Full Time
Hiki hapa Kikosi cha Yanga dhidi ya Ndanda leo
Kikosi cha Yanga dhidi ya Ndanda leo
- Klaus Kindoki
- Paul Godfrey
- Jaffary Mohammed
- Andrew Vincent
- Kelvin Yondani
- Feisal Salum
- Mrisho Ngassa
- Papy Tshishimbi
- Heritier Makambo
- Amis Tambwe
- Pius Buswita
- Ibrahim Hamid
- Haruna Moshi
- Gustapha Simon
- Raphael Daud
- Said Juma Makapu
- Deus Kaseke
- Thaban Kamusoko
Magazeti ya leo, Alhamis, March 07 2019



















Alikufa Al Ahly uwanja Taifa, Vita ni nani
Simba inahitaji ushindi wa aina yoyote kwenye mchezo huo ili iweze kutinga robo fainali ya michuano hiyo kwa mara ya pili katika historia yake
Simba iliwahi kutinga robo fainali ya michuano hiyo mwaka 1974
Kwenye msimamo wa kundi D JS Saoura inaongoza ikiwa imejikusanyia alama nane ikifuatiwa na Al Ahly yenye alama saba sawa na Vita Club ambayo inashika nafasi ya tatu
Simba inashika nafasi ya nne ikiwa na alama sita
Bila ya kujali matokeo kati ya Al Ahly dhidi ya JS Saoura, ushindi utaihakikishia Simba kufikisha alama tisa na kujihakikishia moja ya tiketi mbili za kutinga robo fainali
Habari njema kwa Simba ni kwamba itakuwa ikicheza mchezo huo mbele ya mashabiki wake ambapo mkakati uliopo ni kuhakikisha siti zote elfu 60 katika uwanja wa Taifa zinakaliwa
Simba imejijengea rekodi ya kipekee inapocheza uwanja wa Taifa.
Msimu huu imefanikiwa kushinda michezo yake yote iliyocheza kwenye dimba hilo katika michuano ya ligi ya mabingwa
Miongoni mwa timu ambazo zilichezea kichapo ni Al Ahly, mabingwa mara nane wa taji la ligi ya mabingwa na vigogo wa soka barani Afrika
Al Ahly iliifunga Simba mabao 5-0 katika mchezo wa duru ya kwanza lakini ilishindwa kufua dafu ilipokuja ‘kwa Mkapa’
Morali hiyo iliyotumika kwa Al Ahly ndio hiyo itakayotumika kuimaliza Vita Club ambayo pia ilishinda kwa mabao 5-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa DR Congo
Katika mchezo huo Simba haina cha kupoteza, kwani matokeo yoyote tofauti na ushindi yataiondosha mashindanoni.
Hivyo hakuna shaka vijana wa Aussems watacheza mpira wa kushambulia mwanzo mwisho
Kocha Patrick Aussems amewaalika mashabiki wote wa soka Tanzania kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa Jumamosi ili kuweza kuandika Historia pamoja na Simba
Nasumbuliwa na nyonga, hayo mengine tuyapuuze – Ajib

Ajib hakujumuishwa kwenye kikosi cha Yanga ambacho kiko Mtwara kesho kikitarajiwa kucheza na Ndanda Fc. Pia alikosa mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Alliance Fc
Aidha kuhusu taarifa zinazotawala katika vyombo vya habari kuwa yuko mbioni kurejea Simba, Ajib amesema ukweli au uongo wa taarifa hizo utafahamika msimu ukimalizika
“Mimi nina mkataba na klabu ya Yanga, nitaendelea kuitumikia timu yangu. Hizo taarifa za mimi kusajiliwa na Simba ukweli au uongo wake utafahamika mwishoni mwa msimu”
“Mimi ni mchezaji wa Yanga ni vyema nikaulizwa mambo yanayoihusu Yanga, hayo mengine tuwaachie wanaotumia kalamu zao kujinufaisha kwa kuuza magazeti lakini ifahamike mimi ni mchezaji wa Yanga,” Ajib amenukuliwa na Mwanaspoti
Kwa siku za karibuni baadhi ya magazeti yameripoti kuwa Ajib tayari amemalizana na mabosi wa Simba ambao wamemtengea mkataba wa miaka miwili
Hata hivyo hivi karibuni kaka yake Athumani Ajib ambaye ndiye wakala wake, alikanusha taarifa hizo huku akibainisha kuwa wamefanya mazungumzo ya mkataba mpya na Yanga lakini wamekubaliana ni vyema wakasubiri mpaka mwishoni mwa msimu ndio aweze kusaini mkataba mpya
Ni kawaida kwa wachezaji wa soka Tanzania kusubiri mikataba yao imalizike kabisa kabla ya kusaini mikataba mipya.
Utaratibu huo wamekuwa wakiutumia ili kujiongezea thamani hasa inapotokea timu zaidi ya moja zimewasilisha ofa ya kutaka kuwasajili
Gadiel arejea kutoka Afrika Kusini

