Kiungo wa zamani wa Barcelona xavi awa kocha mkuu wa al sadd sc nchini quatar

– Kiungo wa zamani wa Klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Xavi Rasmi ametangazwa kuwa kocha mkuu wa Klabu ya ligi Kuu nchini Qatari , Al Sadd SC kwa Mkataba wa Miaka miwili.

.

– Xavi 39, amecheza game zaidi ya 100 akiwa na Al Sadd kabla ya kutangaza kustaafu mwishoni mwa msimu wa 2018-19, Miaka Mitatu tangu ajiunge na Klabu hiyo.

.

– Xavi, katwaa Ubingwa wa Kombe La Dunia 2010 akiwa na Hispania, Mataji Nane ya Laliga, Mataji Manne ya Champions League Kipindi akiwa na FC Barcelona… 👏👏👏

#Updates

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz

Neymar avuliwa unahodha Brazil ,Daniel Alves apewa Kitambaa

– Siku Baada ya Kuvuliwa unahodha, Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar Jr ameondolewa katika Viwanja vya Mazoezi ya timu hiyo ya taifa Baada ya kupata Majeraha ya mguu wake wa kushoto.

.

– Kocha Tite alitangaza kumpa kitambaa cha unahodha Neymar mwaka jana, na Sasa ameamua kumvisha Dani Alves ambaye atawaongoza wenzake katika fainali za Copa America mwezi ujao wao wakiwa wenyeji.. Neymar alionekana kujilazimisha kufanya mazoezi lakini haikiwa nzuri na baadade Daktari wa timu hiyo ya taifa Rodrigo Lasmar alipoamua atolewe kwenda kufanyiwa uchunguzi zaidi..

#Updates

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz

Kocha wa Ac Milan Gennaro Gattuso ajiudhulu

– Klabu ya AC Milan Imethibitisha kuwa, Gennaro Gattuso ameachana Rasmi na klabu hiyo Kama kocha Mkuu kwa Makubaliano maalumu; Gattuso ameiongoza Milan tangu Novemba 2017, uhamuzi huo kautoa Baada ya Klabu hiyo kushindwa kufuzu kushiriki Michuano ya @championsleague msimu ujao, wakimaliza nafasi ya tano katika Msimamo wa Serie A na kuangukia @europaleague.

.

– Gattuso 41; alisema hatma yake atatoa Baada ya Ligi kumalizika Baada ya game yao dhidi ya SPAL wakishinda 3-2, lakini ushindi wao haikuwafanya kuwashusha Wapinzani wao Inter Milan pamoja na Atalanta waliokuwa wakiwania nao nafasi mbili zilizosalia ukitoa Juventus na Napoli walijihakikishia kufuzu kwa muda mrefu.

.

– Kocha wa Monaco, Leonardo Jardim na kocha wa Lazio, Simone Inzaghi, Sasa wanatajwa kuchukua huenda mmoja wao akatua San Siro; Kwa Kuongeza, Milan Imethibitisha Kwa Mkurugenzi wao wa Michezo, Leonardo nae ametimka Baada ya msimu mmoja kudumu Klabuni hapo.. Anatajwa kutimkia Paris Saint-Germain ambako amewahi kufanya kazi hiyo kabla ya kutua Milan.

#Updates

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz

Adi Yusuf mchezaji wa kitanzania aliyesajiliwa blackpool uingereza

– Blackpool imefanya usajili wake wa kwanza Dirisha hili La Uhamisho kwa kumnasa Mshambuliaji waKimataifa wa Tanzania, Adi Yussuf. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amesaini mkataba wa miaka miwili na Kipengele cha kuongeza mwaka mwingine kuwa Mitatu; Hii imekuja baada ya mkataba wake na Klabu ya Solihull Moors kumalizika.

.

– Katika Kipindi chote cha Mwaka Mmoja na Nusu akiwa na klabu hiyo ya Daraja la tano, Alifunga mabao 21 katika mashindano yote ya Klabu hiyo.. Amejiunga na Blackpool inayoshiriki League One sawa na Daraja La tatu katika mfumo wa Mzima wa Ligi Nchini Uingereza.

.

– Akiongea Baada ya “kusinyaa” Amesema.

— “Hii ni ndoto ya kweli kwangu.” “Jitihada zangu na kufanya kazi kwa bidii, hatimae mafanikio yangu yameonekana, natoa shukrani kwa kila mtu aliyeniamini na kwa kila mmoja ndani ya Solihull, “Ninataka tena kuwa na uhusiano na kila mtu Kipindi nitakacho kaa hapa.”.

— “Nilipoweza kufanya kazi katika Solihull. Nina hakika niweza kufanya kazi katika Ligi hii” Aliongeza Yussuf.

.

– Yussuf alianza kusakata Soka katika Timu ya Pili ya Leicester City, na Mpaka anajiunga na Blackpool, katimiza jumla ya vilabu 14 tofauti katika vilabu vyote hivyo timu 5 alicheza kwa mkopo. Nyota huyo anatarajia kutua nchini Moja kwa Moja ataingia kambini katika timu ya taifa ya Tanzania kwa Maandalizi ya AFCON 2019..

#Updates #transfers

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz

Yanga yakamilisha usajili wa kiungo mnyaruanda Patrick papy sibomana

✍🏻 Kumekucha Jangwani, Klabu ya Yanga SC Imekamilisha Usajili wa kiungo wa Kimataifa wa Rwanda, Patrick Papy Sibomana kwa Mkataba wa Miaka Miwili akitokea Klabu ya kwao Rwanda, Mukura Victory.

:

✍🏼 Sibomana 22, Aliwahi kuitumikia Klabu ya APR FC ya kwao Rwanda, mwaka 2017 akasaini Mkataba wa kuitumikia Klabu ya Shakhtyor Soligorsk ya Nchini Belarus kisha kurejea Rwanda mwaka huu na kutua Mukura na kisha Sasa Yanga SC ya Tanzania.

:

✍🏼 Nyota huyu ni Miongoni mwaka Wachezaji wanaounda timu ya taifa ya Rwanda “Amavubi” akiichezea timu hiyo tangu mwaka 2013 mpaka Sasa, Kafunga Magoli mawili na Moja ya Goli lake aliifunga Taifa Stars katika Mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki Tanzania ikipoteza 2-0 mwaka 2015 ndani ya Dimba La Amahoro Stadium, Kigali..

#Updates #transfers

@Sokawaytz

credit: @sokawaytz