi.” “Katika nchi za wenzetu zilizoendelea kocha mkuu amekuwa akimtumia zaidi kocha msaidizi kwa kumtuma kwa ajili ya kwenda kufuatilia wachezaji wanaowahitaji kwa ajili ya kuwasajili hata ikiwa nje ya nchi ambaye anafuatilia mechi na mazoezi anayofanya mchezaji, hivyo tunahitaji msaidizi mwenye weredi atakayeshirikiana vyema na kocha mambo mbalimbali” “Tukiachana na kazi ya kutafuta kocha, pia tutawatumia wachezaji wa zamani waliowahi kuichezea Yanga kuweza kuwatuma mikoani kwa ajili ya kusaka vipaji,”
Alisema Dr. Mshindo Msolla -Noel Mwandila alijunga na klabu ya Yanga misimu miwili iliyopita kama kocha wa viungo chini ya kocha George Lwandamina ila baada ya kuondoka kwa Lwandamina na Shadrack Nsajingwa ndio akawa kocha msaidizi wa klabu ya Yanga.
.
Cc : Yossima Sitta Jr

Mwinyi Zahera amesema lengo la kwanza la kikosi chake msimu ujao ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema lengo la kwanza la kikosi chake msimu ujao ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu

Yanga imeshindwa katika mbio za kuwania ubingwa msimu huu na wapinzani wao Simba ambao wanahitaji alama moja tu kutoka michezo mitatu

Hata hivyo licha ya kumaliza katika nafasi ya pili, Zahera amesema timu yake imefanikiwa kulingana na mazingirwa waliyokuwa nayo

“Tulianza kwa kuwa na malengo ya kumaliza nafasi ya sita au saba, lakini baada ya kuona tunafanya vizuri licha ya kuwa na changamoto nyingi, tukasema tujaribu kuwania ubingwa,” amesema Zahera

“Bado naamini tulistahili kushinda kombe kama sio kudhurumiwa baadhi ya michezo”

“Sasa nafurahi timu imepata viongozi, nimewaambia wajipange. Hatutaki tena haya ya mwaka huu yatukute msimu ujao”

“Tunahitaji kuwa na timu imara itakayoshinda na kutwaa ubingwa mapema”

Zahera amesema huu ukiwa msimu wake wa kwanza Tanzania, umemsaidia kufahamu ushindani wa ligi, aina ya wachezaji anaowahitaji na mbinu gani atumie ili kuweza kufanya vizuri

“Tutatengeneza timu imara, tutasajili wachezaji wa kiwango cha juu ambao watafanya timu yetu iwe kali sana msimu ujao”