Gadiel aliondoka wiki iliyopita kwenda Afrika Kusini baada ya kupata mwaliko kutoka Bidvest
Bado hakuna taarifa iliyotolewa kama amefuzu majaribio hayo au la
Kamati Maalum Yanga kutua Bungeni, kutambulishwa Dodoma

Tarehe 06/04 kutafanyika uzinduzi rasmi wa kuichangia Yanga.
Tukio hilo la aina yake litaanza saa 12:00 jioni katika ukumbi wa Morena Hotel iliyopo Dodoma huku likiwa mubashara Azam 2 Tv, Kiingilio hakikisha umevaa jezi ya Yanga tu.
Wasanii wafuatao wapenzi wa Yanga watakuwepo makao makuu ya nchi ili kuratibu shughuli hiyo, Mhogo Mchungu, Mr Blue, Msaga Sumu, Single Mtambilike, Wema Sepetu, Haji Mbotto, Rado, Riyama, Uwoya, Madee, Papii Kocha, Ray Kigosi, Frola Mvungi, Kajala Masanja, Barafu, Chopa Mchopanga.
Wengine ni Kalapina, Rich One, Batuli, Haji Adam, Jacqueline Wolper , Yussuf Mlela ,Stamina,Esha Buheti, Steve Nyerere, Chuchu Hans, Dude, Shamsa Ford, Johari, mtangazaji Zamaradi Mketema, MC Pilipili, Seneta Msungu!
Hafla hiyo ya uzinduzi pia itahudhuriwa na watu maarufu na mashuhuri katika medani tofauti
Zahera aahidi ushindi mchezo dhidi ya Ndanda Fc

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake, Zahera amesema baada ya kufanya mazoezi kwa takribani siku mbili Mtwara, vijana wake wako tayari kwa ajili ya mchezo wa leo
“Nafurahi tumefanya maandalizi mazuri. Wachezaji hawakupata matatizo tangu tulipowasili hapa Mtwara,” amesema
“Hali ya hewa ni joto sawa na Dar es salaam, hivyo haiwezi kuwa changamoto kwetu
“Juzi jioni tulifanya mazoezi ya kuondoa uchovu jana pia tulifanya mazoezi mepesi ya kunyoosha minofu. kikosi changu kipo sawa kuelekea mchezo wa leo”
Yanga inasaka ushindi muhimu leo ili iendelee kuchimbia kileleni mwa msimamo wa ligi
Magazeti ya leo, Alhamisi, April 04 2019

















Mazembe yatua nchini, yapitia Mbeya

Mazembe imekuja nchini kwa kutumia ndege binafsi ambapo timu hiyo kabla ya kuja jijini Dar es salaam ilitua kwa muda mkoani Mbeya
Simba leo ilitarajiwa kucheza na JKT Tanzania mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Hata hivyo mchezo huo uliahirishwa baada ya mvua kubwa iliyonyesha mapema mkoani Morogoro kujaza maji kwenye uwanja wa Jamhuri
Simba sasa inaelekeza nguvu zake kuelekea mchezo dhidi ya TP Mazembe








