Kikosi bora cha msimu huu mwaka 2018-2019 na Kagawa 10

Makala

TUONGEE KUHUSU MPIRA na kagawa10.

KIKOSI BORA CHA MSIMU KUTOKA KATIKA TIMU 20 ZA LIGI KUU(TPL) 

   Wakati ligi kuu ikielekea ukingoni siku ya leo, nimeona nitoe kikosi bora ambacho kitajumuisha wachezaji waliofanya vizuri katika ligi kuu ya Tanzania(tpl),wachezaji ni wengi waliofanya vizuri katika ligi yetu ya bongo ambayo inachangamoto nyingi sana hila wachezaji wamejitaidi kuonesha uwezo wao.  Kikosi hiko kipo kama hivi

1. Aishi manura (simba) 

2. William lusian gallas ( lipuli) 

3. Bruce kangwa(azam) 

4. Erasto nyoni (simba)  

5. Kelvin yondani (yanga)  

6. Feisal Toto ( yanga)  

7. Clastus chota chama (simba)  

8. Jonas gerrald mkude (simba) 

9. Meddie kagere (simba)  

10. Herriet makambo (yanga)  

11. Ibram ajibu migomba (yanga)  

Sub

1.Aron kalambo ( prison) 

2. Hussein zimbwe (simba)  

3. Salim ayee (mwadui)  

4.Yakubu (azam)  

5. Jonh Boko (simba)  

6. Emmanuel okwi (simba)  

7. Aggrey morris. 

Wengi watajiuliza kwanini ajibu nimemuweka kwenye kikosi,  jibu lao ni hivi namba hazidanganyi naazaje kumuweka nje mtu anaeongoza kwa kusaidia upatikanaj wa magoli(assist 15) kwa msimu huu japo mech nyingi alikua ayupo kutokana na matatizo binafsi na timu yake, pia kumuweka jonas mkude kama namba nane wakati asili yake ni kiungo mzuiaji,  inatoka na kutumika sana eneo ilo na kufanya vizuri katika msimu uku nyuma yake akiwa saidiwa na james kotei napenda kumwita chuma. 

Yote kwa yote wachezaji ni wengi hila kwangu hao nimeona wamefanya vizur sana kwa msimu mzima. 

Makala hii imeandikwa na kagawa 10.

Aston Villa yarudi ligi kuu ya uingereza

– Aston Villa imefanikiwa kupanda Ligi Kuu Nchini Uingereza “Premier League” Baada ya ushindi wa Magoli 2-1 dhidi ya Derby Country mapema siku ya jana, katika Mafanikio hayo waliyopata kwa Mara ya kwanza takribani miaka Mitatu kwa Kiasi kikubwa imechangiwa na Wachezaji kutoka Bara La Afrika.

.

– Mfungaji bora wao Tammy Abraham licha tu ya kuichezea timu ya taifa ya England U21 lakini Nigeria wameendelea kumshawishi kurejea nyumbani kabla ya kuanza kucheza Senior team Moja kwa Moja, Mshambuliaji Anwar El Ghazi licha tu ya kuichezea timu ya taifa ya Uholanzi U21 Morocco hawajaacha kumshawishi kurejea nyumbani, Beki na nahodha wa Misri, Ahmed Elmohamady, Albert Adomah wa Ghana wa Nyota wa Ivory Coast, Jonathan Kodjia wameisaidia Aston Villa kwa kiasi chake kuhakikisha imerejea Ligi Kuu… Baada ya wao kupanda wanahitimisha Timu tatu Baada ya Mbili kutangulia ambazo ni Norwich City na Sheffield United.

.

– Magoli kutoka Kwa, Anwar El Ghazi na John McGinn yaliweza kutosha na kuwapandisha PL vijana hao wa kocha Dean Smith katika Dimba la Wembley, Martin Waghorn aliwafuta machozi Derby kwa Goli lake Dakika 10 za Mwisho wa Mchezo huo..

#Updates

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz

Daniel Alves apewa unahodha timu ya taifa ya Brazil

– Imethibitisha Rasmi, Dani Alves ndiye nahodha mpya wa timu ya taifa ya Brazil katika Michuano ijayo ya Copa América, Kocha Tite kampiga chini Staa wao, Neymar Jr ambaye alimpa kitambaa hicho mwaka jana kuwa nahodha wa Brazil.

:

Brazil wanatarajia kuwa wenyeji wa Copa America, Mabingwa hao Mara Nane Mara ya mwisho mwaka 2016 walifanya vibaya lakini mwaka huu wakiwa kundi A pamoja na Bolivia , Peru na Venezuela watajaribu kufanya vema zaidi, Brazil game yao ya kwanza katika Michuano hii wataanza na Bolivia ndani ya Sao Paulo siku ya June 14..

#Updates

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz